-Ni njia ya asili-hauhitaji dawa au kifaa.
-Haina homoni.
-Hakuna kuchelewa kurudi kwa urutubisho- Unaweza kushika mimba mara baada ya kuwacha kutumia njia hii.
-Ni njia nafuu zaidi. kwa ujumla, ni bora kushinda hali ya kutokuwepo na njia ya uzuiaji mimba yoyote, na unaipata bila malipo.
– Haihitaji kuenda kwa mtoa huduma za matibabu au agizo la daktari (5).
Je kuna madhara yoyote ya mbinu ya kuchomoa uume?
Mbinu ya kuchomoa uume haina madhara. Lakini kuna hatari ya kushika mimba kabla uwe tayari.
Ni yapi mabaya ya mbinu ya kuchomoa uume?
-Ni ngumu kufanya kwa njia sahihi kila wakati. Ingawa kuchomoa uume ni bora kushinda kutotumia njia yoyote ya uzuiaji mimba, ina hatari kiasi ikiwa hautaki kushika ,mimba.
-Kiwango cha kufeli kwa njia hii kiko juu. Kama hautaki kushika mimba, unapaswa kutumia njia ingine ya uzuiaji mimba (5).
-Ina jitihada kubwa. Mwanamume lazima avute nje uume kila wakati mnafanya ngono.
-Haitoi kinga dhidi ya magonjwa ya zinaa (STIs), ikiwemo VVU.
-Ni ngumu kukumbuka kama umelewa.