Vasektomi hufanywa aje?

Vasektomi hufanywa aje?
Vasektomi hufanywa aje?

Vasektomi ni utaratibu wa upasuaji ambao ni wa haraka na mara nyingi huwa bila uchungu.Unahitaji kuwekewa dawa ya anasthesia mahali pa upasuaji, na utaratibu uendele ukiwa macho na inachukua dakiaka 10-30. Kulingana na aina ya upasuaji, vasektomi inaweza kufanywa kwenye ofisi ya daktari au kituo cha afya, na unapswa kuwa na uwezo wa kurudi nyumbani siku hio hio.

Jinsi ya kujiaandaa kwa vasektomi

Kabla ya siku ya upasuaji, ni muhimu kukutana na mtoa huduma za matibabu wako.

Wakati mnakutana, utapata ushauri ambayo inapaswa kukusaidia kuamua kama vasektomi itakufaa. Utapata taarifa, ikiwemo hatari na manufaa, cha kutarajia wakati na baada ya upasuaji, na kwanini ni muhimu kutumia njia ya ziada ya uzuiaji mimba kwa miezi mitatu baada ya upasuaji.

Mchakato wa mashauri itakupa fursa ya kufanya maamuzi bora, ikiwemo kubadili mawazo saa yoyote kabla upasuaji ufanyike. Ukibadilisha mawazao, bado una haki ya kupata taarifa na huduma za njia mbadala za uzuiaji mimba. Unaweza kuamua papo hapo, ama urudi nyumbani ufikirie.

Mtoa huduma za afya pia atakupima mwili kwa ujumla (ikiwemo sehemu za siri) na achukue hata taarifa za zamani kuhusu afya yako. Hakikisha umetaja madawa yoyote unayotumia au matibabu yoyote unayopata.

Ukiamua kuendelea na upasuaji, utahitajiwa kutoa idhini yako. Katika vituo vingine vya afya,wewe na mtoa huduma za afya mtahitajiwa kutia saini kwenye fomu ya idhini.

Mara umepeana idhini, unaweza amua tarehe ya upasuaji. Utashauriwa jinsi ya kujiandaa kwa upasuaji ifuatavyo:

-Vaa nguo zenye starehe.
-Tumia dawa yoyote unayopewa na mtoa huduma za matibabu.
-Dumisha usafi.Oga kabla uende kufanyiwa upasuaji na unyoe nywele kwenye sehemu ya siri ambazo zinaweza kuzuia kufikiwa kwa korodani.
-Panga mbinu ya usafiri kuenda na kutoka kwenye kituo cha afya.

Hatua ya kufuata ni kuenda kwa mtoa huduma za matibabu kwa utaratibu wa vasektomi.

Mbinu za vasektomi

Kuna aina mbili za mbinu za vasektomi-bila mkato na yenye mkato (7)

Vasektomi bila mkato (No-Scapel)

Pia inajulikana kama mbinu ya “kufikia vas”, vasektomi inayofanywa bila mkato inahusisha kuweka tundu ili kufikia mirija (vasa deferentia) ambayo hubeba manii hadi kwa uume. Mirija kisha hufungwa na kukatwa au huzibwa.

Utaratibu utachukua dakika 20, ikienda sana.

Unakuwa upasuaji wa vasektomy ambao unatumiwa sana duniani, tofauti na mbinu ya mkato , ni chale moja inawekwa kwenye korodani, dawa maalum ya anaesthesia inayotumika inahitaji tu kudungwa sindano mara moja badala ya mara mbili.

Haihitaji kushonwa ili kufunga ngozi.Mbinu bila mkato inachukua muda mfupi zaidi, michibuko na maumivu kidogo, na kuna maambukizi na hematomas (mkusanyiko wa damu unaosababisha kufura) kidogo katika eneo la chale. Kwa ujumla, utaratibu huu unajulikana kwa kupona haraka na bila matatizo.

Vasektomi ya mkato

Vasektomi ya mkato ni utaratibu wa haraka unaohitaji kutembelea mtoa huduma za matibabu, lakini bila kulazwa zahanatini au hospitalini. Inachukua dakika 20-30 na dawa ya anaesthesia inatumiwa kufanya korodani ikufe ganzi. Mtoa huduma za matibabu ataweka chale mbili kwenye korodani na azikate na atoe kipande kidogo cha kila mrija.

