1. SISI NI NANI & WIGO WA SERA HII:
Find My Method (inayojulikana kama ‘Shirika’ au ‘Sisi’) ni shirika lisilo la faida linaloendesha jukwa la kidijitali linalojumuisha tovuti na teknolojia zinazohusiana. Dhamira yetu ni kuwapa watu ulimwenguni kote taarifa sahihi na zilizoandaliwa kuwafaa binafsi kuhusu njia za uzuiaji mimba, na kuwawezesha kushiriki ngono salama, kuzuia mimba zisizotarajiwa, na kufanya uchaguzi huru wa ngono na afya ya uzazi.
Jukwa hii ya kidijitali, inayojulikana kama ‘Mfumo,’ inakusanya taarifa zinazoweza kumtambulisha mtu (PII) kutoka kwa Watumiaji, ambazo hujumuisha watu binafsi wanaohusishwa na Shirika kama vile wafanyakazi, wakandarasi huru, na waombaji kazi (wanaojulikana kama ‘Watumiaji’). Sera hii ya Faragha inaangazia aina za PII tunazokusanya na kueleza haki zinazohusu PII tunazozikusanya.Ingawa Shirika linamiliki na kudhibiti vipengele vingi vya Mfumo, utendakazi fulani hutolewa na Watoa Huduma Wengine ili kuimarisha ufanisi wake.
Tumeunda na tunatii Sera hii ya Faragha ili kulinda faragha ya Watumiaji.
2. MABADILIKO KWA SERA HII NA NOTISI ZA ZIADA ZA FARAGHA
Tunadumisha haki ya Kubadilisha Sera hii ya Faragha katika siku zijazo. Watumiaji hawatajulishwa kuhusu mabadiliko madogo ambayo hayaathiri maslahi yao ya faragha, kama vile uboreshaji wa ulinzi wa faragha, urekebishaji wa makosa ya herufi, au uongezaji wa taarifa zisizo muhimu. Kwa mabadiliko yoyote makubwa, tutawajulisha Watumiaji kupitia majukwa yaliyotajwa. Ikiwa Mtumiaji bado hajatoa anwani ya barua pepe halali, hatuwezi kumfahamisha kuhusu mabadiliko yoyote kwenye Sera hii. Sera hii ya Faragha inaweza kubadilishwa au kuongezwa kwa kuchapisha toleo jipya au notisi za faragha za ziada zinazotumika kwa mawasiliano maalum nasi. Notisi hizi zinaweza kuongezwa katika Sera hii, kuchapishwa kwenye tovuti ya Shirika, na/au kupatikana kivyao.
3. VIUNGO KWA TOVUTI ZINGINE
Sera hii ya Faragha haiendelei kutumika hadi kwa tovuti za watu wengine ambazo zinaweza kufikiwa kupitia viungo kutoka kwa Mfumo. Hatuwajibiki kwa maudhui, vipengele, utendakazi, au desturi za faragha za tovuti kama hizo zilizounganishwa au huduma. Ukusanyaji wa data na matumizi ya tovuti yoyote iliyounganishwa ya wahusika wengine inasimamiwa na notisi, taarifa au sera za faragha, pamoja na masharti yao ya matumizi, ilivyobainishwa na huyo mhusika wa tatu. Tunakuhimiza uzisome.
4. TAARIFA ZINAZOWEZA KUMTAMBULISHA MTU BINAFSI AMBAZO TUNAZIKUSANYA
Katika Sera hii ya Faragha, maelezo yote yanayoweza kumtambulisha mtu binafsi kwa pamoja yanaitwa “PII.” Tunakusanya anuwai mpana wa PII kutoka kwa Watumiaji, ambazo zinatofautiana kulingana na Mtumiaji na muktadha. PII inaweza kujumuisha:
- Jina
- Anwani ya barua pepe
- Nambari ya simu
- Anwani ya IP, mtoa huduma wa intaneti, aina ya kivinjari na lugha
- Eneo
- Majira ya Saa
- Lugha zilizotumika
- Umri, jinsia, picha za kibinafsi na taarifa zingine za kibinafsi ambazo Watumiaji hutoa kwa hiari
- Afya na haki za taarifa za ngono na uzazi zinazotolewa kwa hiari na mtumiaji, ikijumuisha maelezo na maswali kuhusu njia za uzuiaji mimba na ujauzito, sababu za kujihusisha na mfumo, pamoja na uwezo wao wa kupata na kufadhili huduma za afya ya uzazi.
- Hali ya ajira na taarifa kuhusu mwajiri
- Ushuhuda na ukadiriaji unaotolewa kwa kipengele chochote cha Mfumo
5. JINSI TUNAVYOKUSANYA TAARIFA ZAKO ZA KIBINAFSI
Tunaomba idhini yako kabla ya kukusanya PII, na kwa kuingia katika Mfumo, Watumiaji wanakubali (1) sheria na masharti yaliyoelezwa katika Sera hii ya Faragha na (2) ukusanyaji, utumiaji na uhifadhi wa taarifa wanazotoa na kwa Shirika na/au taarifa yoyote ambayo Mfumo inakusanya kutokana na teknolojia wanazozitumia.
Tunaweza kutumia mbinu zifuatazo kukusanya Taarifa za Kibinafsi:
- Michango ya hiari ya Watumiaji
- Shughuli za Watumiaji kwa sehemu yoyote ya Mfumo ikiwa ni pamoja na Watoa Huduma za Wengine
- Mazungumzo/ mawasiliano na Watumiaji
Tutaendelea kutafuta njia bora na salama za kukusanya PII na kurekebisha Sera ya Faragha ili kuonyesha mabadiliko yoyote.
