Kiraka cha kuzuia mimba (kudhibiti mimba)

Kiraka cha kuzuia mimba (kudhibiti mimba)
Kiraka cha kuzuia mimba (kudhibiti mimba)

Kiraka cha kuzuia mimba ni nini?

Kiraka cha kuzuia mimba pia kinajulikana kama kiraka cha kudhibiti mimba, ni kitu kidogo,chembamba chenye umbo wa mraba cha plastiki kinachonyumbulika ambacho kina bandikwa kwa mwili kuzuia mimba.Pia kinajulikana kama Ortho Evra au Evra, kiraka kinafanana na bengeji ya Band-Aid na kina upana wa chini ya sentimita 5.

Kiraka cha kuzuia mimba hufanya aje kazi?

Unabandika kiraka kwa ngozi yako, na inawachilia homoni bandia za projestini na estrojeni ndani ya mkondo wa damu kupitia ngozi. Homoni hizi ni sawa na homoni za projesteroni na estrojeni ambazo kiasili zinapatikana ndani ya mwili ya mwanamke. Homoni hizi mbili zinazuia ovari yako kuwachilia yai (kupevuka kwa yai). Pia zinafanya ute wa shingo ya kizazi uwe nzito ili kuzuia manii kufika kwa yai.

Kiraka cha kuzuia mimba kina ufanisi wa kiasi gani?

Kwa mwanamke wa kawaida, kutumia kiraka kina ufanisi wa asilimia 93 (wanawake 7 kati ya wanawake 100 wanaotumia kiraka kwa mwaka watashika mimba). Ikiwa hakuna makosa itafanyika kwa matumizi, kiraka kina weza kuwa na ufanisi wa hadi asilimia 99 wa kuzuia mimba.[1].

Kiraka cha kuzuia mimba hufanana aje?

Kiraka cha kuzuia mimba hutumika aje?

Kabla ya kupata njia hii ya uzuiaji mimba, ni muhimu kutembelea mtoa matibabu wako kwa uchunguzi wa kiafya kubaini ikiwa kiraka kitakufaa. Katika nchi zingine, utahitaji maagizo ya daktari kabla ununue kiraka cha kuzuia mimba.

Kiraka ni rahisi kutumia na inafanya kazi kama vile tembe mchanganyo. Kila kiraka kinafanya kwa wiki moja. Unabandika tu kiraka kipya kwa mwili wako, mara moja kila wiki, kwa wiki tatu mfululizo. Kwa wiki ya nne, hautumii kiraka.

Fikiria kwa makini kuhusu ni wapi unataka kukibandika kiraka-kitakuwa hapo kwa wiki nzima. Ni vyema kutoweka kiraka sehemu ya ngozi iliyolegea au iliyo na mikunjo mingi. Hakikisha kila mara kwamba eneo utabandika kiraka liko safi na limekauka na halina kidonda, haliwashi, na halina nywele nyingi. Haupaswi kukiweka kwenye eneo ambalo kita ambuliwa na nguo ya kubana.
Ambua tu nusu ya plastiki angavu kwanza, ili ubaki na sehemu ya kushika isiyo nata.Usiguse sehemu ya kunata na vidole vyako.
Finyilia kiraka kwenye sehemu ya mwili uliochagua. Kifinyilie kwa sekunde 10 ili kijibandike vizuri.
Cha muhimu kabisa ni kukumbuka kutumia kiraka kipya kila wiki. Hii itasaidia kuweka ufanisi chake cha kuzuia mimba.

Ni wapi pa kubandika Kiraka cha kudhibiti mimba?

Unaweza kuweka kiraka kwenye tako, bega, nyonga, tumbo, sehemu ya nje wa juu ya mkono au eneo la kifua. Usiweke kwenye matiti, viungo vya uzazi,nyayo za miguu yako, au viganja vya mikono yako. Kiraka kinapaswa kuwa kwenye mwili wako kila mara, mchana na usiku [2].

Je Kiraka cha kuzuia mimba kina simamisha hedhi?

Pengine utapata hedhi yako katika ile wiki haujatumia kiraka. watu wengine hawapati hedhi kabisa. Mara wiki ya nne imepita, anza kutumia kifungu kingine cha viraka kwa kuweka kiraka kipya kwa ngozi yako. Huenda bado hedhi inaendelea ikifika wakati wa kuweka kiraka kingine. Hii ni jambo la kawaida. Weka tu kiraka kipya.

Angalia vidokezi na mbinu hapa chini ya kufanya iwe rahisi kutumia kiraka.

