Tembe yenye projestini pekee (Tembe ndogo)

Tembe yenye projestini pekee (Tembe ndogo)
Tembe yenye projestini pekee (Tembe ndogo)

Tembe yenye projestini pekee ni nini?

Tembe yenye projestini pekee, pia inayojulikana kama tembe ya uzuiaji mimba ya projestini pekee ya njia ya mdomo au tembe ndogo, ni kidonge kidogo chenye homoni moja inayotumiwa kuzuia mimba. Ina viwango vidogo mno vya homoni bandia ya projestini. Homoni hii inafanana na hamoni ya projesteroni ambayo hupatikana kwenye mwili wa mwanamke. Tembe moja inamezwa mara moja kwa siku, kwa saa sawa kila siku. Kuna aina mbalimbali za chapa za tembe yenye projestini pekee zinazopatikana, na chaguo mpya zinazidi kuongezwa kwenye soko [1].

Tembe yenye projestini pekee hufanya aje kazi?

Tembe hii hufanya ute wa shingo ya kizazi uwe nzito, na huu ute nzito unazuia manii kuingia kwenye tumbo la uzazi na kusafiri hadi mirija ya uzazi ili kurutubisha yai.

Ni nini tofauti kati ya tembe yenye projestini pekee (tembe ndogo) na tembe mchanganyo?

Tembe yenye projestini pekee ni tofauti na tembe mchanganyo kwa maana ina homoni moja tu ya kike. Kwa hivyo, inaweza kutumika na wanawake wanaonyonyesha na wanawake ambao hawawezi kutumia njia za uzuiaji mimba zenye estrojeni kwa sasabu yoyote ile. Haisimamishi hedhi ya kawaida kwa wanawake wengi. Tembe ndogo imeundwa na chapa mbalimbali na kwa kawaida itakuwa ndani ya pakiti yenye tembe 28 hai. Hii inamisha kwamba tembe zote 28 zina homoni ya projestini. Pakiti pia inaweza kukuja na tembe 24 zenye homoni na tembe 4 bila homoni. kabla ya kutumia tembe, soma maelekezo ndani ya pakiti kila mara kwa makini na hakikisha kwamba umeelewa jinsi ya kutumia tembe na kitu unachohitaji kufanya iwapo utakosa kumeza tembe au utahisi kichefuchefu [2].

Tembe yenye projestini pekee hufanana aje?

Tembe yenye projestini pekee (tembe ndogo) humezwa aje?

Kitu cha kwanza unahitaji kujua ni kwamba wakati bora zaidi wa kuanza kumeza tembe ni siku ya kwanza hadi ya tano ya hedhi yako. Hii ni kwasababu unapata kinga mara hio hio dhidi ya hatari ya kupata mimba. Hata hivyo, kuanza kumeza tembe wakati wowote ni sawa. Tofauti pekee ni kwamba utahitaji kutumia njia ya ziada ya uzuiaji mimba, kama kondomu, kwa saa 48 ya kwanza. Hii itaipa muda tembe kupata ufanisi.

Je ni vipi utapata ufanisi wa juu zaidi kwa tembe yenye projestini pekee?

Ikitumika sahihi, tembe yenye projestini pekee inaweza kuwa na ufanisi wa zaidi ya asilimia 99 kwa kuzuia mimba. Hata hivyo, ina ufanisi wa asilimia 93 kwa wanawake ambao hawanyonyeshi [3].
Lazima ukumbuke kumeza tembe kila siku, hata iwe nini, na uanze pakiti mpya kwa saa. Tembe inaweza kumezwa saa yoyote ya siku. Wanawake ambao hawanyonyeshi wanapaswa kumeza tembe wakati sawa, kila siku. Kumeza tembe yenye projestini pekee ikiwa umechelewa zaidi ya saa tatu kutafanya ufanisi wa tembe upungue.
Hata hivyo, aina mpya, kama vile Cerazette, inaweza kumezwa ndani ya saa 12 ya siku sawa kila siku. Ikiwa kuna uwezo utasahau kumeza dawa, unaweza kuweka king’ora cha kuku kumbusha au uweke saa ya kumeza tembe iambatane na shughuli zako za kila siku kama vile kupiga meno mswaki. Meza tembe moja kila siku mfululizo na usiwache hata siku za hedhi. Ukimaliza pakiti ya kwanza, anza pakiti mpya siku inayofuata [5].

Tembe yenye projestini pekee inaanza kufanya kazi mara hio hio:

-ikiwa umetoka tu kujifungua na uimeze ndani ya siku 21 baada ya kuzaa.
-Ikiwa unaitumia kati ya wiki sita na miezi sita baada ya kuzaa na ikiwa unanyonyesha mtoto tu bila kumpa chakula kingine na haujapata hedhi yako.
-punde baada ya mimba kuharibika au mimba kutolewa.
-Siku baada ya kuwacha kutumia njia ya uzuiaji mimba ya homoni. (Ikiwa unatoka kwa matumizi ya tembe mchanganyo, meza tembe ya kwanza ya projestini siku inayofuata siku ulimeza tembe yako ya mwisho yenye homoni. Ikiwa utaanza kumeza tembe yenye projestini pekee nje ya hali hizi, unapaswa kutumia njia ya ziada ya uzuiaji mimba, kama kondomu, kwa saa 48 za mwanzo.)
-ukianza kuzitumia siku mbili kabla ya utoaji wa kifaa cha ndani ya mji wa mimba ((IUD) [4].

Ni nini ninapaswa kufanya ikiwa nimesahau kumeza tembe ndogo?

