Kuna madhara gani ya kutumia dayaframu?
-Unaweza kupata mzio wa silicone ama dawa ya kuua manii. Hali ya kuwashwa inaongeza hatari ya kupata maambukizi kwenye uke. Ikiwa una mzio wa silicone au dawa ya kuua manii, haupaswi kutumia dayaframu.
-Ingawa sio kawaida, unaweza kupata maambukizi kutokana na bakteria nyingi ukeni (bacterial vaginonosis) au maambukizi ya fangasi (candidiasis).
-Wanawake wengine hubaki wamepata maambukizi kwenye njia ya mkojo mara kwa mara.
-Kwa hali nadra mno, unaweza kupata madhara ya kuwepo na sumu inayoletwa na bakteria kuwemo mwilini.
Ni yapi mabaya ya kutumia dayaframu ya kuzuia mimba?
-Unahitaji agizo la daktari na kupimwa na mtoa huduma za matibabu kabla uitumie.
-Inahitaji jitihada kubwa. Wanawake wengine wanapata ugumu wa kuingiza dayaframu lakini bado unapaswa kuiingiza kila wakati unafanya ngono.
-Unahitaji kuridhika na mwili wako. Kuingiza dayaframu kidogo ni sawa kama kuingiza tamponi. Ikiwa unaweza kufanya hivyo, basi unaweza kutumia dayaframu. Ikiwa haupendi kuweka vidole vyako ndani ya uke wako, dayaframu sio chaguo bora kwako.
-Inahitaji nidhamu ya kibinafsi na mpangilio. Unahitaji kukumbuka kuingiza dayaframu kabla ya ngono. Na unahitaji kuikumbuka kila wakati unafanya ngono.
-Inaweza kusukumwa kutoka mahali pake na uume mkubwa, mwanamume anaposukuma kwa nguvu, au staili fulani za ngono.
-Haitoi kinga dhidi ya magonjwa ya zinaa.
-Ni ngumu kukumbuka kuitumia ikiwa umekunywa pombe (7).
Ni kwa hali gani dayaframu ya kuzuia mimba haitakufaa?
Dayaframu huenda haitafaa wanawake ambao
-wanatafuta njia ya uzuiaji mimba ambayo ina ufanisi wa juu wa kuzuia mimba;
-wamejifungua chini ya wiki tatu zilizopita;
-wana historia ya madhara ya kuwepo na sumu inayoletwa na bakteria kuwemo mwilini.
-Una hali ya kimaumbile ambayo itazuia dayaframu kuingia sahihi kwenye shingo ya kizazi ama aina yoyote ya uke kujigawa mara mbili (8).