Ni jambo la asili kuvutiwa na mtu. Ikiwa unafikiria kufanya ngono baada ya kipindi cha kujinyima ngono, ni muhimu uchukue muda kuwaza kuhusu sababu zako za kungoja.
Ukiamua hautafanya ngono sasa hivi, zungumza na mwenzi wako kuhusu sababu zako za kutofanya ngono. Pia zungumza kuhusu vitu unavyoweza kufanya na vile hauwezi.
Ukiamua kwamba unataka kuanza kufanya ngono, zingatia kutumia njia ya uzuiaji mimba ambayo itakufaa. Hakikisha umefanya hivyo kabla ya kufanya ngono.
Chochote utakacho amua, zingatia kukuwa na njia za uzuiaji mimba kama kondomu za nje (kiume), kondomu za ndani (kike) na njia za dharura za uzuiaji mimba, endapo utazihitaji.
Bado haiendi sawa? Ikiwa “Sio sasa hivi” haiwezekani tena, zingatia njia ya uzuiaji mimba ambayo unaweza kutegemea (na inayopatikana kwa urahisi) kabla uanze kufanya ngono. Zingatia njia ya kufanya kwa muda na ambayo athari zake zinaweza geuzika.
Jaribu njia tofauti: kondomu za ndani (kike); vipandikizi; IUD; kondomu za nje (kiume); sindano.
References:
- World Health Organization Department of Reproductive Health and Research and Johns Hopkins Bloomberg School of Public Health Center for Communication Programs (2018) Family Planning: A Global Handbook for Providers. Baltimore and Geneva. Retrieved from https://apps.who.int/iris/bitstream/handle/10665/260156/9780999203705-eng.pdf?sequence=1