Jinsi ya Kuthibitisha Mimba

Jinsi ya Kuthibitisha Mimba

Tunapendekeza ujibu Maswali Mtandaoni kuhusu Mimba. Maswali haya yatakusaidia kutambua dalili za mimba na kukuongoza kwa hatua za kufuata. Kuthibitisha hali yako ya mimba kwa kutumia kipimo cha kuaminika ni muhimu ikiwa unashuku kuna uwezo una mimba.Vipimo vya damu au mkojo ndivyo njia sahihi zaidi na vinaweza kupatikana kupitia mtoa huduma za afya au vifaa vya kupima mimba nyumbani. Jifunze zaidi kuhusu vipimo vya mimba kwenye ukurasa huu.

Kipimo cha mimba ni nini?

Kipimo cha mimba kinagundua uwepo wa homoni wa human chorionic gonadotropin (hCG) kwenye mkojo au damu, ambayo inazalishwa tu wakati wa mimba.

Kila chapa cha kifaa cha kupima mimba kiko tofauti,kwa hivyo fuata maagizo ili uweze kusoma matokeo ipasavyo.

Aina za vipimo vya mimba

Kuna aina mbili za vipimo-mkojo na damu-na kila kimoja kina kiwango chake cha usahihi.

Pia vinajulikana kama “vipimo vya mimba nyumbani”, vipimo vya mkojo ni vya haraka, rahisi kutumia na vya faragha. Unaweka mkojo wako kwenye kifaa kilichotibiwa maalum ili ufanye kipimo. Unaweza fanya hivi kwa njia kadhaa:

Shikilia kifaa cha kipimo ili mkojo uipitie unapokojoa
Shikilia kifaa cha kipimo ili mkojo uipitie unapokojoa
Kusanya mkojo kwenye kikombe kisha ukitumbukize kifaa cha kupima ndani ya kikombe
Kusanya mkojo kwenye kikombe kisha ukitumbukize kifaa cha kupima ndani ya kikombe
Kusanya mkojo kwenye kikombe kisha utumie chombo cha kuachilia matone kwenye kifaa cha kupima
Kusanya mkojo kwenye kikombe kisha utumie chombo cha kuachilia matone kwenye kifaa cha kupima
Usahihi

Vipimo vya mkojo vinaweza kuwa sahihi kama vipimo vya damu, kwasababu vina usahihi wa 97-99%. Usahihi upo juu wakati hedhi tayari imechelewa.

Wakati wa kufanya kipimo

Inapendekezwa ungoje hadi siku ya kwanza ya kuchelewa kwa hedhi kabla ufanye kipimo cha mkojo cha mimba. Hii kwa kawaida itakuwa karibu wiki mbili baada ya kushika mimba. Hata hivyo, vipimo vingine vina usahihi kuliko vingine na vinaweza kufanywa mapema.

Ikiwa matokeo yataonyesha hauna mimba lakini bado unashuku kwamba kuna uwezo una mimba, jaribu kufanya kipimo tena baada ya wiki moja ili kuhakikisha.Vipimo vinginge vya mimba vya nyumbani vinapendekeza ufanye hivi licha ya matokeo ya kwanza.

Mahala pa kufanya kipimo

Unaweza kununua kipimo cha mimba cha nyumbani kwenye duka za kuuza dawa hata bila maagizo ya daktari. Bei italingana na chapa, lakini baadhi haviko ghali. Kulingana na nchi unapoishi,unaweza kupata vifaa vya kupima mimba kwa taasisi za kiafya za umma.Wakati unanunua kifaa cha kipimo cha mkojo,hakikisha hakijafikisha tarehe ya mwisho wa matumizi na usome maagizo kwa makini ili uelewe jinsi inavyofanya kazi.

Matokeo ya kipimo cha mimba

Kila chapa kina njia ya kuonyesha matokeo; inaweza kuwa ishara za kuongeza au kutoa, ishara za pau, ama kama ni kipimo cha kidijitali, inaweza kuonyesha maneno “mimba’ au ‘hakuna mimba’ Ni muhimu kusoma maagizo kwa makini ili ujue matokeo yataonekana vipi ili uepuke kukanganyikiwa.

