-Ina jitihada kubwa. Kufuatilia kila siku kunahitajika kutumia njia za kutegemea uelewa wa uzazi sahihi, na pia unahitaji muda wa kupanga na kuweka rekodi.
-Dawa zingine zinaweza kusababisha mabadiliko kwa ute wa uke, na kuifanya iwe vigumu kutabiri njia zingine za uelewa wa uzazi.
-Inahitaji kujidhibiti.Utahitaji kuepuka ngono au kutumia njia mbadala ya uzuiaji mimba kwa angalau wiki moja kila mzunguko wa hedhi.
-Inafanya kazi tu ikiwa wewe na mwenza wako mtashirikiana.
Mbinu za kalenda na siku sanifu hazifanyi kazi kwa wanawake ambao wana hedhi isiyotabirika, ikiwemo vijana (9).
-Kama hivi karibuni umewacha matumizi ya njia ya uzuiaji mimba yenye homoni, unahitaji kutumia njia bila homoni kwa miezi michache.Homoni huathiri mzunguko wa hedhi, na itafanya njia za uelewa uzazi kukosa ufanisi mwanzoni. Tumia njia bila homoni wakati unajifunza kufuatilia mzunguko wako wa hedhi.
-Haitoi kinga dhidi ya magonjwa ya zinaa (STISs) ikiwemo VVU.
Je, njia za uelewa wa uzazi zina madhara yoyote?
La. Hakuna madhara ama hatari zinazojulikana wakati unatumia njia za uelewa wa uzazi.