Tembe | Find My Method
 

Last modified on October 13th, 2020

birth-control-pill
 • Tembe imekuwa kwa miaka takriban 50. Nirahisi kumeza na inaweza kuwa na madhara chanya.
 • Ufanisi: Tembe ina ufanisi ikichukuliwa kikamilifu, lakini wanawake wengi hawaichukui kikamilifu. Kwa matumizi kamilifu, wanawake 99 kati ya 100 wataweza kuzuia mimba. Kwa matumizi ya kawaida, ama jinsi watu wengi huitumia, tembe huzuia mimba kwa wanawake 91 kati ya 100 wanaoitumia.
 • Madhara: Za kawaida zaidi ni ulaini wa matiti, kichefuchefu, matone ya damu na kupungua kwa tamaa ya ngono
 • Jitihada: nyingi .Unahitaji kumeza tembe saa sawa kila siku.
 • Haikingi dhidi ya magonjwa ya zinaa (STI)

Ufupisho

Birth Control Pill

Summary Contraceptive Pill

“Tembe”ni kidonge kidogo na inakuja ikiwa imewekwa kwa kifurushi cha kila mwezi. Watu wengine huiita “njia ya mdomo ya kuzuia mimba” Unaimeza mara moja kwa siku, saa sawa kila siku. Kuna aina nyingi za tembe zinazopatikana, na pia aina mpya hupatikana mara nyingi. Nyingi zao hufanya kazi kwa kuachilia homoni inayozuia ovari kuachilia yai. Homoni pia hufanya ute wa shingo ya kizazi uwe nzito, na kuzuia mbegu za kiume kufikia yai.

Aina za tembe [5]:

Mchanganyo. Tembe za mchanganyo hutumia aina mbili za homoni-estrojeni na projestini kuzuia kupevuka kwa yai. Kifurushi cha mwezi cha tembe za mchanganyo huwa na tembe za homoni za wiki 3 na tembe bila homoni za wiki 1. Utameza tembe bila homoni ukingoja hedhi yako kila mwezi.

Projestini pekee. Tembe hizi hazina estrojeni ndani na zinapendekezwa ikiwa huwezi tumia estrojeni, au ikiwa tembe za mchanganyo hukuletea madhara. Zinawachilia kiwango kidogo cha projestini kila siku ya mwezi na hazikuletei hedhi kwa wiki uliotarajiwa.

Maelezo

[13]
Tembe huhitaji nidhamu. Unahitaji kukumbuka kumeza tembe kwa saa sawa kila siku. Usipoimeza kwa saa sawa kila siku, haitafanya kazi vizuri sana.

Unataka hedhi za kutabirika. Ikiwa Unapenda kupata hedhi kila mwezi, bila matone ya damu, basi tembe itakua chaguo nzuri.

Unaweza kosa kupata hedhi. Tembe zingine zitafanya usipate hedhi kabisa, na hio ni salama kwa asili mia 100.

Wavuta sigara wa miaka zaidi ya 35, muwe waangalifu. Kwa wanawake walio na miaka zaidi ya 35, kuvuta sigara wakati unatumia tembe kunaongeza hatari ya madhara fulani. Unashauriwa kuzungumzia swala hili na mtoaji wako wa matibabu.

Unataka kukomesha matumizi ya njia ya kupanga uzazi na ushike mimba haraka. Utaweza kushika mimba siku chache baada ya kuwacha tembe. Ukiwacha kutumia tembe na hauko tayari kushika mimba, tumia njia ingine ya kuzuia mimba.

Jinsi ya kutumia

Ikiwa unaweza kumeza dawa ya aspirini, unaweza kutumia tembe. Lakini cha muhimu: Lazima ukumbuke kuimeza kila siku, kwa saa sawa, hata iwe nini.

Tembe zingine zinakuja ndani ya vifurishi vya siku 21. Zingine ndani ya vifurishi vya siku 28. Zingine zitakuwezesha kuwa na hedhi ya kawaida kila mwezi. Zingine zitakuletea hedhi mara moja ndani ya miezi 3. Na zingine zitafanya ukose hedhi mwaka mzima.Kuna aina nyingi za tembe zinapatikana, na zinaweza kukukanganya. Mtoaji huduma za afya au mfanyakazi wa afya ya jamii aliye pata mafunzo anaweza kukusaidia kuamua tembe gani inakufaa [1].

Madhara

Kila mtu ni tofauti. Kile unachopitia pengine hakitafanana na mtu mwingine.

