Hatari ya kupata madhara mabaya baada ya vasektomi iko chini sana. Hata hivyo, matatizo yanaweza kutokea. Haya yanaweza kujumuisha
-Maambukizo eneo la mkato. Hii hutokea tu ukifanya vasektomi ya mkato-iko nadra sana kwa vasektomi bila mkato. Hata hivyo, ni nadra maambukizo yatokee ndani ya korodani.
-Maumivu makali ya muda mrefu (yaneweza kuendelea kwa miezi ama miaka) kwenye korodani au mapumbu. Utafiti mkubwa unaojumuisha maelfu ya wanaume ulionyesha kuwa ni asilimia 1 tu ya wale ambao wamefanya vasektomi hupata maumivu haya. Utafiti mdogo wa wanaume 200 ulionyesha kuwa asilimia 6 hupata haya maumivu. Kikundi cha wanaume ambao hawajawahi kufanya vasektomi waliokuwa kwenye utafiti kilionyesha kuwa asilimia 2 walipata maumivu sawa na haya.
Chanzo cha maumivu haya haijulikani, lakini inadhaniwa kwamba yanaweza kutokea wakati kuna shinikizo linacho sababishwa na kuvuja kwa manii kutoka kwa mirija ambayo haikuzibwa vizuri au ikiwa kuna uharibifu wa neva.
Tiba hutofautiana na inajumuisha kusongesha korodani juu,dawa za maumivu, sindano ya anaesthesia kwenye mshipa wa mapumbu ili kukufa ganzi neva inayoenda kwenye korodani, upasuaji wa kuondoa eneo lililoambukizwa au kutengua vasektomi.
-kutokwa damu chini ya ngozi (hematoma) ambayo inaweza kusababisha uvimbe au mchubuko.Hii matatizo ni nadra, lakini ikifanyoka, wasiliana na mtoa huduma za matibabu mara hiohio kwa tiba.
-mzio wa anaesthesia
-Hatari nadra mno kwamba mirija yako yanaweza kujileta pamoja-hai ambayo inaweza kuishia kwa mimba (11)
Ni nini mabaya ya kufanya vasektomi?
-Upinduliaji wa vasektomi, ingawa inawezekana, kwa kawaida ni ngumu na ghali na pia haihakikishi kurudi kwa urutubisho. Kabla ufanye vasektomi, kuwa na hakika ya asilimia 100 kwamba hautaki kupata watoto wako uliowazaa.
-Inachukua hadi miezi mitatu kufanya kazi, na ukitaka kuepuka mimba, lazima utumie njia ya ziada ya kuzuia mimba wakati wa kipindi cha kungoja.
-Haikukingi dhidi ya VVU na magonjwa ya zinaa.
Ni mambo gani yanaweza kuongeza hatari ya kupata matatizo ya vaseketomi?
-Upasuaji wa awali katika eneo hilo.
-Maambukizi. Usitumie njia hii ikiwa una maambukizi kwenye korodani, uume au tezi dume (kwa mfano, magonjwa ya zinaa).
-Uvutaji sigara.
-Matatizo ya kutokwa damu.