Je, ngono katika sehemu za nje ni aina ya mbinu ya kuepuka ngono?

Je, ngono katika sehemu za nje ni aina ya mbinu ya kuepuka ngono?
Je, ngono katika sehemu za nje ni aina ya mbinu ya kuepuka ngono?

Ngono katika sehemu za nje ni nini?

Kwa mujibu wa Cosmopolitan, maneno ” ngona katika sehemu za nje” yalibuniwa mnamo 1980 na Carol Queen, mtaalamu wa maswala ya ngono na mwandishi ambaye alitaka watu waelewe tofauti kati ya “ngono” na vitendo vingine vya kingono vya kuleta furaha, ambavyo watu wanaweza kufurahia bila kufanya ngono ya uume kuingia ndani ya uke.

Ngono katika sehemu za nje inachukuliwa kuwa vitendo vya kimapenzi au kingono ambavyo havihusishi uume ndani ya uke. Ingawa unaweza kuepuka ngono ya uke, bado unaweza kufanya vitendo vingine vya kingono. Kutegemea jinsi watu mbalimbali wanafafanua ngono, watu wengine huchukulia ngono katika sehemu za nje kama aina ya mbinu ya kuepuka ngono (4).

Sawa na mbinu ya kuepuka ngono, ufafanuzi wa ngono katika sehemu za nje hutofautiana. Kwa watu wengine, ngono katika sehemu za nje ni chochote ambacho hakihusishi uume kuingia katika uke, mkundu au mdomo, na wengine huichukulia kama kitendo chochote cha kingono, ikijumuisha katika uke, mkundu au mdomo, ambacho hakihusishi uume. Kulingana na ufafanuzi wako, hapa chini kuna vitendo ambavyo vinaweza kuchukuliwa kama ngono katika sehemu za nje.

Vitendo vinavyochukuliwa kama ngono katika sehemu za nje

Ngono ya mkundu

Hii inaweza kufanywa na watu wa jinsia yoyote ambao wana uume ama kifaa cha ngono. Vifaa vya ngono vya ngono ya mkundu vinaweza kuwa tofauti na vifaa vya ngono vya kutumiwa ukeni.

Ingawa watu wengine huchukulia ngono ya mkundu kama aina ya mbinu ya kuepuka ngono, wengine huichukulia kama aina kamili ya ngono ambayo sio sehemu ya kuepuka ngono ama ngono katika sehemu za nje.

Licha ya jinsi unachukulia ngono ya mkundu, lazima uchukue tahadhari ya hatari ya kuambukizwa magonjwa ya zinaa kwa

-kutumia kinga (kondomu ya nje au ya ndani inapendekezwa);
-kutotumia kifaa kimoja cha ngono kwenye uke na mkundu bila kukiosha kwanza; na
-kudumisha usafi sahihi katika mkundu.

Ngono ya mdomoni

Hii inajumuisha mwenza wako kutumia mdomo yao katika sehemu zako za msisimko wa raha, ikiwemo sehemu za siri. Kwa mawasiliano mazuri, ngono ya mdomoni inaweza kuwa njia ya kufurahisha ya kumpa raha mwenza wako. Watu wengine hawachukulii ngono ya mdomoni kama aina ya mbinu ya kuepuka ngono ama ngono katika sehemu za nje.

Licha ya hayo, ngono ya mdomoni haikupi wewe ama mwenza wako kinga dhidi ya magonjwa ya zinaa. Hakikisha kubaki salama kwa kutumia kizuizi ya ulingo wa mpira, kama vile kondomu ama dental dam. Hii itazuia mchozo wa uke na shahawa, ama kitu chochote kutoka sehemu mbalimbali ya mwili wa mwenza wako kuingia mdomoni mwako.

Kuchechemua mwenza wako kwa mikono

Wenza wanaweza kujipa raha kwa kutumia sehemu zingine za mwili, ikiwemo mikono na vidole (kutia vidole).

