Sheria na Masharti

Tovuti hii inakabiliwa na sheria, masharti na ilani tofauti, kwa kutumia Huduma, unakubali Sheria na Masharti yote, bonyeza hapa.
Sheria na Masharti

 

Kwa ujumla

findmymethod (www.findmymethod.org) inamiliki na kuendesha tovuti hii. Nyaraka hii inaongoza uhusiano wako na www.findmymethod.org (“Tovuti”). Upatikanaji na utumiaji wa Tovuti hii na habari- picha, maandishi na video zinazopatikana katika Tovuti hii (ambazo kwa ujumla zinaitwa “Huduma”) zitatawaliwa na Vigezo, Masharti na notisi (“Masharti za Huduma”) zifuatazo.

Kwa kutumia huduma hizi, unakubali Masharti za Huduma, jinsi tutakavyo yasasisha mara kwa mara. Unastahili kuangalia ukurasa huu mara kwa mara kuona kama kuna mabadiliko tumeweka kwenye Masharti ya Huduma.

Tuna haki ya kutoa au kubadilisha Huduma bila kukupa ilani. Hatuta wajibika kisheria ikiwa kwa sabubu yoyote Tovuti hii haitapatikana wakati wowote kwa muda wowote. Mara kwa mara, tunaweza kuzuia upatikanaji wa sehemu ya Tovuti au Tovuti hii yote.

Tovuti hii inaweza kujumuisha viungo vya tovuti zingine (“Tovuti Zilizounganishwa”) ambazo haziendeshwi na www.findmymethod.org. Tovuti hii haina udhibiti kwa Tovuti Zilizounganishwa na haitawajibika kwa ajili zao au kwa hasara au uharibifu unayoweza kupata kwa kuzitumia. Utumiaji wako wa Tovuti Zilizounganishwa utatawaliwa na masharti ya matumizi na huduma zilizo kwenye tovuti hizo.

 

Sera ya Faragha

Sera yetu ya Faragha, ambayo inaongoza jinsi tutatumia taarifa yako ya kibinafsi, inaweza kupatikana katika www.findmymethod.org/privacy-policy. Kwa kutumia Tovuti hii,unakubali yalio humo ndani na kukubali kwamba data zote ulizopeana ziko sahihi.

 

Makatazo

Ni sharti usitumie Tovuti hii vibaya. Hauruhusuwi: Kutenda au kuhumiza uhalifu; Kuambukiza au kusambaza virusi vya kompyuta, trojan, worm, logic bomb au kitu chochote kibaya, na kilio na uharibufu wa kiteknolojia, kwa kuvunja uaminifu ama kwa njia yoyote ya kukera na kuchukiza; Kudukua kipengele chochote cha Huduma; kuharibu data;kukasirisha watumiaji wengine; kukiuka haki za wamiliki za mtu mwingine; Kutuma matangazo au habari za matangazo ambayo hajaombwa,ambayo kwa kawaida hujulikana kama “spam”; au kujaribu kuathiri utendaji na utendakazi wa vyombo vya kompyuta vya Tovuti hii au vilivyo fikiwa kupitia Tovuti hii. Kuenda kinyume na amri hii itakuwa hatia na www.findmymethod.org itashtaki hatia kama hii kwa mamlaka za kutekeleza sheria na kufichua utambulisho wako kwao.

Hatutawajibika kisheria kwa hasara au uharibifu utakaotokana na ushambulizi wa kimtandao unaoitwa distributed denial-of-service attack, virusi vya kompyuta au vitu vinginge haribifu kiteknolojia, programu za kompyuta, data au vitu vingine unavyomiliki kwasabu ya kutumia tovuti hii au kwa kupakua chochote kulichochapishwa humu, au tovuti yoyote iliyo unganishwa nayo.

 

Haki za uvumbuzi, Programu na Maudhui

Haki za uvumbuzi kwa programu na maudhui zote (ikijumuisha picha) utakazozipata kwenye Tovuti au kupitia Tovuti hii zitabaki mali ya www.findmymethod.org au watoaji leseni wake na zitalindwa na sheria za hakimiliki za sehemu mbalimbali duniani. Haki kama hizi zote zitahifadhiwa na www.findmymethod.org na watoaji lesini wake. Unaweza kuweka, kuchapisha na kuonyesha maudhui yaliomo kwa matumizi yako ya kibinafsi pekee. Hauruhusiwi kuchapisha, kubadilisha, kusambaza au vinginevyo kunakili, kwa muundo wowote, maudhui yoyote au nakala ya maudhui uliyopewa au yaliomo kwenye Tovuti hii wala huwezi kutumia maudhui kama hizi kwa kufanya biashara yoyote.

