Pete ya uke huingizwa kwa njia gani?

Pete ya uke huingizwa kwa njia gani?
Pete ya uke huingizwa kwa njia gani?

Pete ni rahisi kutumia. Unapaswa tu kukumbuka siku ya kuiingiza na siku ya kuitoa. Pia unapaswa kuridhika na mwili wako.Ikiwa hauwezi kuweka vidole vyako ndani ya uke wako, pengine pete sio chagua bora kwako. Ni kama kuweka tamponi. Ikiwa unaweza kufanya hivyo, basi unaweza kujifundisha kutumia pete.

Pete ya ukeni huingizwa wakati wowote wa mzunguko wa hedhi yako. Hata hivyo, kuiingiza siku ya kwanza ya hedhi yako itaifanya ipate ufanisi mara hio hio. Ukiiweka wakati mwingine wowote, utahitaji kutumia njia ziada ya uzuiaji mimba kwa sibu saba za kwanza.

Kabla ya kupata njia hii ya uzuiaji mimba, ni muhimu kutembelea mtoa matibabh2u wako kwa uchunguzi wa kiafya ili kubaini ikiwa itakufaa. Katika nchi zingine, utahitaji maagizo ya daktari kabla ununue pete ya uke ya kuzuia mimba.

Kuingiza pete ya ukeni

Kuanzia, nawa mikono yako kwa sabuni na maji. Wacha yakauke yenyewe kwa upepo. Ya kufuata, jiweke jinsi unahisi ukiwa umestareheka, kwa mfano, kusimama ukiwa umeweka mguu mmoja juu, kuchuchuma au kulala chini. Kuingiza pete ndani, ishikilie kati ya kidole gumba na kidole cha shahada na uingize jinsi unavyo weza kuingiza tamponi. Itasimama kwenye pande ya ukuta wa uke wako. Pahali inaposimama kwenye ukuta wa uke haijalishi, bora haikuumizi. Pia unaweza kutaka kujaribu mbinu ya “kupinda” ambamo unapinda pete ili kuiingiza.

Tofauti na kikombe cha hedhi au dayaframu, pete ya uke sio lazima ifunike mlango wa tumbo la uzazi (shingo ya kizazi) ili ifanye kazi. Ikiwa pete inafanya una hisi hauna starehe, isukume ndani zaidi ya uke hadi uhisi una starehe.

Sio lazima utoe pete wakati unafanya ngono na pia haipendekezwi. Hata hivyo, ikiwa unataka kufanya hivyo, ni sawa kuitoa ukifanya ngono, kuiosha au kwa sababu zingine zozote lakini hakikisha tu kwamba unairudisha ndani ya saa 48.

Mara umeingiza pete, inapendekezwa uiwache ndani kwa wiki tatu. Itoe mwanzo wa wiki ya nne [3]

Jinsi ya kutoa Pete ya Uke

Kutoa pete ya ukeni, ingiza kidole ushike upindo wa chini wa pete na uivute nje. Iweke ndani pakiti ilinunuliwa nayo na uitupe pa kutupa takataka-epuka kuitupa kwenye choo cha maji. Iwache nje kwa wiki moja, kisha ingiza pete mpya na uanze mzunguko tena.

Pete ikishatoka nje, huenda ukapata hedhi yako.Usijali ikiwa bado unatokwa na damu ikifika wakati wa kuweka pete mpya.Hili ni la kawaida na hedhi yako itaisha punde.

Ni nini itafanyika nikisahau kutoa Pete ya Uke?

Ukisahau kutoa pete baada ya wiki tatu na ukaiwacha ndani hadi wiki ya nne, hakuna chochote maalum unapaswa kufanya. Itoe tu na uendelee na mzunguko mpya ilivyopangwa.

Ikiwa pete ya uzuiaji mimba imewachwa ndani kwa zaidi ya siku saba za ziada, itoe punde iwezekanavyo, na uweke mpya mara hio hio. Kisha tumia njia ziada ya uzuiaji mimba, kama kondomu, kwa siku saba za kufuata.

