Vasektomi

Vasektomi
Vasektomi

Vasektomi ni nini?

Vasektomi, pia inayojulikana kama “kufunga uzazi wa mwanamume” ama “uzuiaji mimba kupitia upasuaji kwa mwanamume” ni njia ya kudumu ya uzuiaji mimba ambayo inaziba mirija ya kubeba manii. Hii hufanya iwe ngumu kumpachika mtu mimba. Inawafaa wanaume ambao hawana nia ya kupata watoto wowote au watoto wenginge ikiwa tayari wana watoto.Haidhuru utendaji wa ngono wa mwanamume kwa njia yoyote.

Vasektomi hufanywa kupitia utaratibu wa upasuaji ulio rahisi na salama inayolenga kuzuia mimba daima na kwa ufanisi wa juu (1).

Mara vasektomi imekamilika, urutubisho haitarajiwi kurudi kwasabu utaratibu huu unapaswa kuwa wa kudumu. Hata hivyo, ukitaka kupata tena urutubusho baada ya vasektomi, unaweza kufanya hivyo kwa upasuaji wa kufungua mirija tena ama utaratibu wa kurudisha manii ambayo inafanywa kama sehemu ya in vitro fertilization. Chaguo hizi mbili kwa kawaida huwa ghali, ngumu na hazipatiki maeneo mengine. Kama utafaulu kufanya upasuaji wa kufungua mirija ama utaratibu wa kurudisha manii, hakuna hakikisho kwamba utaweza kumpachika mtu mimba (2).

Ni kwa hali gani vasektomi itakuwa chaguo bora?

Ni muhimu kuzungumza na mwenza wako kubaini kama vasektomi itakuwa chaguo sahihi kwako. vasektomi itakuwa chaguo bora kama

-familia yako ni kubwa ya kutosha-tayari una watoto wa kutosha ama hautaki watoto kamwe.
-Wewe na/ama mwenza wako mna tatizo la kijenetiki ambalo linaweza kupitishwa kwa mtoto wako wa kuzaa.
-Mimba itasababisha matatizo ya kiafya makubwa. Kama kuna sababu ya kiafya inayohitaji wewe au mwenza wako kutoshika mimba kamwe, vasektomi huenda ikawa chaguo bora.

Hali ambazo vasektomi inafanywa hutofautiana katika nchi tofauti, kuna nchi huikubali kwa sababu kadhaa na nchi zingine huweka vikwazo. Kuna nchi ambazo hazina sheria maalum na huwacha maamuzi ya kufanya vasektomi kwa mtoa huduma za matibabu. Kama unazingatia kufanya vasektomi, ni muhimu kufanya utafiti wa sheria gani katika nchi yako inaikubali. (3).

Ni nani anaweza kufanya vasektomi?

Baada ya kupata ushauri, mwanamume yeyote anaweza kufanya vasektomi. Hii inajumuisha

-wanaume waliyoowa au wale hawajaowa;
-wanaume walio na watoto au wale hawana;
-wanaume vijana na wanaume wazee (mwanamume yeyote mwenye umri zaidi ya miaka 25 anaweza kufanya vasektomi, bora uwe tayari unashiriki ngono na una afya bora ya kiakili na kimwili, hakuna miaka ya juu zaidi; Kujua kama uko tayari kwa upasuaji ni maamuzi inawachiwa mtoa huduma za afya wako);
-kuwepo au kusiwe na ruhusa ya mwenza;
-wanaume wanao ugua ugonjwa wa seli mundu;
-wanaume walio katika hatari ya juu ya magonjwa ya zinaa (STIs), ikiwemo VVU; na
-wanaume wanaoishi na VVU, iwe wanatumia dawa za kupunguza makali au la.

Cha muhimu ni kwamba vasektomi inapaswa kufanywa tu kwa mtu ambaye ana hakika hatajuta kufanya upasuaji (4).

Vasektomi hufanya aje kazi?

Mkato mdogo au tundu huwekwa kwenye korodani ili kumpa nafasi mtoa huduma za afya kufikia mirija miwili (vasa deferentia) ambayo hubeba manii hadi kwa uume. Mirija kisha hukatwa na kufungwa au kuzibwa kupitia kuchomwa (cauterization) ( kuweka umeme au moto).

Vasektomi huzuia mimba kwa kuweka manii nje ya shahawa. Mara umefanyiwa vasektomi, shahawa humwagwa, lakini haiwezi kusababisha mimba (5).

Vasektomi ina ufanisi kiasi gani?

Vasekti ni mojawapo wa njia za uzuiaji mimba zenye ufanisi wa juu. Ndani ya mwaka wa kwanza wa matumizi, njia hii ni salama kwa asilimia 99 kwa kuzuia mimba. Hata hivyo, ufanisi huu hauji mara hio hio baada ya upasuaji. Lazima utumie njia ingine ya uzuiaji mimba kwa angalau miezi mitatu baada ya vasektomi au hadi uwe na hakika kwamba hakuna manii kwenye shahawa. Chanzo kuu cha mimba ndani ya mwaka wa kwanza baada ya vasektomi ni kutotumia njia ya uzuiaji mimba mfululizo ndani ya hio miezi mitatu ya kungoja.

Sawa na utaratibu wa kufunga mirija ya kizazi ya wanawake, hatari ndogo ya kushika mimba hubaki baada ya mwaka wa kwanza wa matumizi , hadi mwenza wa mume atakapofika kukoma kwa hedhi.

Ndani ya miaka mitatu ya matumizi, ufanisi huwa asilimia 98. Hii huwa kwasababu ya mambo kama kutotumia njia ya uzuiaji mimba wakati wa kungoja; sehemu iliyokatwa ya vas deference inamea tena; au kama mtoa huduma za matibabu alifanya makosa wakati wa upasuaji (6).

