Zaidi ya kukupa furaha na kupitisha mkojo: Jinsi ya kutunza uume wako

Zaidi ya kukupa furaha na kupitisha mkojo: Jinsi ya kutunza uume wako

Ulifikiria nini baada ya kusoma kichwa? Usiseme, lakini iweke wazo hilo.
Wacha tuchukue muda mfupi kuishukuru uume. Bila uume, pengine huenda binadamu hawangekuwa duniani; ebu fikiria kuhusu hilo kwa muda mfupi. Uume pia ni chombo chenye nguvu cha kufanyia vitu vingi; bali na kuwa sehemu ya mwili inayokupa furaha na kupitisha mkojo, afya ya uume wako inaweza athiri afya yako kwa jumla.

Sasa turejelee ulichokifiria baada ya kusomwa kichwa. Ulishanga ulipokisoma? Ulitaka kujua zaidi au pengine haukujali? Mara nyingi tukiwauliza watu walio na uume jinsi hao hutunza uume wao, sisi hupata majibu ya kutamausha. Majibu ya kawaida zaidi ni kama: Sina mpangilio wa utunzaji; Wanaume hawajitunzi; Mimi hunywa pombe kusahau mambo hayo;Mimi huvuta sigara/hunywa pombe kwa mambo hayo; Mimi hutazama mechi au hucheza michezo za video kusahau mambo hayo; au wengine husema kwamba kufanya ngono vizuri husaidia.

Kufumbua swala la kujitunza

skincare for healthy life

Kujitunza ni nini haswa? Kueleza kwa ufupi, ni shughuli yoyote tunayoifanya kujiboresha na kuboresha afya yetu. Tukisema afya, tunamaanisha kuwa na ustawi wa kiakili, kimwili, kimawazo, kingono na hata kiroho; na kusudi kuu ya kujitunza ni kutufanya tuwe watu walio na afya bora.

Kujitunza ni rahisi sana; Unaweza anza sasa hivi kwa kujifunza stadi msingi. Hauhitaji mafunzo yoyote maalum kwa maana mpangilio inajumuisha shughuli rahisi za kila siku za kukusaidia.

Kwa bahati mbaya, watu wengi hawana stadi za kujitunza kwasababu hawajui ni kitu kipi kitaipa uume wao afya bora. Juu ya hayo, jamii pia huwachukulia wanaume wanaotunza miili yao vyema kama watu walio na mienendo za ajabu.

Lakini kumbuka kwamba kujitunza kunakufaidi wewe, sio jamii. Tazama orodha hii ya vitu unavyoweza kufanya ili kuleta mabadiliko kwa afya ya uume wako na pia kwa afya yako kwa jumla.

erotic bath

Mwogo wa kuamsha nyege

Hili unaweza kufanya hata bila mwenzi; oga kwa maji ya vuguvugu na iliyo na manukato ya kuleta tamaa. Kutoka kwenye kifua chenye nywele hadi kwenye wayo wa mguu, papasa papasa ili uhisi kila kitu- haswa vinundu na vipele.

Epuka kupima urefu wa uume wako

Kile unachotumia kupimia urefu wa uume wako, itupe na ukome kabisa kupima urefu. Urefu wa uume wako hauathiri kiwango cha raha ya ngono utakayo hisi; kwahivyo wacha wasiwasi juu ya urefu wa uume.

Mazoezi

Neno hilo lisikupe uoga; kutembea, kufanya yoga na kujitunza ni aina za mazoezi nyepesi.Itakuwa jambo nzuri ikiwa unaweza kujogi au kukimbia mara tatu kwa wiki.Mazoezi yanasaidia mzunguko wa damu mwilini kote lakini pia uume wako hupata manufaa kwasabu mazoezi huisaidia kusimama wima.

balls check for penile health

Tunza mapumbu

Saratani ya tezi-kibou nie saratani ya pili kawaida zaidi  kwa wanaume. Chunguza mapumbu yako mara kwa mara kuona kama kuna mabadiliko kwenye ukubwa na umbo na pia ikiwa kuna mabongebonge. Tafadhali muone daktari ikiwa kuna jambo ambalo silo la kawaida.

