Na ikiwa siwezi kukumbuka kupima joto la mwili, kuweka rekodi za hedhi au kuchunguza ute wa ukeni kila siku?

Njia hii itafanya kazi ikiwa tu umejitolea kuitumia sahihi na kwa msimamo. Kuna nyenzo nyingi kama vile apu, vipimajoto, na shanga za mzunguko wa hedhi za kukusaidia kuchunguza na kuweka rekodi za hedhi yako.
Bado haiendi sawa? ikiwa hauna hakika kwamba unaweza kuchunguza dalili zako za rutuba kila siku, zingatia njia ingine inayohitaji jitihada kidogo.
IUD au Vipandikizi ni nzuri kwa kinga ya miaka, sindano kwa kinga ya miezi, pete inabadilishwa tu kila mwezi, na unabadilisha kiraka mara moja kwa wiki.
Jaribu njia tofauti: Vipandikizi, IUD, kiraka, pete and sindano.