Madhara ya tembe ndogo

Madhara ya tembe ndogo
Madhara ya tembe ndogo

Madhara ya tembe ndogo ni gani?

Madhara sio ishara ya ugonjwa na baadhi yao yatapungua au kuisha ndani ya miezi za kwanza za matumizi ya tembe. ingawa kwa kawaida yanakuwepo, wanawake wengine hawapati madhara yoyote kamwe. Madhara yanayoripotiwa sana yanajumuisha:
-Mabadiliko kwa mzunguko wa hedhi ya mtumiaji, ikijumuisha, ziwe ambazo hazitabiriki, zikuje mara chache, ziwe kwa siku mingi zaidi, au zipote kabisa (wanawake wanaonyonyesha wanaweza kuchelewa kupata hedhi yao kwasababu kunyonyesha huleta mabadiliko kwenye mzunguko wa hedhi );
-kuumwa kichwa;
-kizunguzungu;
-maumivu ya tumbo;
-matiti chungu;
-mabadiliko ya hisia; na
-kichefuchefu (kuepuka kichefuchefu, meza tembe pamoja na chakula au wakati wa kulala)
Wanawake ambao hawanyonyeshi wanaweza kupata uvimbe kwenye ovari (ovarian follicles) [8].

Hatari

Ikilinganishwa na tembe mchanganyo, tembe ndogo inaufanisi wa chini kidogo kwa uzuiaji mimba. Hii ni kwasababu haizui kupevuka kwa yai bora kushinda tembe zenye estrojeni.
Ukishika mimba wakati unatumia tembe yenye projestini pekee, kuna hatari mdogo kwamba mimba itatunga nje ya mji wa mimba. Hata hivyo, uwezo wa mimba kutunga nje ya mji wa mimba uko chini wakati unatumia tembe ya projestini pekee kuliko ikiwa hautumi njia yoyote ya kisasa ya kuzuia mimba.

Ikiwa, baada ya miezi mitatu, unahisi kwamba madhara yamezidi kiasi unaweza kuvumilia, tumia njia tofauti ya uzuiaji mimba na ubaki una kinga. Kondomu zinakupa kinga nzuri wakati unatafuta njia ya uzuiaji mimba itakayokufaa. Kumbuka kwamba tembe yenye projestini pekee haikukingi dhidi ya mangonjwa ya zinaa.

Je tembe yenye projestini pekee ya kudhibiti mimba inaweza kusababisha chunusi?

Ingawa projestini haisababishi chunusi, ni mojawapo ya vitu vinavyochangia kukuwepo kwa chunusi. Projestini huongeza sebum (majimaji ya kunata na yenye mafuta inayozalishwa wakati ngozi unaundwa). Sebun nyingi zaidi kwenye ngozi inaweza kuziba vitundu vidogo na kufanya mazingira yawe mazuri mno kwa bakteria kuishi. Hali hii hufanya ngozi uwe na chunusi. Chunusi aina hii hujulikana kama chunusi ya homoni. Ikiwa utapata chunusi wakati unatumia tembe yenye projestini pekee, zungumza na mtoa matibabu wako kuhusu chaguo zako za matibabu. Ikiwa hii madhara itakuwa zaidi ya vile unaweza kuvumilia, unaweza kuzingatia kubadilisha na kutumia njia tofauti ya uzuiaji mimba.

Je kuna uhusiano kati ya tembe zenye projestini pekee na saratani?

Utafiti wa hivi karibuni uliyoendeshwa na jarida la PLOS medicine l unaonyesha kwamba kutumia tembe yenye projestini pekee inamweka mtu kwenye hatari ndogo ya kupata saratani ya matiti, sawa na hatari inayopatikana kwa tembe mchanganyo. Hata hivyo, hatari hii iko juu zaidi kwa wanawake wenye umri wa juu lakini hatari itaisha ndani ya miaka chache baada ya kuwacha kutumia tembe. Habari njema ni kwamba tembe hizi hukinga wanawake dhidi ya saratani zingine za wanawake kama saratani ya mji wa mimba na saratani ya ovari. Ikiwa unazingatia kutumia tembe yenye projestini pekee kama njia ya uzuiaji mimba , zungumzia uzuri na ubaya wa tembe na mtoa matibabu wako.

Je, ninapaswa kuwa na wasiwasi kuhusu tembe yenye projestini pekee ya kudhibithi uzai kusababisha matone ya damu?

