Kondomu ya ndani haina madhara makubwa. Hata hivyo, inaweza kusababisha wewe au mwenzi wako kuwashwa kidogo.
Ubaya wa kondomu ya ndani
– Inahitaji matumizi sahihi. Ingawa ina ufanisi wa hadi asilimia 95 ikitumiwa sahihi, watu wengi hawatumii kondomu za ndani kamilifu (kila wakati wanafanya ngono). Hili likifanyika, ni watu 79 tu kati ya 100 wanaotumia njia hii wataweza kuepuka mimba.
– Inaweza kuteleza, kupasuka au sehemu ya nje irudi ndani (ijipindue). Ikiwa chochote kati ya hivyi kitatokea,zingatia kutumia njia ya uzuiaji mimba ya dharura haraka iwezekanavyo ili kukinga mimba. Ikiwa unashuku kuwa afya yako ya kingono ipo kwenye hatari, pima magonjwa ya zinaa na/au tumia dawa za Kinga baada ya kuwemo hatarini (PEP) ukifuata miongozo ya ngono salama.
– Zinaweza kuwa ngumu zaidi kupata na ghali zaidi kushinda kondomu za nje.
– Kondomu za ndani zinahitaji jitihada na kujitolea kwa kiwango cha juu. Ili ziwe na ufanisi, ni lazima uhakikishe umezitumia sahihi, kila wakati. Pia unahitaji kufanya mazoezi kwa muda ndio ujue kuzitumia,
– Watu wengine watakuwa na mzio wa aina fulani ya mafuta ya kulainisha (Ikiwa hivyo, jaribu chapa tofauti ya kondomu au njia tofauti ya uzuiaji mimba)
– Zinaweza kupunguza hisia za ngono wakati unafanya ngono.
Kondomu zingine za ndani (kike) zinaweza kuwa na kelele fulani ya kuudhi wakati wa ngono (lakini aina mpya zilizotengenezwa kwa nitrile hazina (5).
-Ni ngumu kukumbuka kuzitumia ikiwa umekunya pombe.