Ulihisi vipi mara yako ya kwanza kufanya ngono?

Ulihisi vipi mara yako ya kwanza kufanya ngono?

Ngono ni kitu cha asilia, na pia ni fumbo. Inaleta maumivu? Nitafika upeo wa raha ya ngono? Je, niingoje? Hakuna jibu sahihi na kila mtu huwa na uzoefu tofauti. Kwa simulizi za mapenzi kamili na simulizi za kusikitisha, soma hapa chini upate mambo wanawake wengine walioomba kufichwa majina yao halisi waliambia Find My Method kuhusu mara yao ya kwanza kufanya ngono.
………………………………………………………………………………………………………………………………………

Sikumbuki vizuri mara yangu ya kwanza kufanya ngono. Nilikuwa na miaka 18; Alikuwa kipenzi wangu wa kiume wa kwanza na tuliifanya kwa nyumba ya wazazi wangu. Kwa vile sikumbuki kisa hicho vizuri, naweza sema mambo mawili: Kwanza, haikuwa muhimu jinsi nilivyofikiria na ni kitu sikuwa nimepanga, sikupata nafasi ya kujitayarisha kwa chochote; Nilikuwa na kondomu kwenye begi langu na ujasiri wa kusema “ngoja, una kinga?”

 

Tendo la ngono huonekana ya mahaba sana kwenye filamu na vitabu na kwahivyo wanawake wengi husikitishwa wakikosa ngono yenye mahaba hivyo. Siku yangu ya kwanza ilikuwa shuleni, na nadhani haikuwa nzuri vile, lakini ikaendelea kuwa bora zaidi. Sasa hivi nafurahia maisha yangu ya ngono zaidi na ninafursa ya kujaribu vitu vipya kwa uhuru.

Usiruhusu siku ya kuanza ikufanye ukate tamaa.

Tasty Taco Jr

………………………………………………………………………………………………………………………………………

Siku yangu ya kwanza kufanya ngono ilikuwa siku chache baada ya kuhitimu umri wa miaka 30. Na pia sikuwa nimewahi jisaga kwahivyo sikujua cha kuhisi. Lakini nilikuwa nishasoma kwamba ni nzuri na watu huipenda.

Mwenzi wangu alikuwa mzuri sana. Tulikuwa tumejuana na kupendana muda mrefu na tulipo fanya ngono, tulikuwa na hisia nyingi za furaha – kupapasana na kubusiana, kujiona tukiwa uchi. Siku ya kwanza tulilala pamoja kitandani, tulikumbatiana tu na kuzungumza. Usiku wa pili tulijaribu; alikuwa na uzoefu na akaniongoza. Hakuingiza uume wake kwasabu uke wangu haukuwa na unyevu wa kutosha na mwenzi wangu akafika kilele na kumwaga nje. Ninakumbuka aliuliza “naweza mwaga juu ya mwili wako?” alimaanisha ikiwa angemwaga juu ya mwili wangu au kama nilitaka afanye hivyo kwenye tishu) na nilichanganyikiwa kwasababu hata sikuwa najua lugha ya ngono- ‘Kumwaga’ ni nini? Tulizungumza kwa muda mfupi mimi nikijifanya nilijua alichokuwa akizungumzia, na yeye akieleza kile alitaka kufanya.

Kwa ufupi, kulikuwa na mate mingi na jasho mingi lakini hakukuwa na hisia kali kama cheche. Lakini sikuwa na wasiwasi na bado mimi huipenda huo wakati.

Great Bloomer 

………………………………………………………………………………………………………………………………………

Back view of sexy millennial couple lying on bed hugging and kissing during early weekend morning at home, loving husband embracing wife enjoying romantic moment, relaxing in bedroom together

………………………………………………………………………………………………………………………………………
Nilikuwa na miaka 21 (mzee kabisa) na nilifanya ngono na rafiki wangu; kila kitu kilikuwa cha kutatanisha na kuenda haraka sana. Alifika kilele (hakika) na mimi sikufika. Haikufurahisha hata kidogo na sikupata raha yoyote. Pengine ni kwasababu nilikuwa nimevaa nguo refu sana na nilikuwa nimelewa sana. Lakini nilikuwa na uhakika kwamba ningependa kujaribu tena. 

SexMex

………………………………………………………………………………………………………………………………………

Mara yangu ya kwanza ilikuwa ya kushangaza kwasababu ni jambo sikujua lolote kuhusu ama jinsi ya kuanza. Nilikuwa na miaka 20 na ilifanyika siku yangu ya kuzaliwa. Ilikuwa na mpenzi wangu wa maisha; uhusiano wetu ulikuwa wa kujaliana na wa furaha kwani tulipendana. Kile nilichokiogopa ni kushika mimba.

