-Wanawake ambao wamefanya utaratibu wa kufunga mirija ya uzazi mara nyingi wataenda nyumbani siku hio hio. Hata hivyo, inaweza kuchukua muda kabla dawa za anesthesia ziishe nguvu, kwa hivyo ni jambo la busara kukuwa na mtu atakaye kupeleka nyumbani baada ya upasuaji na, muhimu zaidi, ujipatie muda wa kupona.
-Kuna uwezo utahisi uchungu eneo la mkato. Hii ni kawaida na mtoa huduma za matibabu atakupa dawa za maumivu kutuliza uchungu. Wanawake wengine wameripoti kuhisi kama tumbo limejaa, kuwa na gesi nyingi, kizunguzungu, maumivu ya tumbo, na maumivu kwenye mabega siku baada ya kufunga mirija ya uzazi. Maumivu kwenye mabega kwa kawaida yanasababishwa na gesi inayosukumwa kwenye tumbo ili kulipanua wakati wa upasuaji. Kulala chini kwa muda kwa kawaida kutasaidia kupunguza uchungu.
-Kwa hali nadra, unaweza kupata maambukizi kwenye eneo la mkato. Kama utapata joto la mwili juu ya 38° C (100.4° F), kuzirai, maumivu, na/au kutokwa damu, au utokwe usaha kwenye eneo la mkato na hali iendelee au iongezeke saa 12 baada ya upasuaji, unapaswa kuwasiliana na mtoa huduma za matibabu wako (7).
Inachuku muda gani kupona baada ya upasuaji wa kufunga mirija ya uzazi?
Kwa kawaida, muda unaochukuliwa kupoma utategemea afya yako na kasi ya mwili wako kupona baada ya upasuaji. Kulingana na mbinu ya upasuaji wa kufunga mirija ya uzazi uliofanya, inaweza kuchukua siku 1-21 kupona baada ya upasuaji. Kufanya utaratibu wakati wa upasuaji wa kujifungua hakutaongeza muda wa kupona, na unapaswa kupona ndani ya muda wa kawaida wa kupona. Kwa kawaida inapendekezwa kwamba utulie na uepuke kubeba vitu vyenye uzito juu ya pauni 12 (kilo 6) kwa angalau wiki moja baada ya upasuaji. Kama ulishonwa, nyuzi zitayekuka zenyewe ama mtoa huduma za matibabu atapanda siku uende zitolewe.
Je, baada ya kufunga mirija ya uzazi, ninaweza kuanza kufanya ngono baada ya muda gani?
Ingawa kufunga mirija ya uzazi kutakupa kinga dhidi ya mimba mara hio hio, ongea na mtoa huduma za matibabu wako kuhusu lini unaweza kuanza tena ngono ya ukeni. Hata hivyo, watu wengi wanaweza kuanza ngono ndani ya wiki mbili au tatu baada ya upasuaji.