Kuna hali chache za kiafya ambazo zinaweza kukufanya usiweze kutumia LAM kama njia ya uzuiaji mimba. Kuwa na hali hizi kunamaanisha utashauriwa kukoma kumnyonyesha mtoto au unyonyeshe kwa nanma ambayo itapunguza ufanisi wa LAM.
LAM haikubaliwi kabisa kama
-mtoto ana ugonjwa ambayo ina athiri mtindo wake wa kunyonya mara kwa mara. Watoto ambao wanaugua galactosemia kwa kawaida badala ya maziwa ya mama watapewa chakula ambacho kinaweza kuwasaidia wapone (6).
-unatumia dawa zozote za kubadilisha hisia ambazo zinaweza kuathiri kunyonyesha.
-unatumia dawa dawa yoyote ambayo haiingiani na kunyonyesha, kwa mfano, dawa za kuzuia kuganda kwa damu (anticoagulants)
Kulingana na vipimo vya afya, LAM inaweza kupendekezwa kwa tahadhari kama
-Una UKIMWI au imedhibitishwa una VVU. VVU vinaweza kupitishwa kutoka kwa mama hadi kwa mtoto. Kulingana na makali yake, kama una VVU, utashauriwa kuhusu hatari zinazohusishwa na kunyonyesha na kama itakuwa lazima utumie vyanzo vingine vya virutubisho kwa mtoto wako. Kama una VVU na unapata tiba ya kupunguza makali (ART), unaweza kutumia LAM.
-una kifua kikuu (TB). Ingawa TB haiwezi kupitishwa kupitia kunyonyesha, hali ya kugusana kwa karibu kati ya mama na mtoto wakati wa kunyonyesha kunamweka mtoto katika hatari kubwa ya kuambukizwa.