Njia za uelewa wa uzazi

Njia za uelewa wa uzazi
Njia za uelewa wa uzazi

Njia za uelewa wa uzazi ni nini?

Njia za uelewa wa uzazi, pia zinazojulikana kama “njia ya kiasili ya kupanga uzazi” “njia ya wizani” au “kuepuka ngono kipindi fulani”, ni aina ya mbinu ya uzuiaji mimba ambayo inakuhitaji kuweka rekodi za mzunguko wa hedhi yako ili kubaini siku ambazo unaweza kushika mimba. Hauhitaji kutumia kifaa chochote ama dawa. Kuna njia za uelewa uzazi ambazo zinaweza kutumika peke zao ama zitumiwe kwa pamoja kufuatilia mwanzo na mwisho wa kipindi chako cha urutubisho (1).

Njia za uelewa uzazi zinakusaidia kutabiri ni lini unaweza kushika mimba (siku zako za urutubisho) na zinategemea wewe kuepuka ngono siku hizo. Njia hizi zinakuhitaji kufahamu mabadiliko kwenye mwili wako au kuweka rekodi za siku kulingana na kanuni maalum za njia uliyochagua (2).

Unaweza kushika mimba wakati wa urutubisho wa mzunguko wako wa hedhi, ambayo inaweza kuenda kati ya siku nane na tisa. Wakati wa urutubisho, yai linawachiliwa na ovari (mchakato unaoitwa kupevuka kwa yai) na linaweza kuishi hadi saa 24. Manii, hata hivyo, inaweza kuishi ndani ya mfumo wako wa uzazi hadi siku saba. Kama manii itakuwepo wakati yai limewachiliwa, manii na yai zinaweza kuungana, na kusababisha mimba. Ni muhimu kujua kwamba ukifanya ngono bila kinga hadi siku saba kabla kupevuka kwa yai, bao kuna uwezo wa kushika mimba (3).

Njia za uelewa wa uzazi ziko rahisi.Unafuatilia mzunguko wako wa hedhi na haufanyi ngono siku ambazo unaweza kushika mimba. Kama utafanya ngono siku hizo, tumia njia mbadala ya uzuiaji mimba kama vile kondomu-ya nje au ya ndani-ama dayaframu.

Aina tofauti za njia za uelewa uzazi ni gani?

Kuna aina kadhaa za mbinu unaweza kutumia kufuatilia urutubisho wako na kubaini siku zipi ndani ya mzunguko wako wa hedhi ambazo unaweza kushika mimba.Utahitaji kuchunguza mabadiliko mwilini mwako ili uhesabu uko wapi ndani ya mzunguko wa hedhi. Hii itachukua jitihada nyingi na kujitolea. Kabla uchague mbinu hii, hakikisha unaelewa unachopaswa kufanya. Kuwa tayari kutofanya ngono kwa siku saba kila mwezi ama kutumia njia ingine ya uzuiaji mimba siku hizo.

Njia za uelewa uzazi zimeainishwa katika mbinu ya kalenda- na mbinu za dalili (4)

Mbinu za kalenda

Mbinu ya wizani ya kalenda. Mbinu ya wizani ya kalenda inasaidia kutabiri siku zako za urutubisho kwa kufuatilia mzunguko wako wa hedhi kwa miezi kadhaa. Mzunguko unaanza siku ya kwanza ya hedhi, na ni hapo unaanza kuhesabu. Kubaini siku zako za urutubisho, unapaswa kurekodi angalau hedhi 6-12 kabla ya kutumia mbinu hii, kisha hesabu siku kati ya siku ya kwanza ya kila mzunguko wa hedhi.

Kubaino mwanzo wa siku zako za rutuba, ondoa siku 20 kutoka kwa jumla ya siku za mzunguko wako wa hedhi mfupi sana. Kubaini mwisho wa siku zako za rutuba, ondoa siku 10 kwa jumla ya siku za mzunguko wako wa hedhi mrefu zaidi. Unapaswa kuepuka ngono bila kinga siku zako za rutuba (5).

Unaweza kutumia kitu cha kukusaidia kukumbuka, kama vile programu ya hedhi ama gurudumu la hedhi, au weka tu alama ya siku za hedhi kwenye kalenda yako ya kawaida.

Kama siku kati ya hedhi zako ziko chini ya siku 27, hii mbinu haipendekezwi kwako. Inaweza kutumiwa tu na wanawake ambao wana hedhi za kutabirika.

