Mnong’onezaji wa mambo ya uke: Jinsi ya kupenda uke wako hivyo ilivyo

Mnong’onezaji wa mambo ya uke: Jinsi ya kupenda uke wako hivyo ilivyo

Kabla tuzungumzie mambo ya kuthamini uke, tucheze mchezo ambapo una alama 50 kutoka mwanzo. Nina orodha ya maswali 5 na ikiwa umawahi fanya kile kilichoulizwa kwenye swali, unapoteza alama 10.
Twende:

  1. Umewahi kushikwa na wasiwasi kuhusu rangi ya ngozi kwenye mapaja yako ya ndani?
  2. Umewahi kutumia dawa za kubana uke?
  3. Umewahi kupitisha mvuke ukeni?
  4. Umewahi kujaribu kufanya uke wako unukie vizuri?
  5. Umewahi fikiria kwamba wewe hukojoa kupitia uke?

Umebaki na alama ngapi? Ikiwa hauna alama yoyote iliyobaki, huenda una tatizo la kutothamini uke wako jinsi ilivyo.

Resting in bath. Beautiful curly dark-skinned woman feeling amazingly good while resting in bath thinking about vagina insecurities and vagina self-esteem

Kuthamini uke

Utunzaji wa uke unamaanisha jinsi unavyothamini uke wako. Inamaanisha kuwa na mawazo chanya kuhusu sehemu yako ya siri. Wanawake wengi huwa na matatizo ya kutoridhika na uke wao kwasababu za fikra za kitamaduni, ambazo huzungumzia uke vibaya hadi tunaamini mambo fulani kuhusu uke kamili na haswa “designer vagina”. 

Designer vagina” ni nini? Ni upasuaji mdogo wa urembo wa kuifanya uke upendeze kuangalia. Kwa muda, tumeona uke laini isiyo na chunusi, iliyo na rangi bora zaidi, iliyo na midomo ndogo na yenye rangi kama ya waridi, na tunafikiria kwamba hakuna uke zilizo na madoadoa au tunadhani kwamba kuwa na chunusi inamanisha uke ni mchafu.

Kuwacha nywele ya sehemu ya siri sikuhizi ni kama mwiko; uke ukiwa laini sana wanakuchukulia kama malaya ambaye amelala na wanaume wengi sana ndio maana uume unaingia kwa urahisi. Haya yote ambayo ni mambo ya kawaida sikuhizi yamekuwa mambo ya kuleta aibu.

Beautiful sexy woman with no vagina shame and high vagina self esteem

Kutothamini uke kuna athiri kwa ujumla kujithamini kwetu. Inatuathiri pakubwa. Inaweza kuwa sababu bado haujawai fika kileleni, kwani wanawake wasiothamini uke zao hupata matatizo kufika kileleni. Ni kwasababu tunakosa kujithamini kijinsia na swala la kijinsia inajumuisha mambo mengine kama za kihisia, kiakili, kitamaduni na uhusiano na wengine.

Kuongeza kuthamini uke

Uzuri ni kuwa tunaweza kujifunza kuthamini uke; pata vidokezo hapa kukusaidia kuboresha jinsi unavyothamini uke wako.

Chunguza mambo yanayokuletea aibu.

Kuwa na aibu hutufanya tuwe wanyonge na kuathiri tunavyojithamini. Hili huwa ukweli kwa uke pia; chunguza ni kipi kinakufanya uhisi vibaya kuhusu uke wako. Hili ndilo hatua ya kwanza na muhimu kuboresha jinsi unavyothamini uke wako.

Sahau habari ulizopata

Habari nyingi za kutufanya tuhisi vibaya kuhusu uke zetu huwa sio sahihi au huwa za uongo. Kwamfano, habari kama uke wako unastahili kunukia vizuri au unastahili kuwa na rangi sawa wakati wote. Itabidi usahau mambo kama haya. Njia moja ya kufanya hivi ni kuandika chini kila kitu unafikiria unajua kuhusu uke wako, kisha uthibitishe mambo hayo. Unaweza kutafuta ukweli kwenye tovuti za kuaminika, soma vitabu, uliza wataalamu kujua ukweli wa mambo.

Jifunze tena

Baada ya kuthibitisha na kusahau habari za uongo, anza kujifunza habari mpya kuhusu uke wako. Kuna kurasa za mitandaoni zilizo na habari sahihi za kimatibabu kuhusu uke zenye afya.

Tetea

Kuwa na mawazo chanya kuhusu uke na kuizungumzia na wengine kuna nguvu, na pia hukusaidia kuthamini uke wako zaidi. Kwa kufanya hivi, unaimarisha mawazo chanya kuhusu uke lakini pia unawapa wengine habari kusuhu kuthamini uke.

Two beautiful sexy women, lesbian couple enjoying each other at home - having no vagina shame and high vagina self esteem

Chukua muda wako ufuate vidokezo hivi. Kisha ujibu yale maswali tena. Nina uhakika hautapoteza alama yoyote.

Makala hii ni sehemu ya makala yetu ya Mnong’onezaji wa mambo ya uke. Unaweza kusoma sehemu ya kwanza hapa.

Je, una jambo la kusema?Wacha ujumbe wako hapa chini, wasiliana nasi kwenye kurasa zetu za mitandao ya  kijamii: Facebook, Instagram na Twitter au tutumie barua pepe kwenye info@findmymethod.org. Kwa taarifa zaidi kuhusu njia za uzuiaji mimba, tembelea  findmymethod.org

Kuhusu mwandishi: Amos Sanasi ni mdemografia, na mtaalamu wa maswala yanayohusiana na ngono na pia mwanzilishi wa jina la  rajamu la mambo chanya kuhusu ngono la kwanza nchini Nigeria Revaginate NG ambalo linatoa taarifa za kina kuhusu ngono na vifaa vya ngono, haswa kwa watu walemavu. Yeye huandika kwenye akaunti ya twitter @thesanasi.