Chaguzi za ujauzito

Tunaelewa kuwa kufanya uamuzi kuhusu ujauzito ambao hujaupanga unaweza kukulemea. Kabla ya kuamua jambo lolote, unahitaji kuthibitisha ujauzito wako, ujifunze mwenyewe kuhusu chaguzi zinazopatikana kwako, na kuchukua hatua fulani muhimu. Ili kurahisisha mchakato huu, jaribu kutafuta usaidizi kwa kujadiliana kuhusu chaguzi zako na mshirika wako, rafiki au jamaa mwaminifu au mtoa huduma wa afya anayetegemewa.
Chaguzi za ujauzito

Kumbuka – huu ni uamuzi wako na unapaswa kuchagua kile unachofikiri ni bora zaidi kwako.

Chukua muda wako kushughulikia habari hizi, na ukiamua kuendelea kuwa na ujauzito, jambo muhimu kwako ni kuhakikisha kwamba unawasiliana na daktari. Mtoa huduma wa afya atakuongoza katika mambo yote yanayohusu ujauzito, kwa hiyo ni muhimu kupanga mikutano naye ya mara kwa mara na kufuata ratiba yote.

Unapaswa kuanza kutumia virutubisho, kama vile asidi ya foliki na vitamini D, kwani husaidia katika ukuaji wa mtoto; kuacha sigara na kunywa pombe pia kupunguza kafeini. Unapaswa pia kujaribu kula chakula bora na kuepuka vyakula vinavyoaminika kuwa na madhara kwa mtoto; fanya mazoezi kwa usalama; hakikisha dawa yoyote unayotumia ni salama kwa mtoto; na utunze zaidi ustawi wako wa kimwili na kiakili. Daktari wako anaweza kupendekeza jambo hili, lakini ni vizuri kujua kabla.

Uamuzi wa kuwa mzazi si rahisi na ni haki yako kuchagua unachotaka kufanya. Ikiwa hutaki kutoa mimba lakini pia hutaki kuwa mama, unaweza kufikiria kutunza mtoto asiye wako.
Kuchagua hili kunamaanisha kupata mimba na kuzaa, na kisha kuruhusu mtu mwingine kumlea mtoto wako.

Kutunza mtoto asiye wako ni halali na jambo hili hufanyika katika zaidi ya nchi 160, na zaidi ya robo ya milioni wanafanya hivyo duniani kote kila mwaka. Baada ya muda, mila na sheria kuhusu kutunza mtoto aliyeasilishwa zilipitishwa na zimeendelea, zikizingatia zaidi juu ya ustawi wa mtoto. Hata hivyo, haki za mtoto aliyeasilishwa hutofautiana sana kutoka nchi hadi nchi. Katika baadhi ya maeneo, watoto waliyeasilishwa wana haki sawa na watoto wa kuzaliwa, kama vile haki ya kurithi, wakati katika maeneo mengine kuna sheria na kanuni tofauti, kwa mfano, kuwasiliana na wazazi wa kuzaliwa kunatarajiwa.

Kulingana na mahali unapoishi, tafuta mtu au shirika ambalo linaweza kukupa taarifa za ukweli kuhusu utamaduni na sheria na kukusaidia unapofikiria uamuzi huu.

Ikiwa umeamua kuwa huu sio wakati mwafaka wa kuwa mama, unaweza kutoa mimba. Kulingana na mahali unapoishi, inaweza kuwa vigumu au rahisi kufikia njia hii mbadala. Baadhi ya mambo mengine ambayo yanaweza kuathiri upatikanaji wa chaguo hili ni: umri wako, umri wa ujauzito na bima.

Kila mtu ana uzoefu tofauti na utowaji mimba; kwa wanawake wengine, ni njia rahisi na ya moja kwa moja, kwa wengine inaweza kuwaletea shida kubwa. Na hii ni sawa. Tunapendekeza utafute ushauri nasaha ili uweze kuchunguza chaguo hili na kufanya uamuzi wa busara.

Kuna njia mbili za kutoa mimba: njia ya kutumia vidonge na ya upasuaji.

Utoaji mimba kwa njia ya kutumia vidonge

Unaweza kumeza tembe ukiwa nyumbani ili kumaliza mimba isiyotakikana. Kuna dawa mbili salama: kutumia Mifepristone pamoja na Misoprostol, au kutumia Misoprostol pekee.

Kwa habari zaidi, unaweza kutembelea marafiki zetu kwenye howtouseabortionpill.org na safe2choose.org

Kufyonza utupu kwa mikono

Kufyonza utupu kwa mikono (MVA) ni njia salama sana ya kutoa mimba katika miezi mitatu ya kwanza ya ujauzito, na/au mapema miezi mitatu ya pili hadi wiki 14 za ujauzito. Kikomo cha umri wa ujauzito kwa MVA mara nyingi hutegemea kliniki, pamoja na mtoa huduma ya afya mwenye kutekeleza utaratibu huo.

MVA inafanywa na mtoa huduma aliyefunzwa katika kliniki na unaweza kupata maelezo zaidi kuhusu utaratibu huo hapa.

Marejeleo

Pregnancy Options, Bedsider, www.bedsider.org/pregnancy_options

Pregnancy Options, Planned Parenthood, www.plannedparenthood.org/learn/pregnancy/pregnancy-options

Pregnancy options, New Zealand Family Planning, www.familyplanning.org.nz/advice/pregnancy/pregnancy-options

Pregnancy Choices: Raising the Baby, Adoption, and Abortion, The American College of Obstetricians and Gynecologists, www.acog.org/patient-resources/faqs/pregnancy/pregnancy-choices-raising-the-baby-adoption-and-abortion

Guide to a Safe Manual Vacuum Aspiration Abortion (MVA)”, safe2choose, https://safe2choose.org/safe-abortion/inclinic-abortion/manual-vacuum-aspiration-mva-procedure