Manufaa ya kiafya
-Ufanisi. Kondomu ya ndani ina ufanisi zaidi ikitumiwa pamoja na dawa ya kuua manii. Ikutumiwa sahihi, watu 95 kati ya kila 100 wanaoitumia wataweza kukinga mimba.
-Kinga dhidi ya magonjwa ya zinaa. Kondomu za ndani zinasaidia kukukinga dhidi ya magonjwa mengi ya zinaa, ikiwemo VVU.
-Kufaa watu walio na mzio. Zinafaa watu walio na mzio wa latex. Tofauti na kondomu za nje, kondomu za ndani zimeundwa kwa plastiki au mpira bandia.Unaweza kuzitumia hata ikiwa una mzio wa latex.
Manufaa kwa mtindo wa maisha
-Kuvaa kondomu ya ndani inaweza kuwa sehemu ya kuongeza tamaa ya kingono kabla ya kuingiza uume kwenye uke. Ikiwa unaweza kuzungumza na mwezi wako kuhusu ngono, zungumza kuhusu jinsi mnavyoweza kutumia kondomu kuongeza ridhaa kwa maisha yenyu ya ngono.
-Pete ya nje inaweza kuchechemua kinembe chako na kufanya ngono ilete furaha zaidi kwa mwanamke.
-Inawapa wanawake na watumiaji udhibiti zaidi juu ya ngono iliyo na kinga. Ikiwa mwenzi wako hatavaa kondomu ya nje, lakini bado unataka kinga dhidi ya magonjwa ya zinaa, kondomu ya ndani ni chaguo bora.
-Kondomu ya ndani ni laini, ina unyevu na inahisi asili zaidi wakati wa ngono kuliko kondomu za nje.
-Agizo la daktari halihitajiki, na hauhitaji mashauriano ya daktari ili ununue kondomu ya ndani.
-Inaweza kutumiwa pamoja na mafuta ya kulainisha yenye oili au yenye maji
-Inabaki mahali pake hata ikiwa uume wa mwanamume itawacha kusimama.
-Zinaweza kukaa hadi miaka mitano kabla ya kufika tarehe ya mwisho ya matumizi.
-Hazihitaji hali yoyote maalum ya kuhifadhiwa. Hii ni kwasababu zimeundwa kwa polyurethane,nyenzo ambayo haiharibiki kwenye hali ya unyevu (4).