Kwa vipimo visivyo vya kidijitali, lazima ukumbuke kwamba: Haijalishi ni kwa kiwango kipi matokeo yataonekana nyepesi au nyembamba, ukiona ishara ya “+” dhaifu au ishara ya pau moja ikiwa nene zaidi kuliko ingine,bado ni matokeo inayoonyesha kuwa kuna mimba.Utachukulia matokeo kuonyesha kuwa hakuna mimba wakati hakuna ishara ya pau ingine.

Bila shaka, kuna wakati kunatokea matokeo ya uongo ya kuwepo mimba, kipimo kinasema una mimba wakati hauna. Hili litafanyika ikiwa una damu au protini kwenye mkojo. Dawa zingine, kama vile dawa za kutuliza, dawa za kifafa, na dawa za uzazi, pia zinaweza kusababisha hili.

Matokeo ya kipimo cha mimba

Vipimo vya damu vinaweza kugundua mimba mapema kuliko kipimo cha mkojo- takriban siku sita au nane baada ya kupevuka kwa yai,lakini huchukua muda mrefu zaidi kupata matokeo kushinda kipimo cha mimba nyumbani.

Kuna aina mbili ya vipimo vya damu:

Ya kupima sifa

Aina hii ya kipimo huangalia kama kuna hCG kwenye damu yako au hakuna,na inaweza kugundua mimba karibu siku 10 baada ya utungisho.

Ya kupima idadi

Aina hii ya kipimo hupima viwango vya hCG kwenye damu na inaweza kuigundua hata ikiwa kwa viwango vya chini mno. Madaktari hutumia aina hii ya kipimo kuangalia mabadiliko kwenye kiwango cha hCG na kugundua mimba nje ya mfuko wa kizazi.

Ectopic Pregnancy – SW

Mimba nje ya mfuko wa kizazi hutokea wakati yai lililorutubishwa linapojipandikiza na kukuwa nje ya mfuko wa kizazi, hasa kwenye mirija ya uzazi, ambayo huunganisha ovari na mfuko wa kizazi.

Usahihi

Vipimo vya mimba vya damu huwa sahihi kwa takriban 99%

Wakati wa kufanya kipimo

Vipimo vya damu vinaweza kufanywa karibu siku saba baada ya kupevuka kwa yai (ambayo huwa takriban wiki moja kabla ya hedhi yako) na bado itoe matokeo sahihi.

Mahala pa kufanya kipimo

Kwa vipimo vya damu, unaweza kutembelea daktari au uende moja kwa moja kwenye maabara, baadhi hufanya kipimo hiki. Vina gharimu zaidi ya kipimo cha mkojo.

Matokeo ya kipimo

Mtoa huduma za afya anahitaji kusoma matokeo yako na kukuambia viwango vya hCG na ni kipi kinamaanisha. Viwango hivi vinapimwa kwa vitengo vya mili-international vya homoni ya hCG kwa kila milimita ya damu (mIU/mL).

Je unataka kujua ni vipi mimba hutungwa? Tembelea sehemu ya mimba hutungwa vipi? kufijunza zaidi kuihusu.

Ikiwa unataka kuchunguza chaguo mtu anazo wakati amepata mimba isiyopangwa, tembelea ukurasa wetu wa Chaguo zako baada mimba.

Iwapo mzunguko wako wa hedhi umevurugika, au haujapata hedhi kabisa, tunapendekeza ufanye kipimo cha mimba wiki tatu baada ya kufanya ngono bila kinga.

Matokeo ya kipimo

Marejeleo

“Pregnancy Tests.” Cleveland Clinic, https://my.clevelandclinic.org/health/diagnostics/9703-pregnancy-tests Accessed May 2024
“Pregnancy Tests.” Planned Parenthood, https://www.plannedparenthood.org/learn/pregnancy/pregnancy-tests Accessed May 2024.
“Pregnancy test instructions.” UNC School of Medicine, https://www.med.unc.edu/timetoconceive/study-participant-resources/pregnancy-test-instructions/ Accessed May 2024.
“HCG Blood Test-Quantitative.” University of California San Francisco: Benioff Childrens Hospital, https://www.ucsfbenioffchildrens.org/medical-tests/003509 Accessed May 2024.
“Knowing if you are pregnant” Office on Women Health, https://www.womenshealth.gov/pregnancy/you-get-pregnant/knowing-if-you-are-pregnant Accessed May 2024.
“What are HCG Levels?” American Pregnancy Association, https://americanpregnancy.org/getting-pregnant/hcg-levels/ Accessed May 2024.