Ni yapi mazuri ya kuepuka ngono?
-Kinadharia,Kuepuka ngono ndio njia yenye ufanisi zaidi ya uzuiaji mimba.
-Ni fursa bora ya kukuwa mbinifu kwa namna unafanya mapenzi na kuonyesha mwenza wako mapenzi. Kuna njia zingine za kufanya hivi ikiwemo vitendo visivyohusisha ngono kama kutembea pamoja, kukula pamoja, kubadilishana zawadi na mengineo.
-Haigharimu chochote.
-Haina madhara yoyote.
-Inaweza kuwapa wenza fursa ya kujuana bora zaidi na kwa hivyo, kuboresha uhusiano yao (6).
Ni yapi mabaya ya kuepuka ngono?
-Inajitihada kubwa. Lazima uwe na uwezo mkubwa wa kujidhibiti, na inafanya tu kazi kama hautafanya ngono ya uke (lakini unaweza kufanya ngono ya mdomoni au mkundu).
-Inahitaji nidhamu na kujitolea. Kusema “sio sasa hivi” inafanya tu kazi kama njia ya uzuiaji mimba kama unaifanya mfululizo.
-Inahitaji mawasilino mazuri na mwenza wako.Kama mnachumbiana ama uko katika uhusiano, utahitaji kuwa na uwezo wa kumwambia mwenza wako kile kiko sawa na kile hakiko sawa. Hii inamaanisha kuwa unapswa kuwa huru kuzungumza na mwenza wako kuhusu umbali uko tayari kuenda katika kufanya mambo ya kingono.
-Inahitaji uwe na mwenza anaye kujali. Kama uko katika uhusiano, nyote wawili mnapaswa kuwa sawa na kutofanya ngono ya uke. Lakini kumbuka, kusema “sio sasa hivi” haimanishi haujaruhusiwa kufanya mambo ya kukufurahisha.
-Inaweza kuwa ngumu kuendeleza.
-Ni ngumu kufuata mpangilio ikiwa umelewa.
-Haitoi kinga dhidi ya magonjwa ya zinaa.