Kidokezi 1: Ikiwa utaanza kutumia kiraka ndani ya siku tano za kwanza za hedhi yako, unakingwa dhidi ya mimba mara hio hio. Ikiwa ni nje ya hizi siku tano za kwanza, itachukua siku saba kabla kiraka kikupe kinga. Utahitaji kutumia njia ya ziada ya kujikinga wakati huo.
Kidokezi 2: Ikiwa una mzunguko wa hedhi mfupi yenye hedhi inayokuja kila siku 23 au kidogo, huenda hautapata kinga dhidi ya mimba ukianza kutumia kiraka cha kuzuia mimba siku ya tano ya hedhi yako au baadaye na kwa hivyo, utahitaji njia ya ziada ya uzuiaji mimba kwa siku saba za mwanzo [3].
Kidokezi 3: Usitumie losheni ya mwili, mafuta, poda, sabuni zenye rangi ya malai au vipodozi pahala pana kiraka. Inaweza kufanya kiraka kisijibandike.
Kidokezi 4: Angalia kiraka chako kila siku kuhakikisha kimejibandika vizuri.Kuna uwezekano wa kuwa na nyuzinyuzi kwenye upindo wa kiraka.
Kidokezi 5: Ukitoa kiraka, kikunje katikati kabla ya kukitupa. Hili litasaidia homoni zisiingie kwenye mchanga. Usikitupe kwa choo cha maji.

Ni nini itafanyika ikiwa nitasahau kutoa kiraka?

Ikiwa umesahau kutoa kiraka wakati wa wiki ya mapumziko, unapaswa tu kutoa kile nzee na uweke kipya. Kisha, hakikisha kwamba umekibadilisha siku yako ya kawaida ya kubadilisha. Bado unapata kinga dhidi ya mimba ikiwa ulikitumia kwa njia sahihi hadi uliposahau kukitoa.
Ikiwa imepita saa 48 tangu wakati ulipaswa kubadilisha kiraka, weka tu kiraka kipya na ukibadilishe siku yako ya kawaida ya kubadilisha. Juu ya hayo, tumia njia ya uzuiaji mimba ya ziada kwa siku saba za kufuata. Ikiwa ulifanya ngono siku chache zilizopita, hakikisha umetumia njia za dharura za uzuiaji mimba.
Ikiwa umesahau kutoa kiraka cha kuzuia mimba baada ya wiki ya tatu, toa kile kiraka nzee haraka iwezekanavyo na uanze wiki yako bila kiraka. Kisha anza kutumia kifungu kingine cha kiraka kwa siku yako ya kawaida. Hii inamaanisha utakuwa na wiki mfupi bila kiraka. Pia umekingwa dhidi ya mimba na hautahitaji njia ya uzuiaji mimba ya ziada [4].

Contraception Quiz

Not sure on the method? - Take our dynamic Contraception Quiz.
When it comes to sex, protection is as important as pleasure. But what should one do to start their safe sex journey? Answer some simple questions and based on the responses, we will recommend the next steps.

Take the quiz
External Condom

Compare with similar Contraceptive Methods

Are you wondering if condoms are better than daily pills? Or if you should opt for a birth control implant? We're here to assist you in making this decision. You can select up to 5 contraceptive methods and compare them side by side to weigh the pros and cons of each.

Give a try to our Contraceptive Tool

In the example below, you'll find similar methods to the one you're currently reading about. Feel free to click on any that catch your interest or revisit our Contraceptive Methods page

Our Monthly Top Articles

Mnong’onezaji wa mambo ya uke: Jinsi ya kupenda uke wako hivyo ilivyo

Mnong’onezaji wa mambo ya uke: Jinsi ya kupenda uke wako hivyo ilivyo

Kabla tuzungumzie mambo ya kuthamini uke, tucheze mchezo ambapo una alama 50 kutoka mwanzo. Nina orodha ya maswali 5 na ikiwa umawahi fanya kile kilichoulizwa kwenye swali, unapoteza alama 10. Twen...

Njia 6 tunaweza kuchukua udhibiti wa uzazi wa mpango kama wanaume

Njia 6 tunaweza kuchukua udhibiti wa uzazi wa mpango kama wanaume

Ingawa ngono salama ni jukumu la wanaume na wanawake, mambo ya uzazi wa mpango imechukuliwa tangu kitambo  kama jukumu la mwanamke. Ingekuwa wanaume wangechukua jukumu la kutumia njia za kuzuia mim...

Mnong’onezaji wa mambo ya uke: Jinsi ya kupenda uke wako hivyo ilivyo

Mnong’onezaji wa mambo ya uke: Jinsi ya kupenda uke wako hivyo ilivyo

Kabla tuzungumzie mambo ya kuthamini uke, tucheze mchezo ambapo una alama 50 kutoka mwanzo. Nina orodha ya maswali 5 na ikiwa umawahi fanya kile kilichoulizwa kwenye swali, unapoteza alama 10. Twen...

Njia 6 tunaweza kuchukua udhibiti wa uzazi wa mpango kama wanaume

Njia 6 tunaweza kuchukua udhibiti wa uzazi wa mpango kama wanaume

Ingawa ngono salama ni jukumu la wanaume na wanawake, mambo ya uzazi wa mpango imechukuliwa tangu kitambo  kama jukumu la mwanamke. Ingekuwa wanaume wangechukua jukumu la kutumia njia za kuzuia mim...

Mnong’onezaji wa mambo ya uke: Mambo yanayohatarisha uke na njia za kuitunza

Mnong’onezaji wa mambo ya uke: Mambo yanayohatarisha uke na njia za kuitunza

Uke ni sehemu moja ya mwili isiyoeleweka vizuri. Ingekuwa uke wako ungeweza kuongea,  ungekuambia nini? Nadhani unge changanyikiwa cha kusema. Mara tunaona makala inayosema safisha uke wako na tena...