Kugusana

Hii inajumuisha kujisaga kwa mwili wa mweza wako ili kujifurahisha. Hii inaweza kujumuisha kujichechemua kingono bila hata kuvua nguo zako.

Kutumia vifaa vya ngono

Hii inajumuisha kuchechemua sehemu zako au za mwenza wako za kimapenzi kwa kutumia vifaa bila uhai ambavyo vimeundwa maalum kwa vitendo vya ngono na raha. Kuna aina mbalimbali ya vifaa vya ngono kwa vitendo tofauti.

Sawa tu na ngono ya mdomoni na ya mkundu, watu wengine hawachukulii matumizi ya vifaa vya ngono kama aina ya kuepuka ngono ama ngono katika sehemu za nje. Wengine wanaichukulia hivyo, kwasababu haihusishi ngono ya uume ndani ya uke.

Ingawa vifaa vya ngono haviwezi kusababisha mimba, vinaweza kueneza magonjwa ya zinaa (STIs). Kama unatumia vifaa vya ngono, kila mara hakikisha unadumisha usafi wa kiwango cha juu na ufuate tahadhari zifuatazo za usalama:

-Kila mara kumbuka kusafisha vifaa vyako kwa sabuni bila manukato baada ya matumizi.
-Usimpe mtu mwingine vifaa vya ngono, hasa vile vinatumika sehemu za ndani. Ukiamua kupeana, hakikisha kuwa umetumia kondomu pamoja na kifaa uliwacha mtu mwingine akatumia.
-Epuka kutumia kifaa kimoja kwa wakati moja ndani ya mkundu na ndani ya uke. Safisha kifaa kilichotumiwa ndani ya mkundu kwanza kabla uitumie sehemu ingine.

Kubusu

Kwa ujumla, haizingatiwi kama aina ya ngono. Wenza wengine huzuia mimba kwa kufurahia tendo la kubusiana na kwa wakati huo kuepuka kitendo chochoto cha kingono cha ndani.

Kupiga punyeto pamoja

Kwa wenza wengine, kupigana punyeto pamoja (unapiga punyeto ukiwa na mwenza wako) inachukuliwa kama njia moja ya kuepuka ngono ya ndani na hivyo hatari ya mimba.

Kusinga

Kusingana na mwenza wako kunaweza kuleta furaha ya ngono ikiwa mnatekeleza mbinu ya kuepuka ngono (6).

Je,unaweza kushika mimba ukifanya ngono katika sehemu za nje?

Ndio. Hii hufanyika wakati manii inaingia ndani ya uke. Kwa mfano, wakati uume uliosimama unagusa uke, wakati mwenza anamwaga manii karibu sana na uke, au wakati vidole vilivyoshika shahawa vinagusa uke kabla vioshwe.

Kitendo chochote cha kingono ambacho hakihusishi kuingiza shahawa kwenye uke hakiwezi kusababisha mimba.

Je, unaweza kuambukizwa magonjwa ya zinaa ukifanya ngono katika sehemu za nje?

Ndio. Kufanya ngono katika sehemu za nje hakukukingi dhidi ya magonjwa ya zinaa. Maambukizo mengine yanapitishwa kwa njia ya mdomo, mkundu au ngozi kugusana.

Je “kuloweshana kingono” (sexual soaking) ni aina ya ngono katika sehemu za nje?

Sexual soaking” ni istilahi iliyopewa umaarufu na vijana wa Mormom kule TikTok. Wanafafanua “soaking” kama kitendo cha kingono ambacho kinahusisha ngono ya ndani lakini hakuna kusukuma nyonga ama kusonga. Kwa urahisi, mwamume anaingiza uume ndani ya uke, kisha analala tu hapo bila kusukuma kwa njia yoyote. Kitendo hiki kina umaarufu kati ya wa Mormon ambao hawajaoa, na wale wanaokifanya hawakichukulii kama kitendo cha ngono.

