Madhara ya kiraka cha kuzuia mimba

Madhara ya kiraka cha kuzuia mimba
Madhara ya kiraka cha kuzuia mimba

Madhara ya kiraka cha kuzuia mimba sio kila mara huwa na athari mbaya na kwa kawaida yataisha baada ya miezi michache. Yanajumuisha [7]
-Mabadiliko kwa mzunguko wa hedhi, ( kama vile hedhi nyepesi na zije siku chache, zije siku mingi zaidi au ziwe ambazo hazitabiriki, au zipote kabisa);
-kichefuchefu na kutapika;
-kuumwa kichwa;
-ulaini wa matiti;
-upele au ngozi inayowasha eneo lililo na kiraka;
-maumivu ya tumbo
-maambukizo kwenye uke (mwasho, kuwa nyekundu au kufura kwa uke);
-dalili za mafua/ maambukizi ya njia ya juu ya kupumua; na
-shinikizo la juu la damu. kiraka cha kuzuia mimba kinaweza kuongeza shinikizo la damu kwa kiasi ndogo. Kwa wanawake wengi, ongezeko hili ni kidogo na haliathiri afya yao. Wale wanaokitumia wanashauriwa kupima presha kila miezi michache. Ikiwa kiraka kitasababisha ongezeko la presha liwe juu sana, unashauriwa kuwacha matumizi. Presha itarudi chini ukiwacha kutumia kiraka cha uzuiaji mimba.

Je Kiraka cha kuzuia mimba hufanya uongeze uzani?

Hakuna utafiti unaojulikana umethibitisha kwamba kiraka cha kuzuia mimba kinaweza kusababisha mtu aongezo uzani. Utafiti moja, uliofanywa kwa watumiaji wa kiraka kwa kipindi cha miezi sita, ulionyesha kuwa ndani ya miezi hiyo sita, washiriki hawakuongeza zaidi ya kilo 1, na ule uzito ulioongezwa hauwezi kuhusishwa na kiraka.

Kiraka changu cha kudhibiti mimba kinafanya niwashwe. Nikabiliane nalo vipi?

Ili kuepuka kuwashwa na kiraka, hakikisha umekiweka sehemu ya ngozi iliyo safi na iliyokauka na haijapakwa chochote. Pia haipaswi kuwa na kidonda au mkato wowote na isiwe sehemu ulikuwa umeweka kiraka awali. Ukianza kuwashwa au kupata upele baada ya kuweka kiraka, kitoe na uweke kipya sehemu ingine ya ngozi. Osha sehemu iliyoathiriwa kwa maji na sabuni bila manukato, kisha tuliza ngozi kwa kuweka barafu au/ na kupaka krimu ya kutuliza mwasho. Ikiwa umepata upele mkali na uouma, unaweza kutumia dawa ya antihistamine na dawa ya kupunguza kufura na maumivu. Ikiwa hii itafanyika katika sehemu mpya ya ngozi, kuna uwezekano kwamba una mzio wa kiraka na unapaswa kuzingatia kuzungumza na mtoa matibabu wako kuhusu njia zingine za uzuiaji mimba.

Ni nini itafanyika ikiwa kiraka changu cha kudhibiti mimba kimeanguka?

kwa matumizi ya kawaida, kiraka cha kuzuia mimba kina nata sana na hakipaswi kuanguka, hata kwenye bafu ya maji moto, sauna, bafu,shawa au bwawa la kuogelea. Hata hivyo, kikianguaka,weka kiraka kipya ikiwa kile kimeanguka kilikuwa kimekaa chini ya saa 48, na ukibadilishe siku iliyopangwa ya kubadilisha kiraka. Bado unapata kinga dhidi ya hatari ya mimba ikiwa umetumia kiraka kwa njia sahihi kwa siku saba zilizopita na siku saba kabla ya wiki yako bila kiraka ikiwa uko katika wiki ya tatu.
Ikiwa kiraka kilitoka zaidi ya saa 48 au hauna hakika kuhusu saa imepita tangu kianguke, weka kiraka kipya na ukibadilishe siku yako ya kawaida ya kubadilisha ikiwa umekuwa nacho kwa wiki moja au mbili. Ikiwa ni wiki ya tatu, anza kifungu kipya cha kiraka (ichukulie kama siku ya kwanza) na uruke wiki bila kiraka. Katika hali zote mbili, tumia njia za ziada ya uzuiaji mimba kwa siku saba za kufuata.
Ikiwa ulifanya ngono wakati wa wiki bila kiraka au wiki ya kwanza na kiraka kilianguka, au ikiwa ulifanya ngono wiki ya pili au wiki ya tatu, au wakati kiraka hakikuwa kimejibandika vizuri kwa siku saba, hakikisha umetumia njia ya dharura ya uzuiaji mimba. Pia unaweza kuhitajika kuzungumza na mtoa matibabu wako kuhusu chaguo zako zingine.

