Na ikiwa nimefanya ngono siku isiyofaa?

Ikiwa imepita siku 5 au chache tangu ufanye ngono,na hautaki mimba, tumia njia za dharura za uzuiaji mimba. Ikiwa ni zaidi ya siku 5 zilizopita, enda upimwe mimba ikiwa hedhi yako ya kufuatia itachelewa.

Ukitaka kufanya ngono bila kinga siku ambazo kuna uwezekano wa kushika mimba, na hutaki kushika mimba, pengine uzingatie njia ingine rahisi.

Bado haiendi sawa? Ikiwa unapata shida kubaini siku ambazo unaweza kushika mimba, pengine uzingatie njia kama IUD ama vipandikizi.

Unapenda kwamba hakuna homini kwa njia ya uelewa wa kizazi? Jaribu IUD bila homini au njia za kuzuia manii kama kondomu.

Jaribu njia tofauti: kondomu za ndani (kike), vipandikizi, IUD and kondomu za nje (kiume)


References:

  1. World Health Organization Department of Reproductive Health and Research and Johns Hopkins Bloomberg School of Public Health Center for Communication Programs (2018) Family Planning: A Global Handbook for Providers. Baltimore and Geneva. Retrieved from https://apps.who.int/iris/bitstream/handle/10665/260156/9780999203705-eng.pdf?sequence=1