–Kijuianda kwa utaratibu wa kufunga mirija ya uzazi huanza kwa kufanya maamuzi ya busara kuhusu kufanyiwa upasuaji huo.
-Weka miadi ya kabla ya upasuaji na mtoa huduma za matibabu wako. Wakati umeenda kumuona, daktari atapitia historia yako ya kimatibabu, akueleze kuhusu upasuaji huu, na ajibu maswali yoyote utauliza. Daktari anaweza kupendekeza vipimo vya maabara ambavyo vitasaidia kubaini ikiwa upasuaji utakufaa. Hii inaweza kujuisha kipimo cha ujauzito.
-Mara imebainiwa upasuaji utakufaa, mtoa huduma za matibabu atakupa orodha ya maagizo maalum ya kabla ya upasuaji ambayo yanapaswa kufuatwa, ikiwemo vyakula, vinywaji, na dawa za kuepuka.Pia utashauriwa kuhusu vitu vya kuwacha kufanya. Kwa mfano, utaombwa usinywe pombe au kuvuta sigara kwa angalau wiki mbili kabla ya upasuaji. Kama unatumia dawa zozote, unapaswa kusema ili kubaini kama zitaathiri upasuaji na kama unapaswa kuwacha kuzitumia kabla ya upasuaji. Ni muhimu kufuata maagizo haya.
-Mwishowe, panga mbinu ya usafiri ya kurudi nyumbani. Baada ya upasuaji, huenda utahitaji mtu wa kukupeleka nyumbani.
Unahitaji dawa za nusu kaputi (anesthesia) wakati unafanyiwa upasuaji wa kufunga mirija ya uzazi?
Laparoscopy,mini-laparotomy na laparotomy huhitaji kuweka mkato na kwasababu hii, utahitaji anesthesia. Kwa mbinu ya kufunga mirija ya uzazi ya hysteroscopic ambayo inafanywa kwenye chumba cha upasuaji, utaweza kuchagua kama watumie dawa ya kutuliza ama anasthesia ya kufanya ulale kabisa. Kama upasuaji unafanyika kwenye ofisi, dawa ya utulivu nyepesi ama anesthesia ya eneo ya uke na shingo ya kizazi ni chaguo bora kama zinapatikana kwa usalama.