-ikiwa una ugonjwa wa systemic lupus erythematosus (SLE) na umedhibiti kwa vipimo kwamba una antibodi ambazo zinashambulia mwili (antiphospholipid antibodies);
– ikiwa unatumia dawa maalum kama vile za kuzuia mshtuko, za kupunguza makali ya VVU au antibayotiki ambazo zinaweza kuchochea enzaimu za ini;
-ikiwa una au umewahi kuwa na saratani ya matiti;
-ikiwa umekuwa na kiharusi, kuganda damu kwa mguu au mapafu zako, mshtuko wa moyo au matatizo mengine mbaya ya moyo na;”
– ikiwa una ugonjwa wa uharibifu wa ini au maabukizi kwenye ini au uvimbe.
Ikiwa una dalili zozote ambazo zimetajwa hapo juu, unashauriwa kumwona mtoa matibabu aliyehitimu ili akupe mawaidha kuhusu njia za uzuiaji mimba. Utashauriwa kuhusu njia ya uzuiaji mimba itakayokufaa zaidi.