Manufaa ya kiafya
Kina ufanisi wa kuzuia mimba. Kwa matumizi ya kawaida au jinsi watu wengi hukitumia, kiraka huzuia mimba kwa wanawake 93 kati ya wanawake 100 wanaokitumia. Kwa matumizi kamili, kitazuia mimba kwa wanawake 99 kati ya wanawake 100.
Kinasaidia kupunguza matatizo mengine yanayohusiana na hedhi. Kwa mfano, kinaweza kufupisha hedhi na kupunguza maumivu ya hedhi na dalili kabla ya hedhi.
Kinaweza kufanya hedhi iwe ya kutabirika-kinaweza kufanya hedhi iwe ya kutabirika zaidi, nyepesi na bila maumivu.
Kina weza kupunguza dalili za ungonjwa wa endometriosis.
Kinatoa kinga dhidi ya saratani ya mji wa mimba na saratani ya ovari.
Kinapunguza hatari ya anemia ya upungufu wa madini ya chuma.
Kinapunguza hatari ya uvimbe kwenye ovari, ungonjwa za matiti wa fibrocystic breast syndrome, na
fibroadenomas.
Inaweza kumaliza chunusi
Inabaki na ufanisi hata ukitapika au unahara.
Manufaa kwa mtindo wa maisha
Inahitaji bidii kiasi. Ni chaguo bora kwa wanawake wanaotaka njia ya uzuiaji mimba iliyo sawa na tembe mchanganyo lakini bila wasiwasi wa kumeza tembe kila siku [6]
Ni rahisi kuweka-Nikama kubandika kipande cha selotepu (na unapaswa tu kukibadilisha kila wiki)
Hakikatizi ngono.
Inakupa hedhi inayotabirika. Ikiwa unapenda kupata hedhi kila mwezi, bila matone ya damu, basi kiraka kinaweza kuwa chaguo bora kwako.
Haicheleweshi kurudi kwa urutubisho wa kizazi. Utaweza kushika mimba punde baada ya kutoa kiraka. Ukiwacha kutumia kiraka na hauko tayari kushika mimba, badilisha uanze kutumia njia ingine ya uzuiaji mimba.