Ikiwa umesahau kumeza tembe yenye projestini pekee kwa zaidi ya saa tatu, meza moja punde utakapo kumbuka, na utumie njia ya ziada kwa saa 48 ya kufuata. Meza tembe inayofuata kwa saa yako ya kawaida siku yakufuata.
Pakiti ya tembe yenye projestini pekee ambayo ina tembe 24 ya homoni na tembe 4 bila homoni inakupa fursa ya kumeza tembe saa ingine yoyote ikiwa ulisahau kumeza tembe. Ikiwa mara kwa mara unasahau kumeza tembe, unaweza meza tembe moja ndani ya saa 24 ya kufuata. Hata hivyo, kukosa kumeza tembe kunapunguza ufanisi wa njia hii ya uzuiaji mimba wa kukukinga dhidi ya mimba.

Ni nini napaswa kufanya ikiwa ninahara au natapika baada ya kumeza tembe ndogo?

Ikiwa utatapika kupindukia au uhare ndani ya saa tatu baada ya kumeza tembe yenye projestini pekee, kuna uwezo mkubwa kwamba bado haijanyonywa mwilini kamilifu. Endelea kumeza tembe lakini tumia njia ya ziada ya uzuiaji mimba kwa saa 48 ya kufuata baada ya kutapika au kuhara [6].

Je ninapaswa kuendelea kumeza tembe ndogo ikiwa nimewacha kunyonyesha?

Mara unapowacha kunyonyesha, unaweza kuendelea na njia hii ikiwa umeridhika nayo, au unaweza kuongea na daktari wako au muuguzi wako kuhusu kuanza kutumia njia tofauti ya uzuiaji mimba.

Ni lini itakua salama kufanya ngono bila kinga baada ya kuanza kutumia tembe ndogo?

Inachukua karibu siku 2 ili tembe yenye projestini pekee iwe na ufanisi wa kukinga mimba. Kwa hivyo inapendekezwa utumie njia ya kizuizi kama vile kondomu kwa siku mbili za kwanza. Baadaye, unaweza kufanya ngono bila kinga pasi kuwa na wasiwasi ya kushika mimba. Wakati mwingine, mtoa matibabu wako au maelekezo kwenye kipeperushi kinachopatikana ndani ya pakiti yanaweza kukushauri kutumia njia ya ziada ya uzuiaji mimba kwa siku 7 baada ya kuanza tembe. Mawaidha haya yanetolewa kwasababu.

Maswali elekezi kwa mbinu za kuzuia mimba

Je, unahitaji usaidizi zaidi kuchagua njia yako bora? Jibu maswali yetu elekezi kwa mbinu za kuzuia mimba.

Jibu maswali machache rahisi, na kulingana na majibu, tutapendekeza chaguo za uzuiaji mimba ambazo zinaweza kukufaa.

Jibu maswali
External Condom

Compare with similar Contraceptive Methods

Are you wondering if condoms are better than daily pills? Or if you should opt for a birth control implant? We're here to assist you in making this decision. You can select up to 5 contraceptive methods and compare them side by side to weigh the pros and cons of each.

Give a try to our Contraceptive Tool

In the example below, you'll find similar methods to the one you're currently reading about. Feel free to click on any that catch your interest or revisit our Contraceptive Methods page

Our Monthly Top Articles

Mnong’onezaji wa mambo ya uke: Jinsi ya kupenda uke wako hivyo ilivyo

Mnong’onezaji wa mambo ya uke: Jinsi ya kupenda uke wako hivyo ilivyo

Kabla tuzungumzie mambo ya kuthamini uke, tucheze mchezo ambapo una alama 50 kutoka mwanzo. Nina orodha ya maswali 5 na ikiwa umawahi fanya kile kilichoulizwa kwenye swali, unapoteza alama 10. Twen...

Njia 6 tunaweza kuchukua udhibiti wa uzazi wa mpango kama wanaume

Njia 6 tunaweza kuchukua udhibiti wa uzazi wa mpango kama wanaume

Ingawa ngono salama ni jukumu la wanaume na wanawake, mambo ya uzazi wa mpango imechukuliwa tangu kitambo  kama jukumu la mwanamke. Ingekuwa wanaume wangechukua jukumu la kutumia njia za kuzuia mim...

Mnong’onezaji wa mambo ya uke: Jinsi ya kupenda uke wako hivyo ilivyo

Mnong’onezaji wa mambo ya uke: Jinsi ya kupenda uke wako hivyo ilivyo

Kabla tuzungumzie mambo ya kuthamini uke, tucheze mchezo ambapo una alama 50 kutoka mwanzo. Nina orodha ya maswali 5 na ikiwa umawahi fanya kile kilichoulizwa kwenye swali, unapoteza alama 10. Twen...

Njia 6 tunaweza kuchukua udhibiti wa uzazi wa mpango kama wanaume

Njia 6 tunaweza kuchukua udhibiti wa uzazi wa mpango kama wanaume

Ingawa ngono salama ni jukumu la wanaume na wanawake, mambo ya uzazi wa mpango imechukuliwa tangu kitambo  kama jukumu la mwanamke. Ingekuwa wanaume wangechukua jukumu la kutumia njia za kuzuia mim...

Mnong’onezaji wa mambo ya uke: Mambo yanayohatarisha uke na njia za kuitunza

Mnong’onezaji wa mambo ya uke: Mambo yanayohatarisha uke na njia za kuitunza

Uke ni sehemu moja ya mwili isiyoeleweka vizuri. Ingekuwa uke wako ungeweza kuongea,  ungekuambia nini? Nadhani unge changanyikiwa cha kusema. Mara tunaona makala inayosema safisha uke wako na tena...