6. TUNACHOFANYA NA TAARIFA ZAKO BINAFSI ZINAZOWEZA KUKUTAMBULISHA
Tunatumia PII tunazokusanya kwa njia zifuatazo:
- Kuwasiliana na Watumiaji, ikiwa ni pamoja na kutoa taarifa muhimu zinazohusiana na chaguo za uzazi
- Kuchanganua PII ili kuboresha huduma, bidhaa na thamani zetu
- Kutekeleza kazi za kiutawala za Mfumo na Shirika
- Kufanya Utafiti
- Kwa huduma za pamoja za kidijitali na mashirika mengine, kuwapa PII kuhusu wanachama wao
- Kwa juhudi za kuchangisha pesa, ambazo zinaweza kujumuisha kutoa muhtasari wa PII kwa mashirika yanayoweza kufadhili
- Kutoa PII kwa watekelezaji sheria, mamlaka mengine ya serikali, au wahusika wengine kama inavyotakiwa na sheria
Tunachukua hatua za busara na halali ili kuepuka kulazimishwa kufichua PII yako, lakini kuna wakati ambapo mahitaji ya kisheria hutulazimisha kutii. Kuhusu PII iliyokusanywa na/au kuhifadhiwa na Watoa Huduma Wengine, hatudhibiti matumizi yao na/au uhifadhi wa PII yoyote kama hiyo.
7. HAKI YAKO YA KUPATA, KUSAHIHISHA, KUDHIBITI, NA KUFUTA TAARIFA ZAKO BINAFSI
Watumiaji ambao PII zao tunamiliki wana haki zifuatazo:
- Kufikia na kupokea nakala za PII zao
- Kupokea maelezo ya jinsi tulivyopata na kutumia PII zao
- Kusahihisha au kufuta PII zao
- Kubadilisha jinsi tunavyotumia PII zao
Ili kutekeleza haki hizi, ni lazima Watumiaji watupe anuani ya barua pepe halali, inayoweza kuthibitishwa na wafuate maagizo yaliyowekwa hapa chini katika sehemu ya ‘JINSI YA KUWASILIANA NASI’. Kukosa kutoa anuani ya barua pepe halali, inayoweza kuthibitishwa kunazuia uwezo wetu wa kuthibitisha utambulisho wao na kutekeleza haki zao.
8. SERA YA FARAGHA NA MAZOEA KUHUSU WATOTO
Hatukusanyi taarifa kuhusu watu walio na umri wa chini ya miaka 13 kimakusudi. Mfumo wetu hauna maudhui yanayovutia mahsusi watoto au yanayoweza kuwaathiri vibaya, na sisi wenyewe kwa kujitegemea hatuthibitishi umri wa watumiaji wetu.Iwapo watumiaji watatoa PII kuhusu watu walio na umri wa chini ya miaka 13, tunashughulikia taarifa kama hizo kulingana na Sera hii ya Faragha. Tukifahamu kuwa tunawasiliana na mtu aliye na umri wa chini ya miaka 13, tutamjulisha kwamba idhini ya mzazi inahitajika.
9. USALAMA WA DATA YETU NA SERA NA MAZOEA YA UHIFADHI
Ili kulinda PII zako dhidi ya ufichuzi/matumizi yasiyoidhinishwa, tunachukua tahadhari zifuatazo:
- Kuelimisha wafanyakazi wetu, wawakilishi wetu, na Watoa Huduma Wengine kuhusu Sera hii ya Faragha
- Kuimarisha hatua zetu za usalama ili kuzuia ufichuzi usioidhinishwa na/au matumizi ya PII zako
Sera yetu ya jumla ni kufuta PII zote ndani ya mwaka mmoja baada ya tarehe iliyokusanywa. Walakini, hii haifanyiki kila wakati kwa sababu ya changamano ya Mfumo wetu.Zaidi ya hayo, sera yetu ya uhifadhi haitumiki kwa PII zilizokusanywa na/au kuhifadhiwa na Watoa Huduma Wengine. Pia tunafanya kazi ili kuhakikisha kwamba PII zote zilizokusanywa zimesimbwa kwa njia fiche wakati hazitumiki, ingawa si PII zote zimesimbwa kwa sasa.
10. UFICHUZI WETU WA “USIFUATILIE”
Hatushiriki katika kufuatilia watu binafsi kwenye tovuti za wahusika wengine kwa ajili ya utangazaji lengwa na hatujibu mawimbi ya Usifuatilie (DNT).
11. JINSI YA KUWASILIANA NASI KWA MAOMBI, MAONI, NA MASWALI
Kuwasiliana nasi kwa maombi, maoni na/au maswali, tafadhali tutumie barua pepe kwenye privacy@findmymethod.org. Kabla ya kufichua PII yoyote au kufanya mabadiliko yoyote, tutatumia anwani ya barua pepe iliyo kwenye faili ili kuthibitisha utambulisho wa mtu anayetuma ombi. Faragha yako ni muhimu sana kwetu.
Ikiwa Mtumiaji hatatupa anwani ya barua pepe halali, inayoweza kuthibitishwa, hatuwezi kuthibitisha utambulisho wake, na hii inatuzuia kuruhusu mtu yeyote kutumia haki zozote zinazohusiana na PII tunayomiliki.
12. USASISHAJI WA MWISHO
Sera hii ya Faragha ilisasishwa Agosti 2024. Tutasasisha Sera hii ya Faragha angalau mara moja kila miezi 12.