Tulifanya ngono mara ya kwanza nyumbani kwake na ilikuwa nzuri sana. Unyegereshano huo ulikuwa mojawapo wa vitu vizuri vimewahi kufanyika maishani mwangu. Wakati huo, hatukutimia kinga, sikujua mambo ya upeo wa raha ya ngono wakati huo lakini yeye alijua kwasababu alikuwa na umri mkubwa kunishinda. Ilienda hadi karibu saa moja; kulikuwa na mambo mapya alinionyesha hio siku.

Mwanzoni, niliogopa kwamba kitu kibaya kingefanyika; baada ya hayo nilihisi uchungu mdogo lakini wa kufurahisha. Nilijifunza kwamba ukitaka kufanya ngono mara ya kwanza, ni bora muwe munapendana na muwe kama marafiki wa karibu kabla ya kufanya ngono.

Lulu

………………………………………………………………………………………………………………………………………

Sexy lovers kissing and playing in bed

………………………………………………………………………………………………………………………………………

Dah! Hio ilikuwa siku! Siku yangu ya kwanza kufanya ngono nilikuwa na miaka 20. Ilikuwa na kipenzi wangu wa kiume, ambaye sasa hivi ni mume wangu, kwa bahati nzuri. Hatukupanga kuifanya, na mara ya kwanza tulifikiria tu kunyegereshana kwasababu niliogopa uchungu na nilikuwa na wasiwasi.

Alikuja nyumbani kwangu wakati niko peke yangu. Tulikaa pamoja kwa masaa kadha, tukanywa divai alafu tukaanza kuambiana vile vitu tulipenda kwa mwingine. Ilikuwa wakati wa mahaba sana na akaanza kunigusa na kunibusu na nilihisi vizuri sana.

Alifinya matiti yangu, akazinyonya, akacheza na chuchu zangu, akanigusa huko chini na unyegereshano huu ulinisisimua sana! Ilikuwa vigumu kwetu kudhibiti hisia zetu na tukaanza kufanya ngono. Alikuwa juu yangu na tulifurahia sana, na alichomoa uume wakati alipofika kilele ili kunikinga.

Sikumbuki ikiwa nilifika upeo wa raha ya ngono, Nadhani nilifika lakini kile nakumbuka vizuri ni kuwa tulikuwa na ngono nzuri sana! Tulihisi tumetulia na wenye furaha sana! Kitu bora zaidi ni kuwa alinibusu kwenye paji la uso tulipomaliza.

Kile ningependa kuambia warembo wote huko nje na pia kwa wanaume wote ni kwamba ilukuwa mara yangu ya kwanza lakini sikutokwa damu. Haimanishi sikuwa bikira wakati huo. Sio lazima msichana au mwanamke atokwe damu mara yake ya kwanza kufanya ngono! Katika nchi zingine, swala hili ni mwiko na halizungumziwi wazi. Wanawake wengine watatokwa damu mara ya kwanza wanafanya ngono, wakati wengine hawatatokwa damu,na hali zote mbili ni sawa kabisa. Tuwache mambo haya ya ‘ubikira’, pendaneni kabisa na mioyo yenu ya ndani. Ngono sio lazima iwe nzuri kabisa, lakini kwa mazoea na kujaribu vitu vipya, italeta furaha.

Aphrodite

………………………………………………………………………………………………………………………………………

Sexy legs on lesbian couple in the bed

………………………………………………………………………………………………………………………………………

Siku yangu ya kwanza kufanya ngono ilikuwa tulivu. Nilikuwa na miaka 17 na ilikuwa kipenzi wangu wa kiume wa kwanza. Tulisafiri kufanya ngono mara ya kuanza na ilienda dakika kama moja, haha. Ningependa watu wajue kwamba mara ya kwanza ni ya kupata uzoefu na kutambua hisia zenu, wala sio ya kupata furaya ya ngono. Ngono ni kitu tunaweza kujifunza na kuboresha polepole.

HotGirl 

………………………………………………………………………………………………………………………………………

Kwa bahati nzuri mara yangu ya kwanza ilikuwa na mtu niliyempenda; nilikuwa na miaka 19 na nilikuwa nafikiria kila mtu alikuwa ashafanya mara ya kwanza. Kwahivyo firika kuwa ni mimi nilikuwa nimebaki (kati ya marafiki wangu) ilichangia kunisukuma kuifanya.

