Mbinu ya kunyonyesha kipindi hakuna hedhi (LAM) ni nini?
Mbinu ya kunyonyesha kipindi hakuna hedhi, inayojulikana kwa kawaida kama LAM ama “kunyonyesha kama njia ya uzuiaji mimba,”ni njia ya uzuiaji mimba ya muda ambayo kiini chake ni kunyonyesha. Ina msingi mmoja wa athari ya kiasili ya kunyonyesha kwa urutubisho wa mwanamke. Kunyonyesha kwa asili hupunguza urutubisho.
Neno “lactational” limetolewa kwa “lactation” na linamaanisha kunyonyesha, ilhali “amenorrhea”kwa urahisi linamaanisha kutopata hedhi.
Unaweza kutumia mbinu ya kunyonyesha hadi miezi sita baada ya kujifungua. Hii itafanya kazi tu kama utafikia mambo yaliyo orodheshwa hapa chini:
-Mtoto ananyonya kikamilifu au karibu kikamilifu mara nyingi mchana na usiku.
Kunyonya kikamilifu kunajumuisha maziwa ya mama pekee (mtoto anategemea maziwa ya mama pekee kwa mahitaji yake yote ya virutubisho) na maziwa ya mama pamoja na vyakula vingine (zaidi ya kunyonya, mtoto mara moja moja atapewa maji, vitamini, juisi na virutubisho vingine)
Kunyonya karibu kikamilifu inamaanisha kwamba, ingawa mtoto anapata virutubisho kutoka kwa chakula na/au vinywaji, angalau zaidi ya robo tatu ya virutubisho anavipata kwa kunyonya maziwa ya mama.
-Mtoto ana umri chini ya miezi sita.
-Hedhi yako haijarudi bado.
Kwa ufupi, mbinu hii itafayna kama umetoka tu kujifungu, hedhi yako haijarudi na unamlisha mtoto maziwa ya mama pekee (1).
LAM hufanyaje kazi?
LAM kimsingi hufanya kazi kwa kuzuia kupevuka kwa yai (kuwachiliwa kwa yai kutoka ovari). Kwa hali hii, kunyonyesha mara kwa mara kunasimamisha kwa muda uwachiliaji wa homoni ambazo husababisha kupevuka kwa yai. (2)
LAM ina ufanisi wa kiasi gani?
Ufanisi wa njia hii kwa kuzuia mimba kimsingi unategemea jinsi unavyoitumia. Kama hautaweza kunyonyesha mtoto wako mchanga kikamilifu au karibu kikamilifu, uko katika hatari kubwa kabisa ya kushika mimba.
Inavyotumiwa kwa kawaida, asilimia 98 ya wanawake waotumia mbinu ya LAM wanaweza kuzuia mimba ndani ya miezi sita ya kwanza baada ya kujifungua. Hii inamaanisha kuwa takriban wanawake 2 kati ya kila 100 wanaotumia njia hii watashika mimba.
Kwa matumizi kamilifu, asilimia 99 ya wanawake wanaotumia mbinu ya LAM huweza kuzuia mimba ndani ya miezi sita ya kwanza baada ya kujifungua (3).
Ni kwa hali gani inashauriwa kutumia LAM?
-Haupangi kutumia njia ingine yoyote ndani ya miezi sita baada ya kuzaa na unamlisha mtoto maziwa ya mama pekee.
-kama hauna uwezo wa kifedha wa kununua njia ingine ya kuzuia mimba ndani ya mizi sita baada ya kujifungua.
-Kama unatafuta njia ya uzuiaji mimba ya muda/ muda mfupi kipindi baada ya kujifungua.
-Kama hauwezi kupata njia ingine ya kisasa ya kuzuia mimba.
– Kwa sababu za kidini na kimila.