Matatizo

Matatizo ya kiraka cha kuzuia mimba ni sawa na yale yanayohusika na tembe mchanganyo. Yanaweza kujumuisha

Nadra kabisa

-mshtuko wa moyo
-kiharusi
Kuganda damu kwenye mishipa (venous thromboembolism). Katika hali nadra sana, kuganda damu ya kutishia maisha inaweza kutokea kwenye mishipa au mapafu. Matumizi ya kiraka yanaongeza kidogo uwezo wa kuganda damu. Kwasababu wanawake wanaotumia kiraka cha kuzuia mimba wanapata dozi ya juu ya estrojeni ikilinganishwa na wale wanatumia tembe, hatari ya kuganda damu wakati wa kutumia kiraka uko juu, takriban mtu 1 kati ya watu 500. [8]

Unapswa kumwona daktari wako mara moja, ikiwa utaona yafuatayo:

-kuumwa kichwa sana, au kipandauso
-kupata shida kupumua;
-mguu kufura na iwe na maumivu;
-hisia ya kufa ganzi au ya udhaifu kwenye mkono au mguu;
-matatizo ya ghafla kuongea au kuona;
-kukohoa damu;
-maumivu kwenye kifua, hasa ikiwa unahisi uchungu wakati unavuta hewa ndani; na
-maumivu makali ya tumbo; na
-Kuzirai au kuzimia bila sababu;
Dalili hizi zinaweza kusababishwa na damu kuganda
Ikiwa, baada ya miezi mitatu, unahisi kwamba madhara yamezidi kiasi unaweza kuvumilia, tumia njia tofauti ya uzuiaji mimba na ubaki una kinga. Kondomu zinakupa kinga nzuri wakati unatafuta njia ya uzuiaji mimba itakayokufaa. Kumbuka kwamba kiraka cha kuzuia mimba hakikukingi dhidi ya mangonjwa ya zinaa.

Maswali elekezi kwa mbinu za kuzuia mimba

Je, unahitaji usaidizi zaidi kuchagua njia yako bora? Jibu maswali yetu elekezi kwa mbinu za kuzuia mimba.

Jibu maswali machache rahisi, na kulingana na majibu, tutapendekeza chaguo za uzuiaji mimba ambazo zinaweza kukufaa.

Jibu maswali
External Condom

Compare with similar Contraceptive Methods

Are you wondering if condoms are better than daily pills? Or if you should opt for a birth control implant? We're here to assist you in making this decision. You can select up to 5 contraceptive methods and compare them side by side to weigh the pros and cons of each.

Give a try to our Contraceptive Tool

In the example below, you'll find similar methods to the one you're currently reading about. Feel free to click on any that catch your interest or revisit our Contraceptive Methods page

Our Monthly Top Articles

Mnong’onezaji wa mambo ya uke: Jinsi ya kupenda uke wako hivyo ilivyo

Mnong’onezaji wa mambo ya uke: Jinsi ya kupenda uke wako hivyo ilivyo

Kabla tuzungumzie mambo ya kuthamini uke, tucheze mchezo ambapo una alama 50 kutoka mwanzo. Nina orodha ya maswali 5 na ikiwa umawahi fanya kile kilichoulizwa kwenye swali, unapoteza alama 10. Twen...

Njia 6 tunaweza kuchukua udhibiti wa uzazi wa mpango kama wanaume

Njia 6 tunaweza kuchukua udhibiti wa uzazi wa mpango kama wanaume

Ingawa ngono salama ni jukumu la wanaume na wanawake, mambo ya uzazi wa mpango imechukuliwa tangu kitambo  kama jukumu la mwanamke. Ingekuwa wanaume wangechukua jukumu la kutumia njia za kuzuia mim...

Mnong’onezaji wa mambo ya uke: Jinsi ya kupenda uke wako hivyo ilivyo

Mnong’onezaji wa mambo ya uke: Jinsi ya kupenda uke wako hivyo ilivyo

Kabla tuzungumzie mambo ya kuthamini uke, tucheze mchezo ambapo una alama 50 kutoka mwanzo. Nina orodha ya maswali 5 na ikiwa umawahi fanya kile kilichoulizwa kwenye swali, unapoteza alama 10. Twen...

Njia 6 tunaweza kuchukua udhibiti wa uzazi wa mpango kama wanaume

Njia 6 tunaweza kuchukua udhibiti wa uzazi wa mpango kama wanaume

Ingawa ngono salama ni jukumu la wanaume na wanawake, mambo ya uzazi wa mpango imechukuliwa tangu kitambo  kama jukumu la mwanamke. Ingekuwa wanaume wangechukua jukumu la kutumia njia za kuzuia mim...

Mnong’onezaji wa mambo ya uke: Mambo yanayohatarisha uke na njia za kuitunza

Mnong’onezaji wa mambo ya uke: Mambo yanayohatarisha uke na njia za kuitunza

Uke ni sehemu moja ya mwili isiyoeleweka vizuri. Ingekuwa uke wako ungeweza kuongea,  ungekuambia nini? Nadhani unge changanyikiwa cha kusema. Mara tunaona makala inayosema safisha uke wako na tena...