Kiraka cha kuzuia mimba hakifai kutumika na wanawake ambao:
-wana ugonjwa kali wa ini, uharibifu wa ini au saratani ya ini;
-Wana au wamewahi kuwa na saratani ya matiti;
-wana kipandauso mkali (migrane) iliyo na aura ( eneo la jicho linalong’aa lililopoteza uwezo wa kuona, kabla ya maumivu makali sana ya kichwa);
-wana historia ya kiharusi au mshtuko wa moyo;
-walizaa hivi karibuni (ndani ya miezi mitatu hadi sita) hata hivyo, unaweza kuanza kutumia kiraka baada ya miezi sita au wakati maziwa ya matiti sio chakula kuu cha mtoto wako);
-una historia ya kuganda damu (kwenye mishipa ya kina au kwenye mapafu -deep vein thrombosis au pulmonary embolism) au ikiwa kuna mtu kwa familia yako ambaye ana magonjwa ya damu ambayo yanaweza kuongeza hatari ya damu kuganda;
-unavuta sigara na una umri wa miaka zaidi ya 35 (ikiwa umri wako umezidi miaka 35, kuvuta sigara wakati unatumia kiraka inaongeza hatari ya madhara fulani-inashauriwa ujadili na mtoa matibabu wako [9]);
-unauzito zaidi ya poundi 198 au kilo 90 (ufanisi wa kiraka hupungua ikiwa una uzito wa zaidi ya kilo 90 [10]);
-unatokwa damu kwa hali isiyo kawaida na haija chunguzwa kimatibabu;
-una shinikizo la juu la damu ((hypertension); na
-una ugonjwa wa sukari kwa zaidi ya miaka 20 ambayo imesababisha matatizo kwa macho, neva au figo.
Ikiwa una dalili zozote ambazo zimetajwa hapo juu, ongea na mtoa matibabu aliyehitimu ili akupe mawaidha kuhusu njia ya uzuiaji mimba itakayokufaa zaidi.
Je, kuna kikomo kwa kiwango cha uzito unapaswa kuwa nacho ili utumie kiraka cha kuzuia mimba?
kwa msingi, kiraka kina ufanisi wa chini wa kuzuia mimba kwa wanawake ambao wana uzito zaidi ya poundi 198 au kilo 90. Ikiwa una uzito wa kilo 90 au zaidi, unapaswa kuzingatia kutumia njia ya uzuiaji mimba tofauti.