Upasuaji wa Kufunga mirija ya uzazi sio ngumu. Inaweza kufanywa wakati wowote unapotaka, ikijumuisha mara baada ya kuzaa, na wanawake wengine wanapendelea ifanywe wakati wanafanyiwa upasuaji wa kujifungua.
Kuna mbinu mbalimbali za kufunga mirija ya uzazi:
Mbinu ya Laparoscopy ya kufunga mirija ya uzazi
Mbinu hii inajumuisha kuingiza mrija mrefu mwembamba (laparoscope), ambayo ina kamera, ndani ya tumbo kupitia chale mbili ndogo kwenye tumbo. Tumbo kisha inasukumiwa gesi kuipanua na kuifanya iweze kuonekana vizuri. Laparoscope humwezesha mtoa huduma za matibabu kuchunguza tumbo na fupanyonga na kufikia mirija ya uzazi ili kuiziba au kuikata. Sehemu zilizokatwa kisha hufungwa au hubanwa.
Upasuaji huu kwa kawaida hufanywa kwa kutumia dawa za anesthesia za kulalisha kabisa, lakini anesthesia ya sehemu ya upasuaji tu na dawa za kutuliza zinaweza kutumiwa. Laparoscopy huwa na ufanisi mara hio hio ya kuzuia mimba na unachukua muda mfupi kupona.
Mbinu ya Laparotomy ya kufunga mirija ya uzazi
Kwa mbinu hii, mkato mdogo (sentimita 2-3) huwekwa kwenye tumbo, kisha mirija huletwa juu kupitia mkato ili ikatwe au izibwe. Mkato mkubwa zaidi huenda ikawekwa kwa watu walio wanene mno, kwasababu mirija yao haifikiwi kwa urahisi. Laparotomy inaweza kufanywa wakati wowote na inafanywa kwa kawaida kwa wanawake ambao wana hatari ya juu ikiwa watatumia mbinu ya laparoscopic kufunga mirija ya uzazi.
Laparotomy ni mbinu ya upasuaji kubwa zaidi, lakini ambayo inatumiwa mara chache zaidi ( isipokuwa kwa wale wanajifungua kupitia upasuaji wakati huo huo)
Laparotomy ndogo (Minilap)
Mbinu hii ni mbinu ya laparotomy ambayo haivamii mwili sana. Mkato mdogo zaidi huwekwa kwenye tumbo na inafanywa kwa kawaida wakati wa au mara baada ya kujifungua (baada ya kuzaa).
Kama upasuaji huu utafanywa wakati wa upasuaji wa kujifungua, tumbo tayari litakuwa limefunguliwa na mtoa huduma za matibabu atakata au kuziba mirija ya uzazi bila kuongeza anesthesia. kama inafanywa baada ya kujifungua kupitia uke, katheta yako ya uti wa mgongo (epidural) itawachwa mahali pake ili kukupa utulivu unaohitaji. Lakini kama katheta ilitolewa au haukuwekewa, utapatiwa anesthesia ya uti wa mgongo kabla ya upasuaji huu (5).
Mbinu ya Hysteroscope ya kufunga mirija ya uzazi
Mimbu hii hujumuisha kuweka dawa au koili kwenye mirija ya uzazi kupitia shingo ya kizazi. Hii huweka kovu kwenye mirija ya uzazi au huziziba. Uzuri wa utaratibu huu ni kuwa inavamia mwili kidogo tu na inaweza kufanywa kwa eneo kama la ofisi. Inapendekezwa kwa watu ambao taratibu za upasuaji haziwafai sana (6).
Yai huenda wapi baada ya kufunga mirija ya uzazi?
Kufunga mirija ya uzazi hakusimamishi yai kuwachiliwa na ovari (kupevuka kwa yai). Inazuia tu yai kukutana na manii. Mayai yatakayo wachiliwa baada ya kufunga mirija ya uzazi yana vunjwa na kunyonywa kwa usalama na mwili wako. Pia utaendelea kupata hedhi yako hadi ufike kukoma hedhi.