Uke ni sehemu moja ya mwili isiyoeleweka vizuri. Ingekuwa uke wako ungeweza kuongea, ungekuambia nini? Nadhani unge changanyikiwa cha kusema. Mara tunaona makala inayosema safisha uke wako na tena baadaye tunaona ingine ikisema “kwanini kusafisha uke” ni hatari kufanya.
Kuna habari nyingi zisizo thibitishwa mtandaoni, mara nyingi, tunadanganywa kufanya hivi na vile ‘kutunza’ uke. Kwa ukweli, kutunza uke kunahusu tu kufanya maamuzi kubadilisha mtindo wa maisha ili uke uwe na afya bora.
Hatua ya kwanza ya utunzaji ni kubaini chanzo cha matatizo; Pata orodha hapa ya mambo yanayoweza kuhatarisha uke:
1) Wasiwasi
Haukutarajia hili liwe kwenye orodha, sivyo? Lakini wasiwasi unaweza kuleta hali ya ukosefu wa usawa kwenye homoni na hili linaweza kuleta matatizo kwenye afya ya uke.
Pia, kujikuna uke ni kawaida kwa wanawake wengine wanapokuwa na wasiwasi; Unawashwa na unajikuna na unahisi kujikuna zaidi kwasababu pengine una vijidonda vidogo vidogo vilivyosababishwa na kujikuna na vijindonda hivi huwasha na mzunguko wa kujikuna na kuwasha unaendelea.
2) Kemikali
Mara nyingi, tunaweka kemikali kwenye uke bila kujua. Tishu zilizo na marashi, sabuni za kusafisha uke, sabuni, sabuni za unga, dawa za kuuwa mbegu za kiume, mafuta za kulainisha, mafuta za uke na sabuni za kuosha zote huwa na kemikali. Ute ulio kwenye ukuta wa uke hunyonya kemikali hizi haraka, kwahivyo ni bora upunguze kiwango cha kemikali kwa kukomesha matumizi ya vitu kama sabubi, sabubi za kusafisha uke, mafuta ya uke na pia utumie tishu zisizo na marashi.
Tazama orodha ya viambato kwenye dawa ya kuuwa mbegu za kiume na mafuta za kulainisha kama zina kemikali za glycerin, petroleum jelly, nonoxynol 9, parabens na benzocaine ambazo hujulikana kuongeza ukuaji wa bakteria na mwasho wa ngozi (contact dermatitis)
3) chupi
Hili ni jambo la kushangaza, sindio? Aina ya chupi tunazovaa huathiri afya yetu ya uke zaidi kushinda tunavyofikiri.
Ni vyema kutembea bila chupi lakini kwa wale hawawezi, hakikisha kuwa chupi sio za kubana kwani zinaweza kuzuia unyevu na ziwe eneo pa bakteria kukuwa au zisababishe nywele kutotoka nje ya ngozi (ingrown hair). Wakati unanunua chupi, tafuta inayokutosha vizuri haswa unaponunua G-string kwasababu G-string ndogo inaweza toa bakteria za mkundu izilete kwenye uke na kusababisha maambukizi kwenye njia ya mkojo.
4) Mlo
Vyakula huathiri uke na mwili kwa jumla. Uke yenye afya huwa na kiwango ya asidi ya asili (natural pH) na bakeria nyingi za afya bora; kuna vyakula hubadilisha kiwango cha asidi pH na kusababisha mabadiliko kwenye harufu ya uke.
Pia, matatizo ya uke kama vile kuvimba (thrush) yanasemekana kuwa kawaida zaidi kwa watu walio na viwango vya juu vya glukosi na pia wakati mwingine ni dalili ya matatizo mengine kama mfumo wa kinga uliodhoofika.
5) Matendo ya ngono
Mangonjwa ya zinaa (STIs) ndio adui kubwa ya uke; kumbuka kila mara kutumia njia za uzuiaji mimba zinazozuia manii kama vile kondomu za ndani na nje ili kuepuka kupata STI na usisahau kutumia kondomu mpya ukiwa unabadilisha kutoka kwa mkundu kwenda kwenye uke.
Kuwashwa kila mara, ute uliokuwa na rangi na harufu mbaya zinaweza kuwa dalili ya magonjwa ya zinaa (STIs).
6) Kulamba uke
Kulamba uke huleta raha, lakini ikipita kiasi kwa kuweka asali, krimu (kama ya keki), maziwa, juisi ya matunda, chokoleti au matunda kuifanya iwe tamu zaidi ni hatari na unaweza kupata uvimbe (thrush).
7) Kukauka na kujibana
Ebu fikiria hali mdomo wako hauna mate; hilo lina husu pia uke wako. Kuna aina nyingi ya majimaji ya ukeni na kutoka kwao ni jambo la kawaida; kuweka tamponi zako kwenye kemikali ya alkoholi ili kusitisha majimaji hizi kutoka ni jambo la hatari kwa uke.
Kubana uke pia ni tendo la hatari sana. Ukichunguza jinsi tembe na krimu za kubana uke hufanya kazi, utagundua kwamba kibana uke hukausha uke kwa muda mfupi na kuifanya ikae ndogo, hali inayoweza kusababisha machubuko na kukufanya uhisi uchungu wakati wa ngono.
Kuanzisha mabadiliko chanya
Jinsi bora zaidi ya kutunza uke wako ni kuijali kwa kukuwa mwenye huruma kwake kila mara. Inamaanisha ufanye mabadiliko kwenye mtindo wa maisha. Unaweza fanya hivyo kwa njia hizi:
1) Masomo ya kuendelea
Unyanyapaa kuhusu uke unaweza kupunguzwa tukisoma kuihusu na kufunza wengine.
2) Harakati chanya za uke
Kuna watu wanaotoa habari ya afya ya kijinsia kuhusiana na uke; hili linasaidia watu wanaoishi maeneo ambayo yana rasimali chache kuhusu afya ya uke.
Fuata blogu na kurasa za mitandao ya jamii ambayo yanatoa habari zilizothibitishwa za kimatibabu kuhusu uke.
3) Mazoea
Haitoshi kusoma kuhusu uke, kufanya kile ulichojifunza ndio hali ya juu ya kutunza uke. Ndio kwa sababu unastahili kupata habari zilizothibitishwa za kimatibabu kuhusu uke.
Cha muhimu: Uke ni sehemu ya mwili inayoweza kustahimili mengi: Kuwa mwenye huruma kwake.
Je, una jambo la kusema?Wacha ujumbe wako hapa chini, wasiliana nasi kwenye kurasa zetu za mitandao ya kijamii: Facebook, Instagram na Twitter au tutumie barua pepe kwenye info@findmymethod.org. Kwa taarifa zaidi kuhusu njia za uzuiaji mimba, tembelea findmymethod.org
Kuhusu mwandishi: Amos Sanasi ni mdemografia, na mtaalamu wa maswala yanayohusiana na ngono na pia mwanzilishi wa jina la rajamu la mambo chanya kuhusu ngono la kwanza nchini Nigeria, Revaginate NG ambalo linatoa taarifa za kina kuhusu ngono na vifaa vya ngono, haswa kwa watu walemavu. Yeye huandika kwenye akaunti ya twitter @thesanasi.