Ilikuwa mara yake ya kwanza pia (aliniambia hivyo); pengine ilikuwa uongo, lakini kwa hakika tulitumia kondomu.

Kitu ambacho nahisi hakikukua sawa ni kwamba kulikuwa kwenye lodging, kwasababu sote wawili tulikuwa tunaishi na familia zetu na haingewezekana kuifanya nyumbani. Kwahivyo tulikosa kuenda shuleni na tukaenda kwenye lodging.

Naona nilikuwa na bahati nzuri kwasababu sikuhisi uchungu sana; Wanawake wengine huniambia kwamba walihisi uchungu sana.

Na pia sikufika upeo wa raha wa ngono, lakini bado nilifurahia. Ukweli ni kwamba tulijua staili za kufanya kutokana na filamu za ponografia, kwani ni kwa njia gani ingine tungejua?

Nilifurahi sana baada ya hapo kwasababu ilikuwa na mtu niliyempenda sana na pia niliweza kufanya kile kila mtu alikuwa akizungumzia. Ningependekeza kwa mtu yeyote anayetaka kufanya ngono mara ya kwanza kwamba uifanye na mtu unayemwamini na unaweza kusema kile unachokipenda na kile hukipendi,. Pia ikiwa mtaambukizwa magonjwa ya zinaa au upate mimba usiyotaka, unajua kwamba hauko peke yako na una mtu wa kusimama nawe.Hakika tuliwachana na hatuna uhusiano wowote sasa, lakini sijuti.

Femme Fatale from Space

………………………………………………………………………………………………………………………………………

Beautyful sensual couple in love standing semi nude embracing and kissing each other. Man hugging her passionately over her back

………………………………………………………………………………………………………………………………………

Nilipofanya ngono mara ya kwanza, nilikuwa na miaka 17, na ilikuwa na kipenzi wangu wa kiume wa wakati huo; alikuwa na miaka 18. Tulikuwa tunapendana sana wakati huo. Uhusiano wetu ulienda miaka 3 na ulikuwa mchanga, nzuri na yenye mahaba. Tulikuwa tunapendana sana, nafirkiri mapenzi hayo yalizidi umri zetu.

Alikuwa mpole; unyegereshano uliendelea kwa muda mrefu,na hilo ndicho kitu pekee tulifanya kabla tufanye tendo lenyewe. Na tulipoenda zaidi ya unyegereshano, alifanya polepole sana hata siku hisi kama tulikuwa tunafanya ngono.

Ngono ni jambo muhimu kwangu. Wakati huo, sikuona umuhimu wake. Tukiwa na umri wa miaka 17, tunafikiria kwamba kipenzi wetu wa wakati huo ndiye tukakuwa naye millele, na tutaoana na kuishi pamoja milele. Hili ni aina ya penzi changa, na pia ni penzi nzito na yenye nguvu. Nafurahi kwamba niliifanya na mtu niliyempenda na yeye pia alinipenda. Tulikuwa vijana na wajinga na hatukutumia kinga, au siwezi kukumbuka… na pia sote tulifika kileleni; Ilikuwa mzuri sana kwangu na sikuhisi uchungu. Nilifurahi sana.

Na pia, ingekuwa naweza kurudisha saa nyuma, nadhani singeifanya nikiwa na miaka 17. Ningengoja, na kuifanya mara ya kwanza na kipenzi wangu wa kuime wa sasa.

Divine Orisha

………………………………………………………………………………………………………………………………………

Mimi hufikiria mara yangu ya kwanza na shukrani, hata ikiwa siko pamoja na huyo mtu sasa. Haikunitia hofu; ilikuwa na hisia za mapenzi. Lakini pia nilihisi uchungu, na nafikiria tunastahili kuzungumzia hayo. Uko hapo, mara ya kwanza wa uume kuingizwa kwako,- dah! Itakuwa chungu na utatokwa damu, lakini ikuwa ni mtu anayekuheshimu na kukujali, itakuwa bora.

Missy Miss

………………………………………………………………………………………………………………………………………

Je, una jambo la kusema? Wacha ujumbe wako hapa chini, wasiliana nasi kwenye kurasa zetu za mitandano ya kijamii: Facebook, Instagram na Twitter au tutumie barua pepe kwenye info@findmymethod.org. Kwa taarifa zaidi kuhusu njia za uzuiaji mimba, tembeleat findmymethod.or