Mbinu ya siku sanifu (SDM). Hii mbinu inapendekezwa kwa wanawake ambao mzunguko yao ya hedhi uko kati ya siku 26 na 32. Utahitaji kufuatilia siku za hedhi yako na uepuke kufanya ngono bila kinga kuanzia siku ya 8 hadi siku ya 19 ya mzunguko wako. Wanawake wengine hutumia shanga za rangi (k.m shanga za mzunguko wa hedhi) kufuatilia mizunguko yao ya hedhi, ikiwa shanga nyeupe zina ashiria siku za kuepuka ngono bila kinga (siku za urutubisho) au watumie njia ya ziada ya uzuiaji mimba (6).

Jinsi ya kufuatilia mzunguko wa hedhi kutumia shanga

Mbinu za kutegemea dalili

Mbinu za kutegemea dalili zinahusisha kuchunguza ishara za urutubisho, kama vile ute ya shingo ya uzazi na joto la msingi la mwili. Unahitaji kuepuka ngono wakati dalili hizi zipo. Mbinu hizi zinajumuisha

mbinu ya Siku Mbili (TDM). Utachunguza mchozo wa uke kila siku ili kubaini kama una ute ya shingo ya kizazi. Kuepuka kushika mimba, lazima uepuke ngono bila kinga siku utaona ute ya shingo ya kizazi na siku ya kufuata. Ukiamua kufanya ngono, unapswa kutumia njia ingine ya uzuiaji mimba, kama vile kondomu, hadi ute uishe.

mbinu ya joto la msingi la mwili (BBT). Hii inatumia joto la mwili la mwanamke kubaini ni lini kuna uwezo ana urutubisho. Baada ya kupevuka kwa yai, joto la mwili la mwanamke huongezeka kidogo. Hauna uwezo wa kushika mimba katika kipindi kati ya siku tatu baada ya kuongezeka kwa joto la mwili na mwanzo wa hedhi yako ya kufuata. Kwa mbinu hii, unapaswa kufuatilia joto lako la mwili kila asubuhi kubaini kama uko katika wakati wa kupevuka yai au la. Utapima joto la mwili kila asubuhi kabla usimame na kuiandika kwenye chati. Mbinu hii ina ufanisi sana ikitumiwa pamoja na mbinu ya dalilijoto (symptothermal) ama mbinu ya siku sanifu (1).

mbinu ya kupevuka kwa yai. Pia inajulikana mbinu ya ute wa shingo ya kizazi ama mbinu ya “billing”, inajumuisha kuchunguza ute wa shingo ya kizazi kutambua mwanzo na mwisho wa kipindi cha urutubisho wa mwanamke.Siku nyingu, ute wa shingo ya kizazi ya mwanamke huwa nzito na yenye mnato, lakini wakati unapevuka yai unakuwa yenye majimaji na ya kuteleza. Unahitaji kuchunguza ute ya shingo ya kizazi kila siku. Unaweza kushika mimba kuanzia mwanzo wa ute (wakati ute wa shingo ya kizazi uko angavu,unanyooka, unateleza na una majimaji) hadi siku tatu baada iishe. Kutumia mbinu hii pamoja na mbinu ya joto la msingi la mwili ama siku sanifu kunaongeza ufanisi wake (5).

mbinu ya dalili-joto. Mbinu hii huchanganya mbinu nyingi za uelewa wa uzazi ili kubaini siku unaweza kushika mimba. Mwili wako una ishara nyingi za kuonyesha kwamba unaweza kushika mimba, na mbinu hii hufuatilia baadhi yao kwa wakati mmoja. Hii hujumuisha uwazi shingo ya kizazi uhisi,joto lako la msingi la mwili, na ute wa shingo ya kizazi. Kutumia mbinu mbili au zaidi kutakusaidia kuzuia mimba kwa namna bora (7).

Njia ya uelewa wa uzazi una ufanisi wa kiasi gani?

-Njia za uelewa wa uzazi hazina ufanisi sana. Zina fanya kazi viziri sana kama zitatumiwa kikamilifu (8).
-Kwa matumizi kamilifu, zina ufanisi wa asilimia 95-99. Kwa matumizi ya kawaida, zina ufanisi wa asilimia 76-88 (9).

Soma chati hapa chini kwa taarifa zaidi kuhusu ufanisi wa kila mbinu ya njia ya uelewa wa uzazi.

Ni kwa hali gani njia ya uelewa wa uzazi utakuwa chaguo bora?

