Ili mbinu hii ifanye kazi, mwanamume lazima afahamu ni lini atamwaga manii. Kuchomoa uume kunahitaji uelewa wa juu na uwezo wa kutabiri wakati wa kumwaga manii, na kuvuta uume nje kabla ifanyike.
Kumbuka kuwa majiji kabla ya kumwaga manii (majimaji inayozalishwa wakati uume umesimama) inaweza kubeba manii. Kwa hivyo hata akichomoa uume kabla ya kumwaga, mwanamke bado yuko katika hatari ya kupata mimba.
Ingawa mbinu hii inaweza kutumiwa kama njia ya msingi au ya pili, kuifanya iwe na ufanisi, unashauriwa kutumia dawa ya kuua manii pia.
Mbinu ya kuchomoa uume ina ufanisi kiasi gani?
Mbinu ya kuchomoa uume ni mojawapo wa njia za uzuiaji mimba zenye ufanisi wa chini sana.
Ufanisi wake unategemea kwa kiwango kikubwa uwezo wa mwanamume kukumbuka kuvuta nje uume wake kutoka kwa uke wa mwanamke kabla amwage manii, kila mara wanafanya ngono bila kinga.
Inavyotumiwa kwa kawaida, ni asilimia 80 tu ya watumiaji wataweza kuzuia mimba ndani ya mwaka wa kwanza wa matumizi. Hii inamaanisha kuwa wanawake 20 kati ya 100 wanaotumia njia hii wamo katika hatari ya kushika mimba.
Ikitumiwa sahihi wakati wa kila tendo la ngono, asilimia 94 ya wanawake wataweza kuzuia mimba zaidi ya mwaka mmoja wa matumizi. Hii inamaanisha kuwa wanawake 6 kati ya 100 wanaotumia njia hii sahihi wamo katika hatari ya kushika mimba (kumbuka kuwa bado unaweza kushika mimba kutoka kwa majimaji kabla ya manii)
Kuna uwezo gani wa kushika mimba kama atachomoa uume kisha airudishe ndani?
Kiwango chochote cha manii ambacho kimewachwa baada ya mwanamume kumwaga manii kinaweza kusababisha mimba. Kuhakikisha kwamba uume hauna mabaki yoyote ya manii, mwanamume anapaswa kukojoa na kuosha ncha ya uume kabla ya kushiriki ngono ya uume ndani ya uke tena.