Bado unaweza kufanya ngono na utumie tamponi wakati pete iko ndani. Ingawa mwenza wako anaweza kuhisi pete wakati wa ngono, haitamdhuru kwa njia yoyote [4].

Ni kwanini Pete yangu ya kudhibiti mimba inatoka toka?

Unapswa kuwa na uwezo wa kuangalia uwepo wa pete kutumia kidole chako. Ukipata pete yako ikitoka, kuna uwezo mkubwa kwamba hauingizi sahihi. Ikiwa pete itateleza nje, isuuze ndani ya maji safi, na uiingize tena mara moja.

Ikiwa una hakika pete iko ndani ya uke lakini hauihisi, tembelea mtoa matibabu kwa usaidizi. Hakuna jinsi pete ya uzuiaji mimba inaweza kupotea ndani ya uke.

Contraception Quiz

Not sure on the method? - Take our dynamic Contraception Quiz.
When it comes to sex, protection is as important as pleasure. But what should one do to start their safe sex journey? Answer some simple questions and based on the responses, we will recommend the next steps.

Take the quiz
External Condom

Compare with similar Contraceptive Methods

Are you wondering if condoms are better than daily pills? Or if you should opt for a birth control implant? We're here to assist you in making this decision. You can select up to 5 contraceptive methods and compare them side by side to weigh the pros and cons of each.

Give a try to our Contraceptive Tool

In the example below, you'll find similar methods to the one you're currently reading about. Feel free to click on any that catch your interest or revisit our Contraceptive Methods page

Our Monthly Top Articles

Mnong’onezaji wa mambo ya uke: Jinsi ya kupenda uke wako hivyo ilivyo

Mnong’onezaji wa mambo ya uke: Jinsi ya kupenda uke wako hivyo ilivyo

Kabla tuzungumzie mambo ya kuthamini uke, tucheze mchezo ambapo una alama 50 kutoka mwanzo. Nina orodha ya maswali 5 na ikiwa umawahi fanya kile kilichoulizwa kwenye swali, unapoteza alama 10. Twen...

Njia 6 tunaweza kuchukua udhibiti wa uzazi wa mpango kama wanaume

Njia 6 tunaweza kuchukua udhibiti wa uzazi wa mpango kama wanaume

Ingawa ngono salama ni jukumu la wanaume na wanawake, mambo ya uzazi wa mpango imechukuliwa tangu kitambo  kama jukumu la mwanamke. Ingekuwa wanaume wangechukua jukumu la kutumia njia za kuzuia mim...

Mnong’onezaji wa mambo ya uke: Jinsi ya kupenda uke wako hivyo ilivyo

Mnong’onezaji wa mambo ya uke: Jinsi ya kupenda uke wako hivyo ilivyo

Kabla tuzungumzie mambo ya kuthamini uke, tucheze mchezo ambapo una alama 50 kutoka mwanzo. Nina orodha ya maswali 5 na ikiwa umawahi fanya kile kilichoulizwa kwenye swali, unapoteza alama 10. Twen...

Njia 6 tunaweza kuchukua udhibiti wa uzazi wa mpango kama wanaume

Njia 6 tunaweza kuchukua udhibiti wa uzazi wa mpango kama wanaume

Ingawa ngono salama ni jukumu la wanaume na wanawake, mambo ya uzazi wa mpango imechukuliwa tangu kitambo  kama jukumu la mwanamke. Ingekuwa wanaume wangechukua jukumu la kutumia njia za kuzuia mim...

Yote unayostahili kujua kuhusu uelewa wa kizazi kama njia ya uzuiaji mimba

Yote unayostahili kujua kuhusu uelewa wa kizazi kama njia ya uzuiaji mimba

Je unafanya ngono mara kwa mara? Unatumia njia gani ya uzuiaji mimba? Umesikia kuhusu njia ya uelewa wa kizazi? Wanawake wengi duniani kote wanafanya ngono kwa sababu tofauti na kupata watoto. Hawa...