Vasektomi huanza kuwa na ufanisi lini?

Kwa mujibu wa Taasisi ya Kitaifa ya Afya ya Marekani, inachukua mwanamume kumwaga manii mara 15-20, au miezi mitatu, ili manii iishe kwenye shahawa. Kuongezea, mwanamume mmoja kati ya watano kwa kawaida atangoja muda mrufu zaidi ya hio.

Kwa hivyo, ni lazina uendelee kutumia njia ingine ya kuzuia mimba hadi manii iishe. Kama wenzi watakosa kutumia njia ya kuzuia mimba yenye ufanisi ndani ya miezi mitatu baada ya vasektomi, kuna hatari mkubwa wa mimba kutungwa kabla vasektomi ipate ufanisi.

Kwa hivyo, ni lazina uendelee kutumia njia ingine ya kuzuia mimba hadi manii iishe. Kama wenzi watakosa kutumia njia ya kuzuia mimba yenye ufanisi ndani ya miezi mitatu baada ya vasektomi, kuna hatari mkubwa wa mimba kutungwa kabla vasektomi ipate ufanisi.

Njia moja hakika ya kudhibitisha kama vasektomi imepata ufanisi ni kwa kupimwa shahawa kama ina manii, miezi mitatu baada ya utaratibu.Sampuli kidogo ya shahawa yako itachukuliwa na ipimwe kama ina manii.Kama manii haitapakina, vasektomi yako itakuwa na ufanisi wa asilimia 99 wa kuzuia mimba. Inapendekezwa upimwe shahawa angalau mara mbili.

Kupimwa shahawa mara ya kwanza kunaweza kufanyika miezi miwili baada ya upasuaji, na ya pili ifanywe mwezi wa tatu. Ikiwa shahawa yako itapatika kuwa na manii wakati imepimwa baada ya miezi mitatu, , tembelea mtoa huduma za matibabu wako wiki mbili au nne baadaye kwa kipimo kingine. Pia unashauriwa kupimwa kila mwaka ama mara kwa mara kuhakikisha kwamba vasektomi inafanya kazi inavyopaswa.

Katika nchi zingine, unaweza kufanya kipimo cha kuangalia rutubisho wewe mwenyewe kutumia kifaa cha kupima manii nyumbani. Kama unapendelea chaguo hii, unapaswa kumuuliza mtoa huduma za matibabu wako kama vifaa hivyo vya kupima vinapatikana katika nchi yako.

Maswali elekezi kwa mbinu za kuzuia mimba

Je, unahitaji usaidizi zaidi kuchagua njia yako bora? Jibu maswali yetu elekezi kwa mbinu za kuzuia mimba.

Jibu maswali machache rahisi, na kulingana na majibu, tutapendekeza chaguo za uzuiaji mimba ambazo zinaweza kukufaa.

Jibu maswali
External Condom

Compare with similar Contraceptive Methods

Are you wondering if condoms are better than daily pills? Or if you should opt for a birth control implant? We're here to assist you in making this decision. You can select up to 5 contraceptive methods and compare them side by side to weigh the pros and cons of each.

Give a try to our Contraceptive Tool

In the example below, you'll find similar methods to the one you're currently reading about. Feel free to click on any that catch your interest or revisit our Contraceptive Methods page

Our Monthly Top Articles

Mnong’onezaji wa mambo ya uke: Jinsi ya kupenda uke wako hivyo ilivyo

Mnong’onezaji wa mambo ya uke: Jinsi ya kupenda uke wako hivyo ilivyo

Kabla tuzungumzie mambo ya kuthamini uke, tucheze mchezo ambapo una alama 50 kutoka mwanzo. Nina orodha ya maswali 5 na ikiwa umawahi fanya kile kilichoulizwa kwenye swali, unapoteza alama 10. Twen...

Njia 6 tunaweza kuchukua udhibiti wa uzazi wa mpango kama wanaume

Njia 6 tunaweza kuchukua udhibiti wa uzazi wa mpango kama wanaume

Ingawa ngono salama ni jukumu la wanaume na wanawake, mambo ya uzazi wa mpango imechukuliwa tangu kitambo  kama jukumu la mwanamke. Ingekuwa wanaume wangechukua jukumu la kutumia njia za kuzuia mim...

Mnong’onezaji wa mambo ya uke: Jinsi ya kupenda uke wako hivyo ilivyo

Mnong’onezaji wa mambo ya uke: Jinsi ya kupenda uke wako hivyo ilivyo

Kabla tuzungumzie mambo ya kuthamini uke, tucheze mchezo ambapo una alama 50 kutoka mwanzo. Nina orodha ya maswali 5 na ikiwa umawahi fanya kile kilichoulizwa kwenye swali, unapoteza alama 10. Twen...

Njia 6 tunaweza kuchukua udhibiti wa uzazi wa mpango kama wanaume

Njia 6 tunaweza kuchukua udhibiti wa uzazi wa mpango kama wanaume

Ingawa ngono salama ni jukumu la wanaume na wanawake, mambo ya uzazi wa mpango imechukuliwa tangu kitambo  kama jukumu la mwanamke. Ingekuwa wanaume wangechukua jukumu la kutumia njia za kuzuia mim...

Mnong’onezaji wa mambo ya uke: Mambo yanayohatarisha uke na njia za kuitunza

Mnong’onezaji wa mambo ya uke: Mambo yanayohatarisha uke na njia za kuitunza

Uke ni sehemu moja ya mwili isiyoeleweka vizuri. Ingekuwa uke wako ungeweza kuongea,  ungekuambia nini? Nadhani unge changanyikiwa cha kusema. Mara tunaona makala inayosema safisha uke wako na tena...