LAM huanzishwa mara baada ya kuzaa. Anza kumnyonyesha mtoto ndani ya saa moja baada ya kuzaa au punde iwezekanavyo. Majimaji ya rangi kama ya njano (colostrum) inayozalishwa na matiti ya mama siku chache za kwanza baada ya kuzaa ina vitu muhimu kwa afya ya mtoto.
Matumizi ya mbinu hii inapaswa kuendelea kipindi chote cha miezi sita ya kwanza baada ya kuzaa mtoto, bora unaweza kumnyonyesa mtoto kikamilifu au karibu kikamilifu na hedhi yako haijarudi.
Kiasi gani ya kunyonyesha kinahitajika ili LAM ifanye kazi?
Ikiwa vizuri, mtoto mchanga atahitaji kulishwa kila anapotaka na kwa angalau mara 10-12 kila siku ndani ya wiki chache za kwanza baada ya kuzaa na, baadaye, angalau mara 8-10 kwa siku, ikiwemo angalau mara moja usiku miezi michache ya kwanza.
Wakati wa mchana hakufai kupita zaidi ya saa nne kabla mtoto anyonye tena na usiku ispite zaidi ya saa sita tangu anyonye ya mwisho.
Je, LAM itafanya kazi kama nina kamua maziwa na pia kunyonyesha?
La, kama unataka kutumia LAM kama njia ya uzuiaji mimba, itakuwa tu na ufanisi kama utamnyonyesha mtoto wako mchanga. Kama unamyonyesha na kutumia maziwa ya poda pia, LAM huenda haitakuwa njia yenye ufanisi kwako.
Nifanye nini baada ya miezi sita?
Mwezi wa sita, watoto wengi hawawezi kulishwa tu kwa virutubisho kutoka kwa maziwa ya mama pekee. Inapendekezwa kwamba uanze kumlisha mtoto vyakula vingine (muachishe maziwa)
Kuanza kumlisha mtoto vyakula vingine inamaanisha kuwa hauwezi kuendelea kutegemea LAM kuzuia mimba. Panga miadi na mtoa huduma za matibabu wako ili kujadiliana kuhusu chaguo za njia za uzuiaji mimba.
Itachukua muda kiasi gani ili hedhi yangu irudi baada ya kutumia LAM kama njia ya uzuiaji mimba?
Kurudi kwa urutubisho baada ya kuwacha kutumia LAM kunategemea ni muda gani zaidi mwanamke anaendelea kunyonyesha. Kuachisha mtoto maziwa huwa ni mchakato wa polepole na inamaanisha watoto wengine watategemea maziwa ya mama kwa muda mrefu zaidi ya watoto wengine. Lakini mara kiwango cha kunyonya kimepungua, kupevuka kwa yai kunawezekana.
Nini itafanyika ikiwa siwezi kunyonyesha au hedhi irudi wakati ninafanya LAM?
Kama kwa wakati wowote hauwezi kunyonyesha mara kwa mara, ama hedhi yako ya kila mwezi umerudi, unapaswa kuzingatia kutumia njia ingine ya uzuiaji mimba yenye ufanisi na uendelee kunyonyesha kwa manufaa ya mtoto mchanga.
Panga miadi na mtoa huduma za matibabu ili kujua chaguo zako ni zipi. Unaweza kushauriwa kutumia kondomu ama utumie tembe zenye projestini pekee, ambazo zinafaa wamama wanaonyonyesha.