Mambo chanya: Kuna vitu vingi kuhusu tembe ambavyo ni vizuri kwa mwili wako na pia maisha yako ya ngono [7].

 • Tembe ni rahisi kutumia-imeze tu kwa maji.
 • Sio lazima ukatize ngono kuitumia
 • Unaweza kuwa na hedhi nyepesi
 • Inakupa udhibiti juu ya wakati wa kupata hedhi
 • Tembe zingine humaliza chunusi
 • Inaweza kupunguza maumivu ya tumbo wakati wa hedhi na dalili za kabla ya hedhi (PMS).
 • Tembe zingine zitakupa kinga dhidi ya matatizo mengine ya kiafya: Saratani ya ndani ya mji wa mimba na saratari ya ovari; anemia ya upungufu wa madini ya chuma; Uvimbe kwenye ovari na ugonjwa wa uvimbe wa fupanyonga

Mambo hasi: Kila mtu huwa na wasiwasi juu ya madhara hasi, lakini kwa wanawake wengi, hakuna shida. Ukipata madhara, huenda yakaisha. Kumbuka, unaingiza homoni mwilini mwako, kwahivyo inaweza kuchukua miezi michache mwili izoe. Ipe muda.

Vitu ambavyo pengine vitaisha baada ya miezi 2 au 3 [10]:

 • Matone ya damu
 • Vidonda kwenye matiti
 • Kichefuchefu na kutapika

Vitu ambavyo vinaweza kuwa muda mrefu:

 • Mabadiliko kwa tamaa yako ya ngono

 

Ikiwa baada ya miezi 3 unahisi kwamba madhara yamezidi kiwango unachoweza kuvumilia, tumia njia ingine uwe na kinga. Kondomu itakupa kinga bora wakati unatafuta njia itakayofaa mahitaji yako.Kumbuka, kuna njia kwa kila mtu, kila mahali!

* Kwa idadi ndogo mno ya wanawake, kuna hatari ya madhara makubwa.

Maswali yanayoulizwa mara kwa mara

Tuko hapa kukusaidia. kama bado unahisi sio ya kufaa, tuna mawazo ya njia zingine. Kumbuka tu: Ukiamua kubadilisha njia, hakikisha una kinga wakati unafanya mabadiliko. Kondomu zitakupa kinga bora wakati unatafuta njia itakayofaa mahitaji yako.

Je, napaswa kuwa na wasiwasi juu ya matone ya damu [4]?

 • Kutokwa matone ya damu inaweza kusababishwa na matumizi ya njia tofauti. Haupotezi damu nyingi ukitokwa na matone ya damu, hata ikiwa inaweza kuonekana hivyo
 • Bado haiendi sawa? unaweza kuwa na bahati nzuri zaidi ukitumia tembe iliyo na dozi ya juu kidogo ya estrojeni au inayokupa estrojeni wakati wa sehemu tofauti wa hedhi yako
 • Jaribu njia tofauti: IUD

Je, tembe itaniletea saratani [13]?

 • Tembe haikuletei saratani. Kwa visa vichache sana, wanawake wanaweza kupata tatizo la damu kuganda. Hatari ya damu kuganda wakati unatumia tembe iko chini kuliko hatari ya damu kuganda ukiwa na mimba. Wanawake wengine wana matatizo za kiafya ambayo humaanisha hawafai kutumia tembe.
 • Ukiwa mwenye afya, tembe za kuzuia mimba ziko salama. Zinaweza kukusaidia kwa shida wakati huu (kama anemia inayosababishwa na hedhi nzito) na baadaye maishani (zinaweza kukukinga dhidi ya aina zingine za saratani)

Je,napaswa kuwa na wasiwasi juu ya damu kuganda?

 • Uko na hatari mdogo mno wa kupata tatizo la kuganda damu wakati unatumia tembe. Hata hivyo, kuna hali za kijeni au za kimatibabu ambazo zinaongeza hatari ya kupata tatizo la damu kuganda.Ukiwa na historia ya tatizo la damu kuganda au wasiwasi maalum kuhusu tatizo la damu kuganda, uliza anayekupa njia za kuzuia mimba kama kweli tembe ni chaguo bora kwako.

Na ikiwa nitapata shida kukumbuka kumeza tembe [10]?

