-Inategemea wewe na mtoto wako muwe na uhusiano bora wa kunyonyesha. Sio kila mtu atapata urahisi wa kiasili wa kunyonyesha. Kutoweza kunyonyesha mara kwa mara inavyohitajika itafanya ufanisi wa mbinu hii upungue.
-LAM hufanya tu kazi hadi miezi sita. Hedhi yako ikirudi, ama baada ya miezi sita ya LAM, ni lazima utumie njia ingine ya uzuiaji mimba.
-Viwango vya kufeli viko juu kama hautatumia njia hii sahihi.
-Haitoi kinga dhidi ya magonjwa ya zinaa (STIs), ikiwemo VVU.
Je, kuna madhara yoyote ya LAM?
Hakuna madhara yanoyojulikana ya kutumia mbinu ya kunyonyesha kipindi hakuna hedhi kama njia ya uzuiaji mimba.