Kufunga mirija ya uzazi ni nini?
Kufunga mirija ya uzazi pia inayojulikana kama “kutasisha mirija”, “kutasisha mwanamke,” “Kufunga mirija miwili”, “njia ya uzuiaji mimba kwa upasuaji wa hiari” ‘mini lap’, “tubectomy”, “oparesheni” au “kufunga mirija yako,” ni aina ya uzuiaji mimba ya kudumu ambayo huziba mirija ya uzazi ili kuzuia mwanamke kushika mimba. Ni utaratibu wa upasuaji unaotolewa kwa watu ambao hawana nia ya kupata watoto au watoto zaidi kama tayari ni mzazi (1).
Neno mrija linamaanisha mrija ya falopa. Yai ambalo limewachiliwa na ovari husafiri kufikia mji wa mimba kupitia mrija wa falopa.
Neno kufunga linamaanisha kuziba au kubana kitu kwa fundo. Kufunga mirija ya uzazi huzuia yai kusafiri kupitia mrija kukutana na manii kwa urutubisho.
Sawa na vasektomi (njia ya uzuiaji mimba ya kudumu kwa wanaume), kufunga mirija kunanuiwa kutoa kinga dhidi ya mimba kwa njia ya kudumu, ya muda mrefu, na yenye ufanisi wa juu. katika hali nyingi, upinduliaji hauwezekani na jaribu lolote la upinduliaji huwa ngumu, ghali na halipatikani kwa urahisi. Hata kama upasuaji wa upinduliaji utafanyika, hakuna hakikisho kuwa utashika mimba. Ni asilimia 50-80 tu ya watu ambao mirija yao imefunguliwa tena wataweza kushika mimba (2).
Ni kwa hali gani kutasisha mwanamke huwa chaguo bora?
-Kama mimba itasababisha matatizo mabaya ya kiafya.
-Kama kuna sababu ya kiafya kwanini wewe au mwenza wako hamupaswi kamwe kushika mimba, kufunga kizazi inaweza kukuwa chaguo bora.
-Unajua kwa hakika kwamba hautaki kushika mimba.
Kufunga mirija ya uzazi kuna ufanisi wa kiasi gani?
Kufunga mirija ya uzazi ni mojawapo za njia zenye ufanisi wa juu sana. Hata hivyo, kuna uwezekano mdogo wa kufeli.
Ndani ya mwaka wa kwanza wa kufunga mirija ya uzazi, chini ya asilimia 1 ya watu watashika mimba. Hii inamaanisha ni upasuaji 5 ya kufunga uzazi kati ya upasuaji 1000. Baada ya mwaka wa kwanza, hadi mwanamke afike kukoma hedhi, hatari mdogo husalia. Katika miaka 10 ya matumizi, takriban asilimia 2 ya watu watashika mimba (wanawake 18-19 kati ya kila 1000)
Ingawa kuna hatari ndogo ya kushika mimba kwa mbinu yoyote ya ufungaji uzazi, ufanisi wa mbinu hutofautiana kiasi, kulingana na jinsi mirija ilizibwa. Wale wanaofunga mirija mara baada ya kujifungua wana hatari ya chini zaidi ya kushika mimba (3).
Kufunga mirija ya uzazi kunaweza kufanywa wakati gani?
-Kufunga mirija ya uzazi kunaweza kufanywa wakati wowote wa mwezi bora imebainiwa kwamba hauna mimba.
-Ikifanywa ndani ya siku saba baada ya mwanzo wa hedhi yako, hakutakuwa na haja yoyote ya kutumia njia yoyote ya uzuiaji mimba kabla ya upasuaji.
-Kama zaidi ya siku saba zimepita tangu mwanzo wa hedhi yako ya mwisho, unaweza kufanyiwa upasuaji wakati wowote bora hauna mimba.
-Kama unabadilisha kutoka kwa tembe za uzuiaji mimba, unaweza kuendelea kutumia tembe hadi umalize pakiti ya kudumisha hedhi yako ya kawaida.
-Kama unabadilisha kutoka kwa IUD, unaweza kufanyiwa upasuaji wa kufunga mirija ya uzazi mara imetolewa.
-Kama unataka upasuaji ufanywe baada ya kujifungua, unaweza kufanywa ndani ya siku saba ama wiki sita baada ya kujifungua, bora imebainiwa kwamba hauna mimba.
-Kama mimba imeharibika ama umetoa mimba bila matatizo, kufunga mirija ya uzazi kunaweza kufanywa ndani ya saa 48.
-kama umetumia tembe za dharura za uzuiaji mimba, kufunga mirija ya uzazi kutakuwa na ufanisi mara hio hio kama imefanywa ndani ya siku saba baada ya mwanzo wa hedhi yako ya kufuata (4).