Jinsi ya kutumia kondomu ya ndani

Jinsi ya kutumia kondomu ya ndani
Jinsi ya kutumia kondomu ya ndani

Kondomu inaweza kuingizwa mapema, hadi saa nane kabla ya kufanya ngono. Hii inakupa udhibiti juu ya usalama wako wa kingono na kukuruhusu kufurahia ngono bila kuwa na wasiwasi wa kushika mimba.

Hatua ya kwanza ni kuangalia tarehe ya mwisho ya matumizi kwenye pakiti ya kondomu na ikiwa imeraruka au ina matundu.Kondomu ambayo imefika tarehe ya mwisho ya matumizi inaongeza hatari ya mimba na magonjwa ya zinaa.

Jinsi ya kuvaa kondomu

-Nawa mikono kwa sabuni na maji. Wacha yakauke yenyewe kwa upepo bila kuguza chochote.
-kwa umakini, toa kondomu kwenye pakiti.
Weka mafuta ya kulainisha na dawa ya kuua manii (ikiwa unapendelea) nje ya sehemu iliyo fungwa ya kondomu. Mafuta ya kulainisha itasaidia kondomu isiraruke na dawa ya kuua manii inasaidia kuongeza ufanisi wa njia hii (hasa kwa hali kondomu itararuka au kutoka).
-Kama umesimama au umeketi, panua miguu yako.Finya kabisa pamoja pande za pete kwenye sehemu iliyofungwa ya kondomu na uingize kama tamponi.
-Sukuma pete ndani ya uke hadi mwisho inapoweza kufika. Isukume hadi ifike kwenye shingo ya kizazi. Kondomu itajipanua yenyewe, na kuna uwezekano mkubwa hautaihisi.
-Hakikisha kondomu haiko kombo. Wacha pete ya nje ining’inie karibu inchi moja nje ya uke wako (itaonekana la ajabu kidogo).
-Elekeza uume uliosimama wa mwenzi wako ndani ya pande ya kondomu iliyo wazi. Ukihisi uume umeteleza kati ya kondomu na kuta za uke au ikiwa pete ya nje imesukumwa ndani ya uke, sitisha ngono na urudishe kondomu vizuri au uweke ingine.
-Usiwe na wasiwasi kama kondomu itasonga upande mmoja hadi mwingine wakati unafanya ngono. Ikiwa uume utatoka nje ya kondomu uingie kwenye uke au mkundu, toa kondomu kwa upole kisha uiingize tena. Endapo mwenzi wako atamwaga manii kwa ajali ndani ya uke wako, zingatia kutumia njia za dharura za uzuiaji mimba ili kuepuka hatari ya mimba.
-Ikiwa unatumia kondomu ya ndani wakati wa ngono wa mkundu, fuata utaratibu sawa.
-USITUMIE kondomu ya ndani pamoja na kondomu ya nje. Kutumia aina hizi mbili za kondomu pamoja hakutaongeza kinga maradufu, kunafanya tu zote mbili ziwe na uwezo mkubwa wa kupasuka.
Kumbuka, ikiwa hii ndio njia unapendelea, ni lazima utumie kondomu KILA MARA (2).

Jinsi ya kutoa kondomu ya ndani

-Finya pete ya nje na uipindue uifunge kuzuia manii kumwagika nje.
-Vuta kondomu nje polepole.
-Itupe kondomu mahali watoto hawafiki. Usiitupe kwenye choo cha maji. Itaziba mifereji.

Maswali elekezi kwa mbinu za kuzuia mimba

Je, unahitaji usaidizi zaidi kuchagua njia yako bora? Jibu maswali yetu elekezi kwa mbinu za kuzuia mimba.

Jibu maswali machache rahisi, na kulingana na majibu, tutapendekeza chaguo za uzuiaji mimba ambazo zinaweza kukufaa.

Jibu maswali
External Condom

Compare with similar Contraceptive Methods

Are you wondering if condoms are better than daily pills? Or if you should opt for a birth control implant? We're here to assist you in making this decision. You can select up to 5 contraceptive methods and compare them side by side to weigh the pros and cons of each.

Give a try to our Contraceptive Tool

In the example below, you'll find similar methods to the one you're currently reading about. Feel free to click on any that catch your interest or revisit our Contraceptive Methods page

Our Monthly Top Articles

Mnong’onezaji wa mambo ya uke: Jinsi ya kupenda uke wako hivyo ilivyo

Mnong’onezaji wa mambo ya uke: Jinsi ya kupenda uke wako hivyo ilivyo

Kabla tuzungumzie mambo ya kuthamini uke, tucheze mchezo ambapo una alama 50 kutoka mwanzo. Nina orodha ya maswali 5 na ikiwa umawahi fanya kile kilichoulizwa kwenye swali, unapoteza alama 10. Twen...

Njia 6 tunaweza kuchukua udhibiti wa uzazi wa mpango kama wanaume

Njia 6 tunaweza kuchukua udhibiti wa uzazi wa mpango kama wanaume

Ingawa ngono salama ni jukumu la wanaume na wanawake, mambo ya uzazi wa mpango imechukuliwa tangu kitambo  kama jukumu la mwanamke. Ingekuwa wanaume wangechukua jukumu la kutumia njia za kuzuia mim...

Mnong’onezaji wa mambo ya uke: Mambo yanayohatarisha uke na njia za kuitunza

Mnong’onezaji wa mambo ya uke: Mambo yanayohatarisha uke na njia za kuitunza

Uke ni sehemu moja ya mwili isiyoeleweka vizuri. Ingekuwa uke wako ungeweza kuongea,  ungekuambia nini? Nadhani unge changanyikiwa cha kusema. Mara tunaona makala inayosema safisha uke wako na tena...