Mimba hutungwa vipi?

Mimba hutungwa vipi?

Mimba hutungwa wakati manii inaingia kwenye mirija ya uzazi na kurutubisha yai. Manii inaweza kukutana na yai na kulirutubisha kwa njia mbalimbali:

  1. Manii inatoka kwa uume hadi ndani ya uke
  2. Manii inaingizwa ndani ya uke kwa njia ya uhamilishaji bandia au yai linarutubishwa nje ya mwili kisha linawekwa ndani ya mfuko wa kizazi.

Ni muhimu kujua kwamba hata ikiwa uwezo ni mdogo mno, bado manii inaweza kurutubisha yai bila uume kuingia ndani ya uke. Hili linawezakana ikiwa manii itamwagwa karibu na uke, au ikiwa majimaji ya uume inayotoka kabla ya manii itamwagika ndani au karibu na uke, au ikiwa manii itaingia kwenye uke kupitia vidole.

Hili lina maanisha kwamba sio lazima uume uingie kwenye uke ndipo mimba itungwe.

Anatomia ya nje ya kike
Anatomia ya nje ya kike
Sehemu ya uzazi ya ndani wa mwanamke
Sehemu ya uzazi ya ndani wa mwanamke
Mwili wa mwanaume
Mwili wa mwanaume

Jinsi mimba hutungwa

Mchakato ambalo huishia kwa mimba huanza katikati mwa mzunguko wa hedhi (yaani siku ya 14 kwa mzunguko wa siku 28), wakati yai lililokomaa linatoka kwenye ovari-hili linaitwa kupevuka kwa yai-na linasafiri kupitia mirija ya uzazi hadi mfuko wa kizazi.

Yai lililokomaa huishi kwa muda wa saa 12 hadi 24, ikisonga polepole ndani ya mirija ya kizazi. Ikiwa haitakutana na manii wakati huu, itakufa na kuondoka mwilini wakati wa hedhi inayofuata.
Ikiwa manii itaingia ndani ya uke, manii itaogelea kupitia shingo ya mfuko wa kizazi ili ifikie mirija ya kizazi ikitafuta yai. Zina hadi siku 6 kupata yai kabla zikufee, na zikikutana na yai, inaitwa rutubisho.
Hivyo, kuna uwezo wa hadi siku sita kati ya tendo la ngono na rutubisho.

Punde rutubisho inafanyika, yai linasafiri kupitia mirija ya kizazi ili kufika kwenye mfuko wa kizazi. Wakati wa safari hii, inaanza kugawanyika iwe na seli zaidi na zaidi, ikiunda mpira ikiendelea kukuwa. Mpira huu wa seli- unaoitwa blastocyst-hufika kwenye mfuko wa kizazi siku tatu au nne baada ya rutubisho.

Mpira wa seli huelea ndani ya mfuko wa kizazi kwa siku zingine mbili au tatu. Wakati unajiambatisha kwenye utando wa mfuko wa kizazi, inaitwa upandikizaji.

Mchakato wa upandikizaji huchukua siku tatu hadi nne kuisha na ni hapa ndipo mimba huanza rasmi. Kinachofanyika cha kufuata ni kwamba kiinitete kinakuwa kutoka kwenye seli ndani ya blastocyst, na kondo la nyuma-mfumo wa muda ambayo husambaza virutubisho na vitu vingine muhimu kwa kiinitete-hukua kutoka kwa seli zilizo nje ya blastocyst.

Wakati huu, homoni ya mimba huachiliwa ambayo huzuia utandu wa mfuko wa kizazi kujiachilia na kujitoa na kuenda mwilini, jinsi inavyofanyika wakati wa hedhi. Ni kwasababu hii watu hawaendi hedhi wakiwa na mimba.

Marejeleo