 • Jaribu kuweka kumbusho kwa simu yako ya mkono.
 • Bado haiendi sawa? Ukiweka mfumo wa kumbusho na bado una shida kukumbuka, pengine uzingatie njia ambayo hauhitaji kuweka mawazoni kila wakati.
  • Unahitaji tu kukumbuka kubadilisha kiraka mara moja kwa wiki.
  • Unahitaji tu kuwa na wasiwasi kuhusu pete kila mwezi.
  • Pia kuna njia unaweza sahau kuhusu kwa miaka mingi: Tazama aina mbili za IUD na vipandikizi.
 • Jaribu njia tofauti: vipandikizi; IUD ; kiraka ; pete

Je ni jambo la kawaida kupata chunusi [5]?

Mbona tembe inanifanya niwe na kichefuchefu [8]?

 • Jaribu hili:Ukitaka kuendelea na tembe unazotumia sasa, jaribu kuzimeza usiku. Unaweza pia kuzingatia kutumia tembe zilizo na kiwango cha chini cha estrojeni.
 • Bado haiendi sawa? Pengine ujaribu njia nyingine ya homoni ambayo haipiti kwa mdomo, kama vile vipandikizi; an  IUD; kiraka; pete; sindano
 • Jaribu njia tofauti: vipandikizi; IUD; kiraka; pete; sindano

Mbona natokwa na damu kabla na baada ya hedhi [4]?

 • Ikiwa umeanza kutumia tembe ndani ya miezi michache iliyopita, jaribu kuvumilia-shida hii itaisha yenyewe. Hakikisha kwamba unameza tembe wakati sawa kila siku bila kukosa siku moja na kumeza mbili pamoja siku ingine.Kukosa kumeza tembe au kumeza tembe mbili pamoja kunaongeza uwezekano wa kutokwa matone ya damu.
 • Bado haiendi sawa? Ikiwa umekuwa ukitumia tembe kwa miezi michache, unazitumia sahihi, na bado unatokwa matone ya damu, basi zingatia njia mpya. Pia unapaswa kupimwa magonjwa ya zinaa na mimba, ili kuhakikisha sio hizo zinasababisha utokwaji wa damu.
 • Jaribu njia tofauti: kiraka; pete; sindano

Na nikisafiri niende ukanda wa muda tofauti? Ninapaswa kubadilisha saa ya kumeza tembe?

Kuna chaguo tofauti [13]:

Chaguo la 1: Tumia saa za nchi yako

 • Unahitaji kujua saa za nchi yako na umeze tembe kwa hizo saa. Kwa mfano, Ukiishi mji wa Mexico na usafiri uende Morocco ambayo ni masaa 6 mbele, unastahili kumeza tembe zako masaa 6 baadaye kuliko kawaida kwa siku. Kwahivyo, ukiwa unameza tembe zako saa tatu asubuhi ukiwa Mexico, zimeze saa tisa alasiri ukiwa Morocco.
 • Ikiwa uliweka king’ora kwenye simu kikukumbushe saa ya kumeza tembe, hakikisha umekibadilisha inavyotakikana ukiwa safarini.

Chaguo la 2: Kufuata ukanda wa muda mpya

 • Ikiwa rahisi zaidi, au ikiwa unahamia eneo lingine kwa muda mrefu, unaweza badilisha mpangilio wako wa kumeza tembe, bora usimalize masaa 24 bila kumeza tembe.Kwahivyo, ukiishi mji wa Mexico na uende Morocco na unataka kuendelea na mpangilio wa saa tatu asubuhi, ni sawa kabisa kumeza tembe zako saa tatu asabuhi, saa ya Morocco,( masaa 18 baada ya tembe yako ya mwisho Mexico).

Ikiwa unasafiri kwa muda mrefu na utahitaji kifurushi kingine cha tembe ukiwa safarini, usisahau kuibeba kwenye begi lako. Ikiwa ulilazimishwa kusafiri ghafla, na hukupata nafasi ya kubeba tembe zako (k.m uko maeneo ya msiba), jaribu kutafuta mtoaji wa mtaa wa huduma za afya au mtoaji wa huduma za afya ya jamii punde iwezekanavyo kwenye eneo lako jipya. Tumia mbinu za asilia za kuzuia mimba wakati ambao bado huwezi pata njia zingine kama kondomu.

Bado haiendi sawa? Ikiwa wewe husafiri sana na unapenda njia ya homoni, pengine ungependa kubadilisha njia utumie pete au kiraka ili usiwe na wasiwasi kuhusu kanda za muda. Ukitaka kusahau kabisa mambo ya kupiga hesabu kanda za muda, chunguza vipandikizi au IUD.

Jaribu njia tofauti: vipandikizi; IUD; kiraka pete

Nilikosa kumeza tembe, au nilimeza tembe kuchelewa. Nifanye nini [6]?

