Manufaa ya kiafya
Wanawake wanaonyonyesha wanaweza kuitumia.
Ikitumika kwa njia sahihi, inaweza kuwa na ufanisi wa asilimia 99 kwa kuzuia mimba.
Ina viwango vya chini vya homoni ikilinganishwa na tembe mchanganyo.
Tofauti na tembe mchanganyo, tembe yenye projestini pekee haileti hatari ya juu ya kusababisha damu kuganda. Kwa hivyo, wanawake wengine ambao hawawezi kutumia tembe mchanganyo wanaweza kuitumia. Kwa mfano, wale walio na kipandauso kali na shinikizo la juu la damu.
Inaweza kutumika kama njia dharura ya uzuiaji mimba baada ya ngono. Tembe yenye projestini pekee, ikimezwa ndani ya saa 72 baada ya kufanya ngono, inaweza kusaidia kusimamisha au kuchelewesha kupevuka kwa yai. Hata hivyo, haiwezi kuzuia au kuvuruga upandikizaji.
Inaweza kusaidia kupunguza dalili kabla ya hedhi au hedhi yenye maumivu.
Inaweza kutumika katika umri wowote, hata na wanawake wenye wanavuta sigara wenye umri wa miaka zaidi ya 35. [7].
Manufaa kwa mtindo wa maisha
Tembe inaweza kumezwa wakati wowote, hata punde baada ya kujifungua.
Tembe ni rahisi kutumia-imeze tu na maji
Inapatikana kwa urahisi na inaweza kununuliwa bila maagizo ya daktari kutoka kwenye duka la dawa na hospitali.
Hauhitaji kukatiza ngono ili kuitumia.
Tembe imesimamiwa na mwanamke na inampa udhibiti kamili.
Matumizi yake yanaweza kukomeshwa saa yoyote bila usaidizi wa mtoa matibabu.
Haicheleweshi urutubisho wa uzazi. Unaweza kushika mimba siku chache baada ya kuwacha kutumia tembe. Ukiwacha kutumia tembe na hauko tayari kushika mimba, tumia njia ingine ya uzuiaji mimba.
Je tembe ndogo husimamisha hedhi?
Matumizi ya tembe ndogo yanaweza kusababisha mabadiliko kwa mzunguko wa hedhi. Mabadikiko haya hayana madhara. Kwa matumizi ya kawaida,tembe hizi zitarefusha kipindi ambacho mwanamke anayenyonyeshsa atakosa hedhi ya kila mwezi. Kwa wanawake wanaopata hedhi kila mwezi, ni kawaida kupata hedhi mara kwa mara au kupata hedhi isiyotabirika.