Chakula

Vyakula unavyokula vinaathiri afya ya uume wako; jaribu kukula vyakula vya kuboresha afya. Badala ya sukari, tumia asali kwani ina madili inayoitwa boron, ambayo husaidia kutengeneza homoni ya testosteroni. Kula mboga na matunda zaidi na haswa tikiti maji ambayo huwa kama  Viagra asilia. Punguza uvutaji sigara kwasabu  nikotini hupunguza uwezo wa uume kusimama. Pia punguza kiasi ya pombe unayokunywa kwasabu pombe inaweza kusababisha uume kusimama kwa ulegevu.  

running in the sun

Tembea jua linapochomoza

Sio kutembea kwenye jua kali; hio ni kama kujiadhibu. Tembea au ota jua asubuhi wakati jua limechomoza . Jua la asubuhi huleta vitamini D ambayo husaidia kutengeneza mbegu za kuime zenye afya. Ni hivyo!

Uerevu kwa maswala za kingono

Kabla ya kushiriki katika ngono, itathmini kwanza hali hiyo. Ikiwa ni ngono na mtu yeyote ule, kwa mfano, jiulize ikiwa una kondomu au vifaa vingine vya kujikinga wakati wa kufanya ngono ya mdomo.Ni bora ikiwa wewe na mwenzi wako mtaamua kwa pamoja aina ya njia za uzazi wa mpango inayowafaa nyote wawili, uhusiano wenu wa kingono na matarajio mengine. Hili linapunguza uwezekano wa matatizo ya kingono.

Mpangilio wa kupimwa afya

Muda utakayo chukua kumwona daktari isikukatishe tamaa; hautachukua muda mrefu sana. Enda umwone daktari ukitoka kazini, pima presha, kiwango cha sukari mwilini na pia magonjwa ya zinaa. Vipimo hivi ni vya muhimu kwa afya ya uume wako; kwa mfano, presha na kiusukari   ni vyanzo vikubwa vya matatizo ya uume kusimama kwa ulegevu na kuhisi uchungu wakati mwanamume anafika kileleni.

washing hands for cleanliness and hygiene

Uume changa

Haujafikisha miaka 70 lakini uume wako una kaa wa mzee na mapumbu yako yana rangi ya kijivu na yanawasha kila wakati? Habari ndio hii! Watu walio na uume pia hupata maambukizi ya chachu. Kuwa na mpangilio wa kubadilisha nguo za ndani na kuziosha; Haukuzirithi, kwahivyo yawache! Na pia zoea kuosha uume wako unapooga; Tumia sabuni kidogo na maji safi. Ipe uume wako jina; Itakufanya uwe na uhusiano bora nao; Itazame uume wako kwenye kio angalau mara moja kwa siku na uisifu kwa kuwa chombo muhimu cha kufanyia vitu vingi.

Afya ya kiakili

Ni sawa kulia; ni sawa kukuwa na mpangilio wa afya ya kiakili.  Wanaume wamo katika hatari kubwa zaidi ya kujitia kitanzi na pia wanaume wachache hutafuta msaada wanapokuwa na matatizo ya afya ya kiakili. Tafuta msaada kutoka kwa wataalamu unapoihitaji.

skincare for healthy life

Kutunza ngozi

Hili silo la wanawake? La ni la kila mtu. Wanaume  wamo katika hatari kubwa zaidi ya kupata saratani ya ngozi kushinda wanawake, na madaktari wa ngozi wanaamini kuwa ni kwasababu wanaume hawana mpangilio wa kutunza ngozi. Jifunze mbinu rahisi za utunzaji ngozi kama vile kuondoa seli zilizokufa kwenye ngozi (exfoliate) na kuhakikisha ngozi una unyevu. Fanya hivi mara kwa mara kutunza ngozi yako.

Je, una jambo la kusema?Wacha ujumbe wako hapa chini, wasiliana nasi kwenye kurasa zetu za mitandao ya kijamii: Facebook, Instagram na Twitter au tutumie barua pepe kwenye info@findmymethod.org. Kwa taarifa zaidi kuhusu njia za uzuiaji mimba, tembelea findmymethod.org

Kuhusu mwandishi: Amos Sanasi ni mdemografia, na mtaalamu wa maswala yanayohusiana na ngono na pia mwanzilishi wa jina la rajamu la mambo chanya kuhusu ngono  Revaginate NG ambalo linatoa taarifa za kina kuhusu ngono na vifaa vya ngono, haswa kwa watu walemavu. Yeye huandika kwenye akaunti ya twitter @thesanasi