 • Meza tembe yako ya kufuata punde tu unapokumbuka, na utumie njia ingine kwa siku 7 baada ya hapo. Ikiwa ilisahau kumeza tembe bila homoni wa wiki ya 4,tupa hio tembe bila homoni kwa hiyo siku na rudi kwenye mpangilio siku ifuatayo.
 • Ikiwa umefanya ngono tangu uende nje ya mpangilio wako wa kumeza dawa, na ni ndani ya siku 5 zilizopita, zingatia kutumia njia ya dharura ya kuzuia mimba.

Jana nilikosa kumeza tembe. Je ni salama kumeza tembe mbili siku moja?

 • Ikiwa ulikosa kumeza tembe basi saa zingine inapendekezwa umeze tembe mbili siku moja. kumeza tembe mbili angalau masaa 10 kati yao haileti shida. kuzimeza zikikaribiana kunaweza kukufanya uwe na kichefuchefu, na hufai kutapika baada ya kumeza tembe.
 • Ukitaka kutumia tembe za kawaida za kuzuia mimba kama njia ya dharura ya kuzuia mimba, unaweza meza tembe 2-4 pamoja.
 • Ikiwa imepita masaa 24 tangu umeze tembe ya mwisho, tumia njia ya pili, kama vile kondomu au  kondomu ya ndani (kike) wakati wowote umefanya ngono kwa siku 7 zijazo.

Na nikitaka kuanza kumeza tembe saa tofauti kila siku?

 • Hio ni sawa. Njia rahisi kabisa kufanya hivyo ni kuanza kifurushi chako kinachofuata wakati unapendelea.Utahitaji pia kutumia njia ingine ukifanya hivi.
 • Ikiwa huwezi kungoja kutumia kifurushi kinachofuata, hakikisha tu kwamba hungoji zaidi ya masaa 24 kati ya tembe ya mwisho na inayofuata.

Je, tembe inaharibu mazingira [13]?

 • Njia yoyote ni bora kuliko kutotumia njia yoyote, ikifika kwa swala la mazingira.
 • Homoni zingine kutoka kwa tembe zitaingia kwenye mazingira kupitia mkojo wa mwanamke. Lakini ni kiwango kidogo kushinda vyanzo vingine vya estrojeni katika mazingira.
 • Estrojeni kutoka kwenye michakato ya viwanda na uzalishaji, mbolea na viuadudu, na madawa yanayopewa wanyama yote yanaingia katika mazingira kwa viwango vikubwa kushinda estrojeni kwa mkojo wa mwanamke kutoka kwenye tembe.
 • Ikiwa hutaki kuongeza homoni kwenye mazingira au mwilini mwako, kuna njia zingine unaweza kutumia. Kondomu zenye ulimbo wa mpira ( latex) na IUD ya shaba yote ni bora. Chochote utakacho amua, chagua njia na uendelee kuitumia.
 • Bado haiendi sawa? Ikiwa unataka kutumia njia yenye ufanisi wa juu bila homoni, jaribu IUD bila homoni.
 • Jaribu njia tofauti: IUD

Je, tembe inazuia mimba ikiwa natumia dawa za antibaotiki?

 • Rifampin ndio antibaotiki pekee ilipatikana kupunguza ufanisi wa tembe. Inatumika kwa kawaida kutibu kifua kikuu.
 • Ikiwa unahitaji kumeza rifampin, zungumza na mtoaji wako kujua njia gani itakuwa bora kwako.

Na ikiwa nilitapika baada ya kumeza tembe [9]?

 • Ukitapika ndani ya masaa 2 ya kuchukua tembe, ichukulie kama kukosa kumeza tembe. Meza tembe inayofuata kwenye kifurushi mara hio hio.
 • Tumia njia ya pili, kama vile  kondomu za ndani (kite), kwa siku saba zijazo kuhakikisha uko salama.

Na ikiwa nilihara baada ya kumeza tembe?

 • Kuhara saa zingine huenda haitaathiri ufanisi wa tembe.
 • Mharo mkali (mara kadhaa kwa siku) unaweza athiri ufanisi wa tembe.
 • Unapaswa kutumia njia ya pili (kama kondomu) ukiwa na mharo mkali. Unapaswa kutumia njia ya pili kila wakati unafanya ngono ukiwa mgonjwa, na kwa siku saba baada ya kupona.
 • Bado haiendi sawa? kusahau kumeza tembe, kutapika punde baada ya kumeza tembe, au kuwa na mharo mkali ndizo sababu tembe ina kiwango cha asilimia 9 ya kufeli. Kama hiyo ni hatari kwako, tumia njia ya pili, ama ubadilishe utumie njia inayohitaji jitihada kidogo.
 • Jaribu njia tofauti: kondomu; vipandikizi; IUD ; pete

Ni salama kutumia tembe kwa miaka bila kuwacha [13]?