Pande zilizokatwa zilizobaki za vas kisha hufungwa au kuchomwa (kuzibwa na moto au stima) ili kuzuia manii kuingia kwenye majimaji ya shahawa. Kwasababu manii haiwezi kutoka, mwenza wa kike hatashika mimba.

Haijalishi mbinu gani imetumika , vasektomi itaziba manii isiingie kwenye shahawa, lakini manii inaweza kubaki kwenye mirija kwa miezi. Unapaswa kutumia njia ingine ya kuzuia mimba (kama kondomu) kwa miezi mitatu hadi manii iishe (8).

Je vasektomi huwa na uchungu?

Kwa ujumla vasektomi huwa haina maumivu. Kwa mujibu wa Advanced Urology Vasectomy Clinic , unaweza kuhisi mchuno wakati wa kuweka dawa ya kukufa ganzi (kabla ianze kufanya kazi). Wanaume wengine wameripoti kuhisi hisia ya kuvuta wakati vasa deferentia zina vutua nje.Lakini hii hufanyika kwa sekunde chache tu.

Ni nini napaswa kutarajia baada ya vasektomi?

Unaweza kupata maumivu, michubuko na uvimbe kiasi baada ya upasuaji. Hii inaweza kutulizwa kwa dawa ya maumivu na itaisha ndani ya siku mbiili. Uvimbe unaweza kutulizwa kwa kuweka barafu sehemu lillilo athirika. Pia unaweza kuvaa suruali za kubana ili kushikilia korodani mahali pake.
Jipange kwa siku moja au mbili ya kupona.

Eneo lililo wekwa tundu kwa kawaida litapona lenyewe. Hata hivyo, unaweza kutumia bandeji ambayo itahitaji kubadilishwa. Damu yoyote ikitoka inapaswa kuisha ndani ya saa 24.

Mtu ambaye amefanyiwa vasektomi anaweza kurudi kwa shughuli zake za kawaida ndani ya siku mbili. Hata hivyo, kwa karibu wiki moja , epuka kufanya kazi ngumu, kufanya ngono, na kufanya chochote kinachoweza kufanya umwage manii. Kumwaga manii punde baada ya upasuaji kunaweza kufanya mkato ujifungue na kuongeza hatari ya maambukizi na matatizo mengine ya baada ya utaratibu wa vasektomi.

Je, baada ya vasektomi, ninaweza kuanza kufanya ngono baada ya muda gani?

Hii itatofautiana kwa mtu mmoja hadi mwingine. Ingawa haupaswi kufanya ngono kwa saa 48 baada ya vasektomi, unaweza kufanya ngono yenye kinga ndani ya wiki moja baada ya upasuaji. Unaweza kufanya ngono bila kinga miezi mitatu baada ya vasektomi au baada ya kipimo cha manii kuonyesha kwamba hakuna manii kwenye majimaji ya shahawa.

Ukianza kufanya ngono tena, wewe na mwenza wako wa kike lazima muendelee kutumia njia mbadala ya uzuiaji mimba hadi mtoa huduma za matibabu wako akushauri uwache.

Upinduaji wa Vasektomi

Hii ni utaratibu unaofanywa kutengua vasektomi. Upinduaji unafanywa kwa sababu mbalimbali, ikiwemo kubadili mawazo, kupoteza mtoto, kuolewa tena, au kutibu maumivu sugu kwenye mapumbu baada ya vasektomi.

Upinduaji wa vasektomi hufanywa kwa kuleta pamoja mirija ya kubeba manii kutoka kwenye mapumbu hadi majimaji ya shahawa. Mara upinduaji umefanywa, manii tena itakuwa kwenye shahawa, na unaweza kumpachika mtu mimba. Ingawa upinduaji kwa ujumla hauleti matatizo yoyote mabaya, kuna hatari chache zikiwemo

-maambukizi kwenye eneo la upasuaji. Sawa na upasuaji wowote, unaweza kupata maambukizo ya baada ya upasuaji, lakini hii inatibiwa kwa urahisi kwa antibayotiki.
-maumivu sugu. Maumivu ya kila mara ni hatari nadra ya baada ya upasuaji.
-kutokwa damu ndani ya korodani. Hii inaweza kusababisha hematona (mkusanyiko wa damu ambayo inasababisha uvimbe). Epuka hii kwa kufuata maagizo ya baada ya upasuaji utakayopewa na mtoa huduma za matibabu, ikiwemo mapumziko ya kutosha, kutumia kifaa cha kuegezea korodani na kuweka barafu baada ya upasuaji. Ni muhimu pia kujua kama utahitaji kuepuka dawa zozote za kuzuia kuganda kwa damu kabla na baada ya upasuaji.

