Mbinu ya kuchomoa uume au kuvuta nje ni nini?
Kuchomoa uume ni moja wapo wa mbinu za zamani sana. Ni rahisi sana-mwanamume anavuta uume nje ya uke kabla amwage manii. Pia inajulikana kama “mbinu ya kuvuta nje” ama “katiza ngono’ (coitus interruptus). Ili mbinu hii ifanye kazi, unapaswa kuifanya sahihi kila wakati (1).
Ni kwa njia gani kuchomoa uume huzuia mimba?
Mbinu ya kuchomoa uume hutegemea mwanamume na kujidhibiti kwake. Anahitaji kutoa uume ukeni kabla amwage manii. Mbinu hii hufanya kazi wakati shahawa inawekwa mbali na uke wa mwanamke, kwa hivyo mwanamume lazima aelewe mitindo yake ya kingono (2).
Ni kwa hali gani kuchomoa uume huzingatiwa ni njia ya kufaa wanandoa?
Mbinu ya kuchomoa uume inaweza kuzingatiwa ya kufaa wenzi wa kingono ambao
-wanafashiriki ngono mara chache;
-hawataki kutumia njia ingine ya uzuiaji mimba;
-wanangoja kuanza kutumia njia ingine ya uzuiaji mimba; na
-hawawezi kupata njia ingine ya uzuiaji mimba (3).