 

Ilani ya kujitoa hatiani kisheria

Maudhui yote na nyenzo zote kwenye tovuti hii zinakusudiwa kutoa habari ya jumla, mazungumzo ya jumla na elimu pekee. Maudhui inatolewa ‘ilivyo” na utumiaji wako au utegemezi wako kwao uko juu yako mwenyewe.

Kamwe, kwa hali yoyote ile, www.findmymethod.org haitawajibika kwa hasara au uharibufi wa aina yoyote, ikiwemo jeraha la kibinafsi, iliyosababishwa na maudhui iliyochapishwa kwenye Tovuti au mahusiano kati ya watumiaji wa Tovuti, iwe mtandaoni au nje ya mtandao.

 

Kuunganisha Tovuti hii

Unaweza kuunganisha ukurasa wetu wa mwanzo, bora tu ufanye hivyo kwa njia iliyo ya haki na halali na ambayo haita haribu sifa yetu au kujinufaisha nayo, lakini ni sharti usiunde kiungo ambacho kitaonyesha uhusiano, kibali au udhibitisho kutoka kwetu wakati haipo. Ni sharti usiuende kiungo kutoka kwa tovuti ingine ambayo haimilikiwi na wewe. Tovuti hii isiwekwe kwenye tovuti ingine, wala usiunde kiungo cha sehemu yoyote ya Tovutii hii isipokuwa ukurasa wa mwanzo. Tunahifadhi haki ya kukunyang’anya rusa ya kuunganisha bila ilani.

Ilani ya kujitoa hatiani kisheria kwa umiliki wa alama za biashara, picha za watu mashuhuri na hakimiliki ya mtu wa tatu
Isipokuwa kama kinyume kitaelezewa wazi, watu wote (pamoja na majina na picha zao), alama za biashara na maudhui, huduma na/au maeneo ya washirika wengine yaliyopo kwenye Tovuti hii hayahusishwi, unganishwi au shirikishwi kwa nji yoyote na www.findmymethod.org na haufai kutegemea kuwepo kwa uhusiano au ushirikiano kama huo. Alama za biashara/ majina yoyote yaliyonyeshwa kwenye tovuti hii zinamilikiwa na wamiliki husika. Mahali alama ya biashara au jina la rajamu litatajwa, itakuwa tu kufafanua au kutambulisha bidhaa na huduma hizo wala sio ishara kwamba bidhaa na huduma hizo zinapendekezwa au kuhusishwa na www.findmymethod.org.

 

Fidia bima

Unakubali kulipa, kulinda na kuchukulia kuwa sio ya kudhuru www.findmymethod.org, wakurugenzi, maafisa, wafanyakazi,washauri, maajenti na washirika wake, kutokana kwa madai, madeni,uharibifu na /au gharama (pamoja na ada ya kisheria na mengine)iliyosababishwa na matumizi yako ya Tovuti hii au ukiukaji wako wa masharti za huduma.

 

Badiliko

www.findmymethod.org itakuwa na haki kwa hiari yake, wakati wowote na bila kutoa ilani, kurekebisha, kutoa au kubadilisha Huduma na/ au ukurasa wowote wa Tovuti hii.

 

Ubatilifu

Ikiwa sehemu yoyote ya Masharti ya Huduma haitaweza kutekelezwa (hata kwenye sharti lolote ambalo linatenga uwajibikaji wetu kwako), hili halitaathiri utekelezaji wa sehemu ingine yoyote ya Masharti ya Huduma.Masharti mengine yote yatatekelezwa na kutumika kamili.Kadri inavyowezekana, ikiwa kifungu/ kifungu kidogo au sehemu yoyote ya kifungu/kifungu kidogo kinaweza kutolewa ili kuhalalisha sehemu iliobaki, kifungu chote kitafasiriwa ifaavyo. Vinginevyo, unakubali kwamba kifungu kitarekebishwa na kufasiriwa kwa njia inayokaribia kabisa maana halisi ya kifungu/kifungu kidogo jinsi ilivyokubaliwa na sheria.

 

Malalamiko

Tuna taratibu ya kushughulikia malalamiko ambayo tutafuata kujaribu kutatua mizozo wakati yanaibuka, tafadhali tujulishe ikiwa una malalamiko au maoni yoyote.

 

Msamaha wa madai

Ukikiuka masharti haya na tusikuchukulie hatua, bado tuna nafasi ya kutumia haki zetu na sheria katika hali yoyote ingine utakayo kiuka masharti haya.

 

Makubaliano yote

Masharti ya Huduma hapo juu, inajumuisha makubaliano yote ya washiriki na itatumika katika nafasi ya makubaliano yoyote au yote yatakayo afikiwa baadaye na yatakayokuwa wakati mmoja na huu, kati yako na www.findmymethod.org. Msamaha wowote wa madai kwa sharti yoyote ya Masharti ya Huduma itafanya kazi tu ikiwa kwa maandishi na kutiwa saini na Mkurugenzi www.findmymethod.org.