Kama unajaribu kujua mwili wako vizuri. Njia za uelewa wa uzazi ni njia nzuri ya kugundua mitindo ya mwili wako. Utajua wakati kuna mabadiliko yoyote na uelewe mzunguko wako wa hedhi bora zaidi.

kama haujali kishika mimba. Kama hautatumia njia hizi sahihi, kiwango cha kufeli kwao kiko juu. Kama uko tayari kujaribu njia za uelewa wa uzazi, unashauriwa kutumia njia ya ziada ya uzuiaji mimba, kama kondomu, wakati bado unajifunza kufuatilia kalenda yako na/au dalili. Lakini kama haufahamu vizuri kuhusu kufuatilia njia za uelewa wa uzazi na kushika mimba itakuwa shida kwako, zingatia kutumia njia ingine ya uzuiaji mimba.

kama una nidhamu ya kibinafsi kamili. Wewe na mwenza wako mnahitaji kukubaliana kutumia njia hii. Pia unahitaji kujua mwili wako vizuri.

kama uko sawa kutofanya ngono kwa kipindi fulani cha mzunguko wa hedhi au kutumia njia ingine ya uzuiaji wakati wa kipindi cha urutubisho. Na njia hii, utahitaji kufuatilia siku ambazo unaweza kushika mimba kila mwezi. Siku hizo, utahitaji kuepuka ngono ama kutumia njia ya uzuiaji mimba bila homoni. Kama hauko sawa na kuepuka ngono ama kutumia njia ingine ya uzazi wa mpango, usitumie njia za kutegemea uelewa wa uzazi.

kama unataka njia bila madhara. Mbinu hii haiongezi homoni za ziada mwilimi mwako. watu wengi wanaotumia njia hii wanataka kitu ambacho hakita athiri mwili yao.

Chati ya njia za uelewa wa uzazi

Maswali elekezi kwa mbinu za kuzuia mimba

Je, unahitaji usaidizi zaidi kuchagua njia yako bora? Jibu maswali yetu elekezi kwa mbinu za kuzuia mimba.

Jibu maswali machache rahisi, na kulingana na majibu, tutapendekeza chaguo za uzuiaji mimba ambazo zinaweza kukufaa.

Jibu maswali
External Condom

Compare with similar Contraceptive Methods

Are you wondering if condoms are better than daily pills? Or if you should opt for a birth control implant? We're here to assist you in making this decision. You can select up to 5 contraceptive methods and compare them side by side to weigh the pros and cons of each.

Give a try to our Contraceptive Tool

In the example below, you'll find similar methods to the one you're currently reading about. Feel free to click on any that catch your interest or revisit our Contraceptive Methods page

Our Monthly Top Articles

Mnong’onezaji wa mambo ya uke: Jinsi ya kupenda uke wako hivyo ilivyo

Mnong’onezaji wa mambo ya uke: Jinsi ya kupenda uke wako hivyo ilivyo

Kabla tuzungumzie mambo ya kuthamini uke, tucheze mchezo ambapo una alama 50 kutoka mwanzo. Nina orodha ya maswali 5 na ikiwa umawahi fanya kile kilichoulizwa kwenye swali, unapoteza alama 10. Twen...

Njia 6 tunaweza kuchukua udhibiti wa uzazi wa mpango kama wanaume

Njia 6 tunaweza kuchukua udhibiti wa uzazi wa mpango kama wanaume

Ingawa ngono salama ni jukumu la wanaume na wanawake, mambo ya uzazi wa mpango imechukuliwa tangu kitambo  kama jukumu la mwanamke. Ingekuwa wanaume wangechukua jukumu la kutumia njia za kuzuia mim...

Mnong’onezaji wa mambo ya uke: Jinsi ya kupenda uke wako hivyo ilivyo

Mnong’onezaji wa mambo ya uke: Jinsi ya kupenda uke wako hivyo ilivyo

Kabla tuzungumzie mambo ya kuthamini uke, tucheze mchezo ambapo una alama 50 kutoka mwanzo. Nina orodha ya maswali 5 na ikiwa umawahi fanya kile kilichoulizwa kwenye swali, unapoteza alama 10. Twen...

Njia 6 tunaweza kuchukua udhibiti wa uzazi wa mpango kama wanaume

Njia 6 tunaweza kuchukua udhibiti wa uzazi wa mpango kama wanaume

Ingawa ngono salama ni jukumu la wanaume na wanawake, mambo ya uzazi wa mpango imechukuliwa tangu kitambo  kama jukumu la mwanamke. Ingekuwa wanaume wangechukua jukumu la kutumia njia za kuzuia mim...

Mnong’onezaji wa mambo ya uke: Mambo yanayohatarisha uke na njia za kuitunza

Mnong’onezaji wa mambo ya uke: Mambo yanayohatarisha uke na njia za kuitunza

Uke ni sehemu moja ya mwili isiyoeleweka vizuri. Ingekuwa uke wako ungeweza kuongea,  ungekuambia nini? Nadhani unge changanyikiwa cha kusema. Mara tunaona makala inayosema safisha uke wako na tena...