kuiingiza sio ngumu. Ndio hizi hatua za kufuata:
-Nawa mikono kwa sabuni na maji. Wacha yakauke yenyewe bila kushika chochote.
-Kagua dayaframu yako kuona kama ina matundu na sehemu dhaifu. Kuijaza na maji safi ni mbinu nzuri ya kufanya hivyo- ikiwa maji yanavuja,kuna tundu. Dayaframu yako ikiwa na tundu inamaanisha kwamba haitafanya kazi vizuri na unaweza kushika mimba.
-Weka karibu milimita 5 ya dawa ya kuua manii kwenye kikombe cha dayaframu (sehemu ya ndani ya dayaframu). Paka dawa kwenye mzingo wake pia (usiweke nyingi sana kwasababu itateleza na iwe ngumu kushika). Jeli yoyote ya kuzuia mimba ama dawa ya kuua manii itafanya kazi, isipokuwa za aina zenye safu ya nyenzo kama plastiki au aina za kuingiza. Usisahau kuangalia tarehe ya mwisho ya matumizi ya dawa ya kuua manii.
-Wakati unaingiza dayaframu, hakikisha kuwa kiasi kikubwa cha dawa ya kuua manii kinasalia ndani ya mkunjo, ambamo itakuwa na ufanisi bora zaidi.
-Ikiwa umeketi au umesimama, panua miguu yako. Tenganisha midomo za nje za uke kwa mkono mmoja. Tumia mkono mwingine kuchuna mzingo wa dayaframu na kuikunja iwe nusu.
-Weka kidole chako cha shahada katikati mwa mkunjo, ili ushikilie dayaframu vizuri na thabiti (utakuwa unaguza dawa ya kuua manii).
-Sukuma dayaframu ndani ya uke, ndani kabisa iwezekanavyo. Hakikisha umefunika shingo ya kizazi. Ikiwa umeiweka sahihi, unapaswa kuhisi kama dayaframu imeshika shingo ya kizazi.Dayaframu ambayo haijaingizwa sahihi utahisi ikikusumbua. Ikiwa unahisi hauko starehe, itoe, na ujaribu kuiingiza tena.
-Dayaframu inaweza kuingizwa kabla tu ya ngono. Pia unaweza kuiingiza saa chache kabla. Haijalishi ni wakati gani uli iingiza, lazima uhakikishe umweiwacha ndani kwa angalau saa sita baada ya ngono. Ikiwa unaenda kufanya ngono tena siku hio, wacha tu dayaframu mahali pake na uingize dawa zaidi ya kuua manii ndani kabisa mwa uke. Kuna dawa za kuua manii ambazo zimetengenezwa halisi kwa kuwekwa kwenye dayaframu na zinaweza kuja na kifaa cha kupaka ambacho unaweza kutumia kama utafanya ngono zaidi ya mara moja ndani ya saa sita. Dayaframu haipaswi kutolewa wakati unaongeza dawa ya kuua manii (4).
-Kama unapata shida kuingiza dayaframu, uliza mtoa huduma za matibabu wako kuhusu kupata kifaa cha kuiingiza au zingatia kutumia njia ingine ya uzuiaji mimba.
-kama una maambukizi kwenye uke wako, epuka kutumia dayaframu. Badala yake, tumia kondomu hadi maambuzi yaishe.
Je, mwenza wangu atahisi dayaframu wakati wa ngono?
Kama imeingizwa vizuri, watumiaji wengi na wenza wao hawatahisi dayaframu wakati wa ngono.
Na ikiwa ninataka kufanya ngono mara nyingi?
Unaweza kuwacha dayaframu ndani saa 6-12 baada ya ngono. Kama utafanya ngono tena ndani ya saa hizo sita, utahitaji kuongeza dawa ya kuua manii zaidi. Wakati umefanya ngono tena, saa itaanza kujiesabu upya, na kuanza saa ya mwisho ulipofanya ngono. Dayaframu isibaki ndani zaidi ya saa 24 mfululizo.
Na dayaframu ikipasuka au kutoka mahali pake wakati wa ngono?
Kama dayaframu itapasuka au kutoka mahali pake wakati inatumiwa, unapaswa mara hio hio kuzingatia kutumia tembe za dharura za kuzuia mimba ili kuzuia hatari yoyote ya mimba.
Baada ya kuingizwa, dayaframu hupata ufanisi baada ya muda gani?
Dayaframu hupata ufanisi mara hio hio inapoingizwa na haitadhuru homoni zako.