1. Ugonjwa wa asubuhi, ambayo licha ya jina, unaweza kufanyika muda wowote kwa siku. Ikiwa unahisi kichefuchefu na unatapika kila mara unapokula, ona daktari.
2. Mabadiliko kwenye matiti ambayo yanafanana na mabadiliko kabla ya hedhi, na pia hisia za kuchoma, mishipa kuonekana zaidi, na chuchu kuwa nyeusi na za kusimama zaidi.
Je nina mimba?
Maswali haya ya maingiliano yanakupa nafasi ya kuchagua ishara na dalili zako na kulingana na matokeo yako ya mwisho,utashauriwa kwa uwezo uliopo wa kuwa na mimba.
Je, ulishiriki ngono bila kinga katika siku 5 zilizopita?
Nitajua aje kwamba nina mimba?
Ikiwa hivi karibuni umefanya ngono bila kinga na unataka kujua kama huenda una mimba au hauna, kuna ishara na dalili fulani unaweza chunguza.
Kukosa hedhi huwa ishara ya kwanza ya mimba,lakini haitegemeki 100%. Hii ni kwasababu hedhi zinaweza kuchelewa kwasababu ya mambo kama, mfadhaiko, kubadili vyakula, madhara ya kutumia mbinu za kuzuia mimba, au tatizo la kimatibabu. Juu ya hayo, mbinu za uzuiaji mimba haziko kamili, na kulingana na ufanisi wa mbinu yako, kuna wakati mbinu za uzuiaji mimba zitafeli kuzuia mimba. Kujielimisha zaidi kuhusu ufanisi na madhara ya kando ya mbinu tofauti za uzuiaji mimba, tembelea, sehemu ya Mbinu za uzuiaji mimba.
Wakati ishara na dalili za mimba zinaweza kuwa tofauti kwa mtu mmoja hadi mwingine, dalili zozote kati ya hizi zinaweza kukuwa ishara kwamba una mimba.
Dalili za awali za mimba
3. Kukojoa mara kwa mara- unaweza kuanza kuamka katikati ya usiku kukojoa.
4. Choo kigumu
5. Majimaji ya ukeni- kuongezeka kwa ute nyeupe kama maziwa bila kuhisi uchungu wowote au kiwasho. Pia uke unaweza kutoa damu yenye rangi ya kahawia au waridi ambayo ni nyepesi na haitoki kwa muda sawa na hedhi.
6. Uchovu
7.Ladha ya kigeni-wanawake wengi wanaeleza kuhisi ladha kama ya chuma kwenye mdomo.
8. Tamaa ya chakula kubadilika visivyo kawaida kama vile kutopenda chai, kahawa, moshi ya tumbaku au vyakula vya mafuta.
9. Hamu isiyi ya kawaida.
Je unashuku kwamba una dalili za kwanza za mimba?
Tunapendekeza kwamba ujibu maswali yetu ya Maswali Kuhusu Mimba.
Lakini, ingawa maswali yatatumia dalili kusaidia kugundua uwezo wa kuwa na mimba, jinsi ya hakika ya kuthibiti ikiwa una mimba au hauna ni kupima mimba. Tembelea sehemu ya Jinsi ya Kuthibitisha mimba kwa mwongozo kuhusu kupima mimba.
Marejeleo
- “Pregnancy Symptoms: 10 Early Signs That You Might Be Pregnant”, WebMD, www.webmd.com/baby/guide/pregnancy-am-i-pregnant#1
- “Am I pregnant?”, NHS, www.nhs.uk/common-health-questions/pregnancy/am-i-pregnant/
- “Am I pregnant? Quiz”, Clearblue, March 2020, www.clearblue.com/am-i-pregnant/quiz
- “Am I Pregnant Quiz | Early signs of pregnancy”, Planned Parenthood, www.plannedparenthood.org/online-tools/am-i-pregnant
- “Am I pregnant? | Pregnancy Quiz”, Patient, www.plannedparenthood.org/online-tools/am-i-pregnant