Ingawa ufafanuzi wa “soaking” kati ya wale wanaoifanya inatokana na imani ya maadili kwamba kuingiza uume bila kusukuma sio ngono (na kwa hivyo sio “dhambi”), kitendo hiki kinaweza kusababisha mimba au kueneza magonjwa ya zinaa.

Ni wakati gani unaweza kufanya ngono katika sehemu za nje?

-Wakati mwenza wako havutiwi au hayuko tayari kufanya ngono ya ndani.
-Wakati hautumii aina yoyote ya njia za uzuiaji mimba.
-Kama unatumia njia ya uelewa wa uzazi na mwenza wa kike yumo katika siku zake za urutubisho.
-Kama wewe ama mwenza wako mna maambukizi ama hali ambayo inaweza kuwazuia nyote ama mmoja wenu kufurahia ngono ya uume ndani ya uke.

Maswali elekezi kwa mbinu za kuzuia mimba

Je, unahitaji usaidizi zaidi kuchagua njia yako bora? Jibu maswali yetu elekezi kwa mbinu za kuzuia mimba.

Jibu maswali machache rahisi, na kulingana na majibu, tutapendekeza chaguo za uzuiaji mimba ambazo zinaweza kukufaa.

Jibu maswali
External Condom

Compare with similar Contraceptive Methods

Are you wondering if condoms are better than daily pills? Or if you should opt for a birth control implant? We're here to assist you in making this decision. You can select up to 5 contraceptive methods and compare them side by side to weigh the pros and cons of each.

Give a try to our Contraceptive Tool

In the example below, you'll find similar methods to the one you're currently reading about. Feel free to click on any that catch your interest or revisit our Contraceptive Methods page

Our Monthly Top Articles

Mnong’onezaji wa mambo ya uke: Jinsi ya kupenda uke wako hivyo ilivyo

Mnong’onezaji wa mambo ya uke: Jinsi ya kupenda uke wako hivyo ilivyo

Kabla tuzungumzie mambo ya kuthamini uke, tucheze mchezo ambapo una alama 50 kutoka mwanzo. Nina orodha ya maswali 5 na ikiwa umawahi fanya kile kilichoulizwa kwenye swali, unapoteza alama 10. Twen...

Njia 6 tunaweza kuchukua udhibiti wa uzazi wa mpango kama wanaume

Njia 6 tunaweza kuchukua udhibiti wa uzazi wa mpango kama wanaume

Ingawa ngono salama ni jukumu la wanaume na wanawake, mambo ya uzazi wa mpango imechukuliwa tangu kitambo  kama jukumu la mwanamke. Ingekuwa wanaume wangechukua jukumu la kutumia njia za kuzuia mim...

Mnong’onezaji wa mambo ya uke: Jinsi ya kupenda uke wako hivyo ilivyo

Mnong’onezaji wa mambo ya uke: Jinsi ya kupenda uke wako hivyo ilivyo

Kabla tuzungumzie mambo ya kuthamini uke, tucheze mchezo ambapo una alama 50 kutoka mwanzo. Nina orodha ya maswali 5 na ikiwa umawahi fanya kile kilichoulizwa kwenye swali, unapoteza alama 10. Twen...

Njia 6 tunaweza kuchukua udhibiti wa uzazi wa mpango kama wanaume

Njia 6 tunaweza kuchukua udhibiti wa uzazi wa mpango kama wanaume

Ingawa ngono salama ni jukumu la wanaume na wanawake, mambo ya uzazi wa mpango imechukuliwa tangu kitambo  kama jukumu la mwanamke. Ingekuwa wanaume wangechukua jukumu la kutumia njia za kuzuia mim...

Mnong’onezaji wa mambo ya uke: Mambo yanayohatarisha uke na njia za kuitunza

Mnong’onezaji wa mambo ya uke: Mambo yanayohatarisha uke na njia za kuitunza

Uke ni sehemu moja ya mwili isiyoeleweka vizuri. Ingekuwa uke wako ungeweza kuongea,  ungekuambia nini? Nadhani unge changanyikiwa cha kusema. Mara tunaona makala inayosema safisha uke wako na tena...