Manufaa ya Kiafya
-Haina homoni.
-Inapunguza hatari ya ugonjwa wa uvimbe kwenye fupanyonga na utasa unaosababishwa kwa kujiziba kwa mirija ya uzazi.
-Inaweza kutoa kinga dhidi ya mangonjwa mengine ya zinaa (STIs), ikiwemo klamidia, kisonono, uvimbe kwenye fupanyonga na trichomoniasis.
-Inaweza kutoa kinga dhidi ya hali ya seli kukuwa na umbo usiyo wa kawaida na saratani ya shingo ya kizazi (6).
-Inaweza kutumiwa wakati unanyonyesha.
Manufaa kwa mtindo wa maisha
-Unaweza kuingiza dayaframu saa kabla ya ngono na uiwache ndani hadi kwa saa 24.
-Ikilinganishwa na kondomu, inakupa fursa ya kukuwa na ngono isiyopangwa na yenye raha zaidi.
-Ni njia ya uzuiaji mimba ambayo inadhibitiwa na mwanamke, kwa hivyo inaboresha hali ya mwanamke kuanzisha ngono.
-Unaweza kufanya ngono mara nyingi unavyotaka ikiwa ndani, bora uongeze dawa ya kuua manii kila mara.
-Wewe au mwenza wako hampaswi kuihisi.
-Utaweza kushika mimba mara umewacha kutumia dayaframu. Ikiwa hautaki kushika mimba, tumia njia ingine ya uzuiaji mimba mara umewacha kuitumia.