Kwanini napata maambukizi ya njia ya mkojo kila mara?

Wanawake wengine wanapata maambukizi ya njia ya mkojo wakitumia diaframu. Kukojoa kabla ya kuingiza diaframu kunaweza kusaidia. Kojoa tena baada ya kufanya ngono.
Pia unaweza kuenda kwa mtoaji huduma za afya kuhakikisha kwamba diaframu inaingia sahihi.
Bado haiendi sawa? Ikiwa bado unapata maambukizi ya njia ya mkojo na unataka kubadilisha njia, zingatia njia ambayo hauhitaji kuingiza kila wakati unafanya ngono.
Jaribu njia tofauti: Vipandikizi, kitanzi, kiraka, kidonge, sindano.


References:

  1. Society of Obstetricians and Gynaecologists of Canada. (2015). Canadian Contraception Consensus Chapter 5: Barrier Methods. JOGC Journal of Obstetrics and Gynaecology Canada , 37. Retrieved from https://www.jogc.com/article/S1701-2163(16)39376-8/pdf