Kutokwa matone ya damu au damu kati ya hedhi zako ni madhara ya kawaida ya tembe yenye projestini pekee ya kudhibiti uzazi hasa ikiwa umeanza kutumia tembe miezi miwili iliyopita. Hili linafanyika wakati mwili wako unazoea njia mpya ya uzuiaji mimba. Kutokwa damu kati ya hedhi zako kunasababishwa na mabadiliko kwa homoni. kwa mzunguko wa hedhi wa kawaida, homoni za projestini na estrojeni za asili ndani ya mwili wa mwanamke zinasaidia kuunda na kuendeleza utando wa mji wa mimba katika maandalizi ya mimba. Hali ya kuingiza projestini kwenye mji wa mimba huvuruga usawa. Hii inaweza kusababisha vipindi vya kutokwa damu au matone ya damu.

Kwa watumiaji wengi, itachukua miezi chache kwa mwili kuzoea njia ya uzuiaji mimba na kurejea mzunguko wa kawaida. Ikiwa matone ya damu hayatapungua na bado unataka kutumia njia ya uzuiaji mimba ambayo haina estrojeni, unaweza kuzungumza na mtoa matibabu wako kuhusu chaguo zenye projestini pekee kama vile vipandikizi na sindano.

Maswali elekezi kwa mbinu za kuzuia mimba

Je, unahitaji usaidizi zaidi kuchagua njia yako bora? Jibu maswali yetu elekezi kwa mbinu za kuzuia mimba.

Jibu maswali machache rahisi, na kulingana na majibu, tutapendekeza chaguo za uzuiaji mimba ambazo zinaweza kukufaa.

Jibu maswali
External Condom

Compare with similar Contraceptive Methods

Are you wondering if condoms are better than daily pills? Or if you should opt for a birth control implant? We're here to assist you in making this decision. You can select up to 5 contraceptive methods and compare them side by side to weigh the pros and cons of each.

Give a try to our Contraceptive Tool

In the example below, you'll find similar methods to the one you're currently reading about. Feel free to click on any that catch your interest or revisit our Contraceptive Methods page

Our Monthly Top Articles

Mnong’onezaji wa mambo ya uke: Jinsi ya kupenda uke wako hivyo ilivyo

Mnong’onezaji wa mambo ya uke: Jinsi ya kupenda uke wako hivyo ilivyo

Kabla tuzungumzie mambo ya kuthamini uke, tucheze mchezo ambapo una alama 50 kutoka mwanzo. Nina orodha ya maswali 5 na ikiwa umawahi fanya kile kilichoulizwa kwenye swali, unapoteza alama 10. Twen...

Njia 6 tunaweza kuchukua udhibiti wa uzazi wa mpango kama wanaume

Njia 6 tunaweza kuchukua udhibiti wa uzazi wa mpango kama wanaume

Ingawa ngono salama ni jukumu la wanaume na wanawake, mambo ya uzazi wa mpango imechukuliwa tangu kitambo  kama jukumu la mwanamke. Ingekuwa wanaume wangechukua jukumu la kutumia njia za kuzuia mim...

Mnong’onezaji wa mambo ya uke: Jinsi ya kupenda uke wako hivyo ilivyo

Mnong’onezaji wa mambo ya uke: Jinsi ya kupenda uke wako hivyo ilivyo

Kabla tuzungumzie mambo ya kuthamini uke, tucheze mchezo ambapo una alama 50 kutoka mwanzo. Nina orodha ya maswali 5 na ikiwa umawahi fanya kile kilichoulizwa kwenye swali, unapoteza alama 10. Twen...

Njia 6 tunaweza kuchukua udhibiti wa uzazi wa mpango kama wanaume

Njia 6 tunaweza kuchukua udhibiti wa uzazi wa mpango kama wanaume

Ingawa ngono salama ni jukumu la wanaume na wanawake, mambo ya uzazi wa mpango imechukuliwa tangu kitambo  kama jukumu la mwanamke. Ingekuwa wanaume wangechukua jukumu la kutumia njia za kuzuia mim...

Mnong’onezaji wa mambo ya uke: Mambo yanayohatarisha uke na njia za kuitunza

Mnong’onezaji wa mambo ya uke: Mambo yanayohatarisha uke na njia za kuitunza

Uke ni sehemu moja ya mwili isiyoeleweka vizuri. Ingekuwa uke wako ungeweza kuongea,  ungekuambia nini? Nadhani unge changanyikiwa cha kusema. Mara tunaona makala inayosema safisha uke wako na tena...