Usiwache dayaframu ndani kwa zaidi ya saa 24. Kutoa dayaframu
-Nawa mikono tena kwa sabuni na maji. Wacha yakauke yenyewe , usiguze chochote.
-Weka kidole cha shahada ndani ya uke na ushikilie juu ya mzingo wa dayaframu.
-Ivute chini kisha nje.
-Baada ya kuitoa nje, ioshe kwa sabuni bila manukato na maji ya uvuguvugu.
-Wacha ikauke kwa upepo. HIfadhi dayaframu pahali penye baridi, pakavu mbali na mwanga wa jua ya moja kwa moja.
-Usitumie poda ama mafuta ya kulainisha yenye oili (kama vaseline, losheni au krimu baridi) kwenye dayaframu kwasababu inaweza kuharibika (5).
Dayaframu ya kuzuia mimba itadumu kwa muda gani?
Kwa matumizi na utunzaji sahihi, dayaframu ya kuzuia mimba inaweza kudumu mwaka moja au miaka miwili.
Kila mara, kagua dayaframu kama ina matundu kabla ya kuitumia. Ikiwa na tundu, wasiliana na mtoa huduma za matibabu wako ili ubadilishiwe.