Mafanikio ya Upinduaji wa vasektomi

Upinduaji wa vasektomi haukuhakikishii mimba. Uwezekano wa mimba baada ya upinduaji wa vasektomi unategemea mambo mbalimabli, ikiwemo muda ambao umepita tangu ufanye vasektomi (kadiri muda unavyopita, ndivyo mafanikio yanavyopungua); kama ulikuwa na matatizo ya uzazi kabla ya vasektomi; umri wa mwenza wako; na mafunzo na uzoefu wa daktari wako wa upasuaji kwa kufanya upinduaji. Ikitegemea mambo haya, uwezekano wa mimba baada ya upinduaji unaweza kuanzia asilimia 30 hadi 90 (9).

Maswali elekezi kwa mbinu za kuzuia mimba

Je, unahitaji usaidizi zaidi kuchagua njia yako bora? Jibu maswali yetu elekezi kwa mbinu za kuzuia mimba.

Jibu maswali machache rahisi, na kulingana na majibu, tutapendekeza chaguo za uzuiaji mimba ambazo zinaweza kukufaa.

Jibu maswali
External Condom

Compare with similar Contraceptive Methods

Are you wondering if condoms are better than daily pills? Or if you should opt for a birth control implant? We're here to assist you in making this decision. You can select up to 5 contraceptive methods and compare them side by side to weigh the pros and cons of each.

Give a try to our Contraceptive Tool

In the example below, you'll find similar methods to the one you're currently reading about. Feel free to click on any that catch your interest or revisit our Contraceptive Methods page

Our Monthly Top Articles

Mnong’onezaji wa mambo ya uke: Jinsi ya kupenda uke wako hivyo ilivyo

Mnong’onezaji wa mambo ya uke: Jinsi ya kupenda uke wako hivyo ilivyo

Kabla tuzungumzie mambo ya kuthamini uke, tucheze mchezo ambapo una alama 50 kutoka mwanzo. Nina orodha ya maswali 5 na ikiwa umawahi fanya kile kilichoulizwa kwenye swali, unapoteza alama 10. Twen...

Njia 6 tunaweza kuchukua udhibiti wa uzazi wa mpango kama wanaume

Njia 6 tunaweza kuchukua udhibiti wa uzazi wa mpango kama wanaume

Ingawa ngono salama ni jukumu la wanaume na wanawake, mambo ya uzazi wa mpango imechukuliwa tangu kitambo  kama jukumu la mwanamke. Ingekuwa wanaume wangechukua jukumu la kutumia njia za kuzuia mim...

Mnong’onezaji wa mambo ya uke: Jinsi ya kupenda uke wako hivyo ilivyo

Mnong’onezaji wa mambo ya uke: Jinsi ya kupenda uke wako hivyo ilivyo

Kabla tuzungumzie mambo ya kuthamini uke, tucheze mchezo ambapo una alama 50 kutoka mwanzo. Nina orodha ya maswali 5 na ikiwa umawahi fanya kile kilichoulizwa kwenye swali, unapoteza alama 10. Twen...

Njia 6 tunaweza kuchukua udhibiti wa uzazi wa mpango kama wanaume

Njia 6 tunaweza kuchukua udhibiti wa uzazi wa mpango kama wanaume

Ingawa ngono salama ni jukumu la wanaume na wanawake, mambo ya uzazi wa mpango imechukuliwa tangu kitambo  kama jukumu la mwanamke. Ingekuwa wanaume wangechukua jukumu la kutumia njia za kuzuia mim...

Mnong’onezaji wa mambo ya uke: Mambo yanayohatarisha uke na njia za kuitunza

Mnong’onezaji wa mambo ya uke: Mambo yanayohatarisha uke na njia za kuitunza

Uke ni sehemu moja ya mwili isiyoeleweka vizuri. Ingekuwa uke wako ungeweza kuongea,  ungekuambia nini? Nadhani unge changanyikiwa cha kusema. Mara tunaona makala inayosema safisha uke wako na tena...