 • Ukitaka kushika mimba, unastahili tu kuwacha kutumia tembe.Tafiti kuhusu tembe kwa miaka zinaonyesha kwamba kutumia tembe kwa miaka haita athiri uwezo wako wa kushika mimba mara ukiwacha kutumia tembe.
 • Ukiwa na utokwaji wa matone ya damu, kuwacha tembe kwa muda kutasaidia kuipunguza. Ukitaka kupumzika kidogo, wacha tembe kwa siku 3-7. Tumia njia ya pili, kama kondomu, kila wakati unafanya ngono wakati umewacha tembe na kwa siku saba za kwanza baada ya kuanza kutumia tembe tena.
 • Bado haiendi sawa? ikiwa wewe huvuta sigara au una hali ya kimatabibu ambayo itafanya tembe iwe hatari kwako, zingatia kutumia njia ya projestini pekee badala yake.
 • Jaribu njia tofauti: vipandikizi; IUD; sindano

 

References

[1] Cooper, D. B., & Mahdy, H. (2019). Oral Contraceptive Pills. StatPearls Publishing. Retrieved from https://www.ncbi.nlm.nih.gov/books/NBK430882/
[2] Dr Marie Marie Stopes International. (2017). Contraception. Retrieved from http://www.mariestopes.org.au/wp-content/uploads/Contraception-brochure-web-200417.pdf
[3] FSRH The Faculty of Sexual & Reproductive Healthcare. (Amended 2019). UK MEDICAL ELIGIBILITY CRITERIA. RCOG, London. Retrieved from https://www.fsrh.org/standards-and-guidance/documents/ukmec-2016/
[4] FSRH Faculty of Sexual and Reproductive Healthcare. (Amended 2019). Faculty of Sexual & Reproductive Healthcare Clinical Guidance: Progestogen-only Pills. Retrieved from https://www.fsrh.org/standards-and-guidance/documents/cec-ceu-guidance-pop-mar-2015/
[5] FSRH The Faculty of Sexual & Reproductive Healthcare. (Amended 2019). FSRH Guideline: Combined Hormonal Contraception. Retrieved from https://www.fsrh.org/standards-and-guidance/documents/combined-hormonal-contraception/
[6] Family Planning NSW. (2015). The Combined Oral Contraceptive Pill. Retrieved fromhttps://www.fpnsw.org.au/sites/default/files/assets/combined_oral_contraceptive_pill.pdf
[7] FPA the sexual health charity. (2019). Your guide to the combined pill. Retrieved from https://www.fpa.org.uk/sites/default/files/the-combined-pill-your-guide.pdf
[8] Reproductive Heath Access Project. (2019). The pill. Retrieved from https://www.reproductiveaccess.org/wp-content/uploads/2014/12/factsheet_pill.pdf
[9] SHINE SA. (2017). Fact Sheet: The Pill. Retrieved from https://www.shinesa.org.au/media/product/2015/04/The-Pill.pdf
[10] Shukla, A., & Jamwal, R. (2017). Adverse effect of combined oral contraceptive pills. Asian Journal of Pharmaceutical and Clinical Research, 10. Retrieved from https://www.researchgate.net/publication/312596820_Adverse_effect_of_combined_oral_contraceptive_pills
[11] Society of Obstetricians and Gynaecologists of Canada. (2017). Canadian Contraception Consensus Chapter 9: Combined Hormonal Contraception. Retrieved from https://www.jogc.com/article/S1701-2163(16)39786-9/pdf
[12] The Royal Women’s Hospital and Family Planning Victoria. (2018). THE CONTRACEPTIVE PILL. Retrieved from https://thewomens.r.worldssl.net/images/uploads/fact-sheets/Contraception-the-pill-2018.pdf
[13] World Health Organization Department of Reproductive Health and Research and Johns Hopkins Bloomberg School of Public Health Center for Communication Programs (2018) Family Planning: A Global Handbook for Providers. Baltimore and Geneva. Retrieved from https://apps.who.int/iris/bitstream/handle/10665/260156/9780999203705-eng.pdf?sequence=1
[14] World Health Organization. (2016). Selected practice recommendations for contraceptive use. Geneva. Retrieved from https://apps.who.int/iris/bitstream/handle/10665/252267/9789241565400-eng.pdf?sequence=1


lang Kiswahili