Mbinu ya kuepuka ngono ama “sio sasa hivi” ni nini?
Mbinu ya kuepuka ngono, ama “sio sasa hivi”, ni kuchelewesha ama kuepuka vitendo vyote au vingine vya ngono. Kama hautafanya ngono ya ukeni, hautashika mimba. Kwa maana mpana, maneno kuepuka ngono yanaweza kumaanishsa vitu tofauti kwa watu tofauti.
Kama unafikiria kuhusu mbinu ya kuepuka ngono kama njia ya uzuiaji mimba, inafafanuliwa kama kuepuka vitendo vya ngono ambavyo huweka manii kwenye uke. Ufafanuzi huu, hata hivyo, hautambui kuwa magonjwa mengine ya zinaa yanaweza kupitishwa kupitia ngozi kugusana.
Kuepuka ngono kimsingi inafanywa wakati mtu ambaye hajawahi kushiriki ngono anachelewesha vitendo vingine ama vyote vya kingono.
Kuepuka ngono ya ufuatilizi inafanywa wakati mtu awali amekuwa akishiriki ngono anaamua kwa makusidi kuchelewesha au kuwacah vitendo vyote au vingine vya ngono.
Kuepuka ngono vipindi fulani inafafanuliwa kama hali ya mtu ambaye hushiriki ngono kuepuka ngono ya uume ndani ya uke wakati wa siku za urutubisho wa mzunguko wa hedhi (1).
Mtu anaweza kuchagua kuepuka ngono ya uke pekee lakini bado aendelee na aina zingine za ngono. Kushiriki vitendo hivyo vingine vya ngono kunafafanuliwa na Planned Parenthood kama ngono katika sehemu za nje.
Mbinu ya kuepuka ngono hufanya aje kazi?
kama haufanyi ngono ya ukeni, hautashika mimba. Mbinu hii ni uamuzi wa kufahamu na wa makusudi wa kutofanya ngono ya uke. Ni uamuzi utahitaji kukumbuka kila siku.
Ili kuendelea kutekeleza mbinu hii, lazima uendelee kujikumbusha kwanini ulichagua kuepuka ngono. Pia kufikiria juu ya matokeo yanayowezekana kama utabadilisha mawazo kutakusaidia. Kama utaamua kufanya ngono, hakikisha umejikinga na njia ingine yenye ufanisi ya uzuiaji mimba.
Mbinu ya kuepuka ngono hutekelezwa vipi?
Ingawa hakuna namna moja ya kutekeleza mbinu ya kuepuka ngono, hapa kuna vidokezo muhimu ambavyo vitakusaidia kutekeleza mbinu ya kuepuka mimba kwa ufanisi:
-Epuka kujiweka katika hali ambazo zitafanya iwe ngumu kutekeleza uamuzi wako.
-Wakiti inawezakana, zingatia kuepuka pombe na dawa ambazo zinaweza kuchanganya hekima yako.
-Tafuta watu unaoweza kuzungumza nao kuhusu uamuzi wako na uwategemee kwa usaidizi.
-Zungumzia uamuzi wako na mweza wako vizuri kabla muanze kufanya ngono.
-Sema ukweli kwa njia wazi kwa mwenza wako kuhusu mipaka yako.
-Jaribu njia zingine za kufanya mapenzi ambazo utafurahia kwa njia sawa.
-Kumbuka kijikinga dhidi ya magonjwa ya zinaa ambayo hayapitishwi kupitia ngono ya uke.
Mbinu ya kuepuka ngono ina ufanisi wa kiasi gani?
Wakati mtu anaepuka ngono ya uke, mbinu ya kuepuka ngono inaweza kuwa na ufanisi wa asilimia 100 wa kuzuia mimba. Ukiitumia kila wakati, una hakikishiwa hautapata mimba.Hata hivyo, inahitaji nidhamu ya binafsi na, kwa hivyo, watu wengine watapata ikiwa ngumu mno kutekeleza. Kama unatumia mbinu hii na pia kushiriki vitendo vingine vya ngono, mbinu hii ya kuepuka ngono huenda haitazuia magonjwa mengine ya zinaa (2).
Ingawa kinadharia mbinu ya kuepuka ngono ina ufanisi wa juu wa kuzuia mimba, watu wengi hawawezi kuitekeleza kwa njia sahihi. Cha muhimu, hakuna ushahidi wa kuonyesha kuwa programu za elimu kuhusu mbinu ya kuepuka mimba kwa vijana hupunguza hatari ya mimba isiyopangwa na magonjwa ya zinaa.Mbinu ya kuepuka ngono inajulikana kukuwa na ufanisi zaidi ikitumiwa na wanandoa wazee, waliokomaa na kukuwa na ufanisi wa chini ikitumiwa wakati kuna matumizi ya dawa na pombe na pia kama kuna hisia kali za kingono kati ya wenza (3).
Ni kwa hali gani unapaswa kuzingatia kutumia mbinu ya kuepuka ngono?
-Kama dini yako haikubali matumizi ya njia zingine za uzuiaji mimba.
-Kama umekubaliana na mwenza wako kuepuka ngono kwa sababu za kimaadili, kidini ama kitamaduni.
-Kama hauwezi kupata njia ingine ya uzuiaji mimba.